IGP Mwema apeleka makachero Arumeru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IGP Mwema apeleka makachero Arumeru

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 1, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema


  Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema, ameunda timu maalum ya operesheni na upelelezi kuongeza nguvu kwa polisi wa Mkoa wa Arusha pamoja na timu ya wataalamu iliyoundwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, kuchunguza vurugu za uvamizi wa mashamba ya wawekezaji wilayani Arumeru kunakofanywa na mamia ya wananchi wilayani humo.

  Naibu Kamishina wa Polisi kutoka makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam, Isaya Mngulu, alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa juzi jioni.

  “Inspekta Jenerali wa Polisi ameunda timu maalum kutoka makao makuu ya polisi kuja kuongeza nguvu na kuhakikisha wahusika wa vurugu hizo wanakamatwa,” alisema na kuongeza timu hiyo itashirikiana na maofisa wa ngazi mbalimbali wilayani Arumeru na mkoani hapa.
  Hata hivyo, Mngulu hakusema idadi ya watu wanaounda timu hiyo, lakini alisema itakuwa chini ya uongozi wake na kwamba itaendelea kufanya kazi wilayani humo kwa muda usiojulikana hadi hapo itakapopata tija.

  “Tunataka kusaidia ili mafanikio yapatikane mapema na kurejesha eneo hili katika hali yake ya utulivu…tunatoa wito kwa wananchi ambaye ana taarifa kuhusu vitendo hivi vya uvunjifu wa amani ambavyo vimetokea wasisite kutoa taarifa za siri kwa polisi, mkuu wa mkoa, watendaji wa kata au makatibu tawala wa wilaya na mkoa,” alisema.

  Mapema wiki iliyopita, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, aliunda timu ya wataalam watano ili kufanya uchunguzi na kuyapatia ufumbuzi matatizo ya uvamizi yaliyofanywa katika shamba la Dolly Estate Ltd, linalomilikiwa na mwekezaji wa kigeni Jerome Bruins.
  Akizungumzia uvamizi huo wa mashamba, Mngulu alisema wawekezaji wanamiliki maeneo hayo kisheria hivyo utawala wa sheria unataka kila mtu

  atii, hivyo kwenda kinyume cha hapo hatua za kisheria zitachukuliwa.
  Alifafanua kuwa zipo njia ambazo wananchi wanaweza kuzitumia kuwasilisha malalamiko yao serikalini ya kukosa maeneo suala ambalo likifanywa kisheria linaweza kumshawishi Rais kutengua umilikishwaji wa mashamba hayo badala ya kuvumia nguvu kwa kuvamia.

  “Watu hawaelewi kwamba tumeongezeka, hivyo ni vema sasa hivi wananchi wakafuata taratibu, kanuni na sheria za ardhi badala ya kuvamia na kusababisha wengine kupoteza maisha…ukienda mbali utaona hao wanaovamia si wote wana uwezo wa kuendeleza maeneo hayo,” alisema.

  Alisema sasa hivi watu wanawavamia wawekezaji lakini siku itafika wataanza kuvamiana wenyewe kwa wenyewe, hivyo ni vema wananchi wanaohitaji maeneo wakafuata utaratibu wa kisheria kutengua umiliki wake.
  Kwa upande wake Kamishina Msaidizi wa Polisi, Engelbert Kiondo, kutoka makao makuu ya polisi, ambaye ni mkuu wa kitengo cha Polisi Jamii, alisema wamekuja mkoani hapa kujua kitaalam kibisa kiini cha matatizo ya uvamizi huo ili waweze kupata tiba yake.

  “Kama kiini ni siasa au ardhi tunataka kujua hilo…siasa ndiyo inayotoa dira nani azalishe nini, amiliki nini na apate nini hivyo huwezi kukwepa siasa katika uvamizi huo,” alisema.

  Alisema wanatarajia kuwapa wananchi elimu ya kuchambua kauli mbalimbali za kisiasa zinazotolewa na viongozi wa siasa ili wasikurupuke na kufanya uvamizi.
  Wilaya ya Arumeru ina jumla ya mashamba makubwa 19 ya wawekezaji wa ndani na nje na kuanzia Aprili 15, mwaka huu, kumekuwa na mfululizo wa matukio ya uvamizi ambapo hadi kufikia jana mashamba matatu ya wawekezaji yamekwisha kuvamiwa na kusababisha uharibifu wa mali na miundombinu.

  SOURCE: NIPASHE

   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hii article imenipa hasira sana. Raia wanauwawa, wabunge wanashambuliwa na kuumizwa vibaya IGP na jeshi lake wako kimya, lakini shamba ya 'mwekezaji linavamiwa' haraka haraka IGP anaunda team ya kuchunguza! Watanzania hawana haki nchi hii? Waende wapi hata pale uhai wao unapokuwa mashakani?
   
 3. kinya

  kinya JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2012
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 483
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  binafsi nilivyo ona title nikadhani kwenda kuchunguza mauaji kumbe aarrrg MWEMA!
   
 4. papason

  papason JF-Expert Member

  #4
  May 1, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  For sure hao makachero wanaenda kuwauwa na ku wa intimidate wananchi wa arumeru na hasa wafuasi wa CDM!
   
 5. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2012
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Dah! Hata mie nimeona sikio la habari nikajua basi uchunguzi wa vifo..damn! Wameongeza hasira mara mbili kwa wananchi..
   
 6. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #6
  May 2, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hiyo mil. 10 kweli kuna mtu atajitokeza, usije kushangaa unajitokeza halafu inakula kwako.
   
 7. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #7
  May 2, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  yani kama vile ulikua na mimi...mara ya kwanza nilivyosoma anatuma makachero nikajua anatuma ili kwenda kuchunguza mauaji ya mwenyekiti wa chadema pale usa river..alaah kuja kusoma kwa undani eti kuchunguza kuvamiwa kwa ardhi na ukizingatia hiyo ardhi sio ya hao wazungu bali ni ya wana arusha wenyewe.....yaani hii nchi mhhh
   
 8. A

  Ahmada umelewa Member

  #8
  May 2, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani hii imeniuma Sana nilipoona kichwa nikafikiri mengine kumbe yaliyomo mengine, Wazungu wamathaminiwa sana.
   
 9. b

  bibi.com JF-Expert Member

  #9
  May 2, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 1,155
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  we still ve slave mind my dear!
   
 10. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #10
  May 2, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Naona jeshi linapoteza dira. kupitia kitengo cha cyber crime, wauaji wa mwenyekiti wangekuwa wamesha wekwa kiminyani, lakini wapi
   
 11. SIMBA WA TARANGA

  SIMBA WA TARANGA JF-Expert Member

  #11
  May 2, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 992
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao makachero uchwara wanaenda kula perdiem tu, na kuua wana CDM, ngojeni mtasikia tu mwingine kakatwa shingo.
   
Loading...