IGP Sirro aongezewa mwaka mmoja kuongoza EAPCCO

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,188
4,100
Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki Mwa Afrika (EAPCCO) wamemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Shirikisho hilo kwa kipindi kingine cha mwaka mmoja.

Uamuzi huo umetolewa leo na nchi 14 wanachama wa Shirikisho hilo kupitia mkutano wake mkuu wa mwaka uliofanyika kwa njia ya mtandao (video conference) ambapo Wakuu hao waliona kutokana na kuibuka kwa ugonjwa wa Corona kumesababisha mambo mengi ya shirikisho hilo kutokamilika kwa wakati.

Hata hivyo IGP Sirro amesema kuwa, hadi sasa Shirikisho hilo limepata mafanikio makubwa huku akieleza kuwa katika kipindi cha 2021 wamejipanga kutekeleza yale ambayo hayakuweza kufikiwa na watahakikisha kuwa nchi wanachama wanaweza kubadilishana uzoefu na kufanya mafunzo ya pamoja ya mbinu za medani.
1600421272569.png
 
1. Ameshindwa kuwakamata waliompiga Lissu lisasi.
2.Hajui alipo saanane , Anzory na wengineo.
3.Hajui kikundi cha wasiojulikana.
4. Ameshindwa kuwabaini waliomteka Roma, Mo , Mdude , Msaidizi wa Membe na wengineo wengi.

Jamaa alikuwa na Heshima kubwa sana ndani Ila imepungu kwa kasi sana

Hongera sirro
 
1. Njaa yake imetoka tumboni imehamia kichwani.

2.Maagizo kutoka juu.
 
Back
Top Bottom