IGP SIRRO: Kuna mambo Kibiti hayazungumziki

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
99,400
2,000
IGP SIRRO: KUNA MAMBO KIBITI HAYAZUNGUMZIKI

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro, akisalimiana na viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro baada ya kufanya ziara jana. Picha na Ramadhan Libenanga

Na Ramadhan Libenanga – Morogoro
MTANZANIA

MKUU wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro, amesema mambo yanayotokea katika matukio ya mauaji ya mfululizo wilayani Rufiji, Ikwiriri na Kibiti mkoani Pwani, hawawezi kuyazungumzia hadharani kutokana na sababu za kiusalama.

Kauli hiyo aliitoa mjini hapa jana alipozungumza na waandishi wa habari wakati akitokea bungeni mjini Dodoma kusikiliza hotuba ya makadirio ya bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018 iliyosomwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango.

IGP Sirro alisema Jeshi la Polisi haliwezi kuyataja mambo hayo kupitia vyombo vya habari kutokana na mambo ya kiusalama na mikakati waliyojiwekea.

“Sio kila jambo la usalama linapaswa kutangazwa, hasa wakati huu wa operesheni ya kuwasaka wauaji hao.

“Kilichopo sasa ni kwamba polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama tunaendelea kuhakikisha hali ya amani inarudi maeneo ya Kibiti,” alisema.

Sirro alitoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja baada ya watu watatu kuuawa Kibiti kwa kupigwa risasi saa nane ya usiku wa kuamkia juzi.

Watu hao waliuawa katika Kijiji cha Nyamisati, ikiwa ni mwendelezo wa matukio ya mauaji mkoani humo yaliyotokea kwa kufuatana ndani ya kipindi cha wiki moja baada ya watu wengine wanne kuuawa, mmoja kutekwa na mwingine kujeruhiwa kwa risasi na kukimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wakazi wa Kibiti, wauaji hao waliwaua wanakijiji watatu; Hamid Kidevu, Yahya Makame na Moshi Machela na kutokomea na maiti zao kusikojulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga, aliliambia MTANZANIA Jumapili kwa simu jana kuwa licha ya juzi kutuma kikosi cha askari katika eneo la tukio kuwasaka wauaji hao na maiti hizo, lakini hadi sasa bado hazijapatikana.

Lyanga alisema bado hajapata taarifa yoyote ya ziada kuhusu tukio hilo.

“Sina taarifa mpya, taarifa ni zile zile kama nilizozitoa jana,” alisema Lyanga.

Mbali na taarifa hiyo ya Lyanga, naye Sirro alizungumzia mtindo mpya wa mauaji hayo yaliyotokea juzi baada ya maiti za wanakijiji hao kutopatikana kwa kusema kuwa polisi nao wanahakikisha wanafuatilia kwa ukaribu jinsi wauaji hao wanavyobadilisha mtindo wao wa kutekeleza uhalifu huo.

Pia alivitaka vyombo vya habari hapa nchini kuacha kuandika habari za uchochezi na kuwatia hofu wananchi wanaoishi maeneo ya Rufiji na Kibiti.

Alilalamika kuwa kuna baadhi ya vyombo vya habari vinaandika habari za mauaji hayo kwa lengo la kusherehesha vyombo vyao.

“Ndugu zangu wanahabari, Jeshi la Polisi linatambua kwa kiasi kikubwa mchango wenu katika kuelimisha jamii, hasa masuala mbalimbali yanayohusu nchi yetu, lakini imekuwa tofauti na habari za mauaji ya Kibiti zinavyoripotiwa katika vyombo vyetu si kizalendo,” alisema.

Siro alisema kuwa vyombo hivyo (sio MTANZANIA Jumapili) vimekuwa vikiripoti kuonyesha kama maeneo ya Rufiji, Kibiti na Ikwiriri ni uwanja wa vita na hali hiyo inawatia hofu waishio uko na wale wanaotamani kwenda kuishi.

Alisema wamekuwa wakishuhudia vyombo vya habari vikiripoti habari za Kibiti kwa kuonyesha watu waliojeruhiwa vibaya wakiambatanisha na silaha za kivita kitu ambacho ni kinyume na uhalisia.

Aliwakumbusha wanahabari kuwa wanapoandika masuala ya kiusalama, wanapaswa kuzingatia ukweli wa taarifa kutoka kwa vyombo husika, ikiwa pamoja na kutanguliza uzalendo ili kuepusha athari zinazoweza kutokea kutokana na taarifa zisizo na uchunguzi wa kina.

“Epukeni kuandika habari zenye sura ya ushabiki katika mauji ya Kibiti na maeneo mengine ili kuelimisha jamii,” alisema.

Tangu mauaji hayo yatokee inadaiwa kuwa watu takriban 38 wameshapoteza maisha.

Baada ya mauaji hayo kuendelea kutokea mfululizo mkoani humo, Rais Dk. John Magufuli, alifanya mabadiliko ya kumwondoa IGP Ernest Mangu katika nafasi hiyo na kumteua Sirro aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kuwa IGP mpya.

Baada ya kuteuliwa, Sirro aliweka mikakati ya kuwabaini wauaji hao na kuwachukulia hatua.

Siku nne zilizopita, Sirro alifika mkoani Pwani na kuzungumza na wazee ili kujua kiini cha mauaji hayo.
 
Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
35,277
2,000
Ni wakati sasa wa kukaa chini na kutafakari kuhusu haya matukio ili yapatiwe ufumbuzi, siasa zitamaliza watanzania
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Copenhagen DN

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
6,057
2,000
Ni wakati sasa wa kukaa chini na kutafakari kuhusu haya matukio ili yapatiwe ufumbuzi, siasa zitamaliza watanzania
watakapokuja kufanya Mumbai, Paris and Westgate style ndio watu watafunguka akili hao akina Sizonje na Mwigulu.

Hawa wapuuzi wanamikakati miovu kama mmoja tu kawauwa polisi 8 na kuiba bunduki je wa2 ama wa3 wavamie easy target kama kanisa msikiti ama sokoni, itakuwaje? Tukotuko tu nakufanya mzaha na usalama wa raia na mijitu iliyokariri hadi ikafika hadi chuo na kupata degree ya uchumi kubwabwaja hovyohovyo.

Be serious MNAKERA
 
Temu JR

Member
Jan 29, 2017
77
125
IGP SIRRO: KUNA MAMBO KIBITI HAYAZUNGUMZIKI

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro, akisalimiana na viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro baada ya kufanya ziara jana. Picha na Ramadhan Libenanga

Na Ramadhan Libenanga – Morogoro
MTANZANIA

MKUU wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro, amesema mambo yanayotokea katika matukio ya mauaji ya mfululizo wilayani Rufiji, Ikwiriri na Kibiti mkoani Pwani, hawawezi kuyazungumzia hadharani kutokana na sababu za kiusalama.

Kauli hiyo aliitoa mjini hapa jana alipozungumza na waandishi wa habari wakati akitokea bungeni mjini Dodoma kusikiliza hotuba ya makadirio ya bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018 iliyosomwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango.

IGP Sirro alisema Jeshi la Polisi haliwezi kuyataja mambo hayo kupitia vyombo vya habari kutokana na mambo ya kiusalama na mikakati waliyojiwekea.

“Sio kila jambo la usalama linapaswa kutangazwa, hasa wakati huu wa operesheni ya kuwasaka wauaji hao.

“Kilichopo sasa ni kwamba polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama tunaendelea kuhakikisha hali ya amani inarudi maeneo ya Kibiti,” alisema.

Sirro alitoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja baada ya watu watatu kuuawa Kibiti kwa kupigwa risasi saa nane ya usiku wa kuamkia juzi.

Watu hao waliuawa katika Kijiji cha Nyamisati, ikiwa ni mwendelezo wa matukio ya mauaji mkoani humo yaliyotokea kwa kufuatana ndani ya kipindi cha wiki moja baada ya watu wengine wanne kuuawa, mmoja kutekwa na mwingine kujeruhiwa kwa risasi na kukimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wakazi wa Kibiti, wauaji hao waliwaua wanakijiji watatu; Hamid Kidevu, Yahya Makame na Moshi Machela na kutokomea na maiti zao kusikojulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga, aliliambia MTANZANIA Jumapili kwa simu jana kuwa licha ya juzi kutuma kikosi cha askari katika eneo la tukio kuwasaka wauaji hao na maiti hizo, lakini hadi sasa bado hazijapatikana.

Lyanga alisema bado hajapata taarifa yoyote ya ziada kuhusu tukio hilo.

“Sina taarifa mpya, taarifa ni zile zile kama nilizozitoa jana,” alisema Lyanga.

Mbali na taarifa hiyo ya Lyanga, naye Sirro alizungumzia mtindo mpya wa mauaji hayo yaliyotokea juzi baada ya maiti za wanakijiji hao kutopatikana kwa kusema kuwa polisi nao wanahakikisha wanafuatilia kwa ukaribu jinsi wauaji hao wanavyobadilisha mtindo wao wa kutekeleza uhalifu huo.

Pia alivitaka vyombo vya habari hapa nchini kuacha kuandika habari za uchochezi na kuwatia hofu wananchi wanaoishi maeneo ya Rufiji na Kibiti.

Alilalamika kuwa kuna baadhi ya vyombo vya habari vinaandika habari za mauaji hayo kwa lengo la kusherehesha vyombo vyao.

“Ndugu zangu wanahabari, Jeshi la Polisi linatambua kwa kiasi kikubwa mchango wenu katika kuelimisha jamii, hasa masuala mbalimbali yanayohusu nchi yetu, lakini imekuwa tofauti na habari za mauaji ya Kibiti zinavyoripotiwa katika vyombo vyetu si kizalendo,” alisema.

Siro alisema kuwa vyombo hivyo (sio MTANZANIA Jumapili) vimekuwa vikiripoti kuonyesha kama maeneo ya Rufiji, Kibiti na Ikwiriri ni uwanja wa vita na hali hiyo inawatia hofu waishio uko na wale wanaotamani kwenda kuishi.

Alisema wamekuwa wakishuhudia vyombo vya habari vikiripoti habari za Kibiti kwa kuonyesha watu waliojeruhiwa vibaya wakiambatanisha na silaha za kivita kitu ambacho ni kinyume na uhalisia.

Aliwakumbusha wanahabari kuwa wanapoandika masuala ya kiusalama, wanapaswa kuzingatia ukweli wa taarifa kutoka kwa vyombo husika, ikiwa pamoja na kutanguliza uzalendo ili kuepusha athari zinazoweza kutokea kutokana na taarifa zisizo na uchunguzi wa kina.

“Epukeni kuandika habari zenye sura ya ushabiki katika mauji ya Kibiti na maeneo mengine ili kuelimisha jamii,” alisema.

Tangu mauaji hayo yatokee inadaiwa kuwa watu takriban 38 wameshapoteza maisha.

Baada ya mauaji hayo kuendelea kutokea mfululizo mkoani humo, Rais Dk. John Magufuli, alifanya mabadiliko ya kumwondoa IGP Ernest Mangu katika nafasi hiyo na kumteua Sirro aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kuwa IGP mpya.

Baada ya kuteuliwa, Sirro aliweka mikakati ya kuwabaini wauaji hao na kuwachukulia hatua.

Siku nne zilizopita, Sirro alifika mkoani Pwani na kuzungumza na wazee ili kujua kiini cha mauaji hayo.
Bado nina imani na jeshi la polisi! Jeshi letu lipo imara, ila kwa hili linaloendelea huko Kibiti mnaonekana kama mnarudi nyuma sana! Haiwezekan kila baada ya siku kadhaa mauaji yatokee na wauaji wapo huko huko. Mbaya zaidi wanapiga hadi polisi wetu bila huruma!! Wakati jeshi linaendelea kuwasaka wauaji, nashauri pia kuwe na mkakati wa kujua kiini cha haya mauaji! Bila kujua kiini chake tunaweza tukawa tunatwanga maji, na tukawakamata wauaji ila tukashangaa tatizo haliishi. Inteligensia ifanye kazi to the maximum, this is too much! Watz wanataka waendelee na maisha yao bila kubugudhiwa, hata kama ni magumu poa tu!
 
Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
10,686
2,000
Ikiwa inteliensia upinzani faster utasikia yule Mama Msemaji wao amekuja na conclusion harak sana!!! Hii naona wametoa matamko hadi yamewaishia!!! Jeshi la mihemko......hamna kitu hadi mkiacha upuuzi wenu wa kutawaliwa na wanasiasa uchwara!!! Weledi uwepoo ndio heshima itarudii.....
 
jamvimoto

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
700
500
Ushauri kwa polisi inteligensia yanu ifanyeni siri
Mkipewa habari wahusika ni biongozi wacuf msiende kukamama viongozi wa cuf tuhii inampa point adui kwani viongozi na wafuasi huanza kumsabikia adui na polisi kukosa ushirikiano kwa viongozi na wafuasi wao ili kuficha siri na hatua mlizo fikia katika upelezi wenu kamateni Pia chadema,ccm na vyama vingine lakini mkiijua target yenu hii haitavunja umoja miongoni mwa wananchi.
Vilevile wakitajwa viongozi wadini fulani wewe chukuwa viongozi wa dini site wahojini lakini mkijua target yenu, hii ina faida mbili kwanza kumdanganya adui kuwa mko karibu ya kupata ukweli, pili kuto leta matengano miongoni mwa jamii.
Itakuwaje wavamizi wapige na kuacha maiti ago Leo wapige na kuchukua maiti.nani kaproove kuwa aliyepigwa kafa au kajeruhiwa muwe lakini huenda wanawaondoa kiaina watu muhimu katika uchunguzi wenu.
mawazo yangu tu
 
kakaye

Member
Jul 21, 2016
87
125
Kuchukia polisi ni kufurahia mauji kwa ndugu zetu toa ushirikiano tafadhali kumbuka wewe ni mtanzania
 
areafiftyone

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
7,387
2,000
Bado nina imani na jeshi la polisi! Jeshi letu lipo imara, ila kwa hili linaloendelea huko Kibiti mnaonekana kama mnarudi nyuma sana! Haiwezekan kila baada ya siku kadhaa mauaji yatokee na wauaji wapo huko huko. Mbaya zaidi wanapiga hadi polisi wetu bila huruma!! Wakati jeshi linaendelea kuwasaka wauaji, nashauri pia kuwe na mkakati wa kujua kiini cha haya mauaji! Bila kujua kiini chake tunaweza tukawa tunatwanga maji, na tukawakamata wauaji ila tukashangaa tatizo haliishi. Inteligensia ifanye kazi to the maximum, this is too much! Watz wanataka waendelee na maisha yao bila kubugudhiwa, hata kama ni magumu poa tu!
Hongera mkuu kama bado una imani na jeshi la Polisi.In it's current state nadhani unahitaji kuwa hypocrite kuwa na imani nalo.Linahitaji complete overhaul.
 
bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
9,283
2,000
Naunga mkono kauli za IGP na Kamanda wa Mkoa RPC kuhusu "waandishi" ktk media kutafuta kiki ktk media wanazomiliki iwe blogs, account za youtube n.k kubandika picha zisizo na uhalisia wa matukio ya mkoani Pwani.

Mfano utaona watafuta " "views" kwa udi na uvumba ktk blogs, youtube na website zao za ki-Tanzania kuna picha za magaidi wa Somalia, Nigeria na Mindanao- Ufilipino ktk "kuhabarisha, kukoleza na kutia chumvi" matukio yaanayotokea Tanzania sehemu za Ikwiriri, Mkuranga na Rufiji.

Wana-media za kijamii, Kuweni kama Jamiiforums ambapo mfano mdau BAK anaweka uzi bila "vikolombwezo" visivyo na uhalisia na bado wasomaji wengi tu wanaufuatilia uzi kwa views kibao na kuweka comments zao.
 
mwayungi

JF-Expert Member
May 9, 2017
1,773
2,000
R.I.P kaka PC fulani maana walimuua kweny3 hiyo ambush mungu awasamehe wauaji wote
 
NAKWEDE

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
28,019
2,000
Mkulu hataki watu watumishi ambao sio waadilifu. Inasemekana amempuzimsha huyo kaka baada ya kugundua kuwa alikuwa anataka kubadili sare za jeshi lile, pia benki ana shilingi za kitanzania bilioni tatu ambazo wanahisi amezipata sio kwa njia za halali, na hapa Mwanza ana hoteli kubwa kubwa kidogo iko barabara ya kwenda airport pale Iloganzala inaitwa ADEN
 
Wong Fei

JF-Expert Member
Apr 13, 2016
3,931
2,000
Angekuwa YOHANE PONDAMALI MAGUGU AU BASHITE ANGESEMA HADHARANI MAANA HASA WASHAZOEA KUROPOKA
 
Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,006
2,000
Iyo ni kweli ila kuna bingwa la maropokaji alishtoa siri kuwa jezi za jesh zilizokamatwa zinausishwa na mauwaji ya kibiti..
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom