LiverpoolFC
JF-Expert Member
- Apr 12, 2011
- 11,498
- 3,390
police jamii
Natumia simu but thanx umetoa point zako msingimaswali ya msingi ya kujiuliza...........
1.hii taarifa ni nzito na inasikitisha kama ni kweli.
2.mbona mleta mada hajataja hata mtu mmoja katika hizo ofisi ambazo zinashiriana na hawa watu?mfano amtaje askari flani au afisa ardhi flani ili taarifa yake iwe na kitovu ie pahali pa kuanzia.
3.taarifa ni ya jumla mno kiasi kwamba inaelea,haina pakushika.
4.taja hata mwananchi mmoja alienyang'anywa ardhi/kiwanja chake ili asaidie hata kuwatafuta hao maafisa wa serikali wanaotumia ofisi zao kinyume na taratibu.
narudi tena mleta mada labda kachukuliwa demu wake na hao watu hakuna usibitisho hata moja tuamini vipi toa ***** wako
kama na wewe kweli ni afande, mweee..
Habari hii ni kweli kabisa. Wiki tatu nyuma walivamia kiwanja Mbezi beach maeneo ya Five Star na kuzungusha ukuta na kuleta walinzi. Nina habari mwenye kiwanja hakupata ushirikiano kabisa na polisi ya Wazo zilipo ofisi za OCD hivyo kwa msaada wa ofisi ya mwanasheria wake waliweza kupata amri ya kusimamisha ujenzi iliyotolewa na mahakama ya Ardhi na kesi itaanza karibuni. Katika uvamizi huo walitumia risasi za moto kumtisha the legal owner na majirani na hata baada ya ku report polisi hawakuchukua hatua yeyote. Habari ni kuwa tapeli mmoja papaa mfadhili wa bendi ndie kiongozi wa kundi lakini anawatumia wasaidizi wake kuongoza uhalifu huu kwa kuwa ameshaonywa karibuni na baadhi ya viongozi wa Polisi na hajatii alichoonywa. Naomba ifahamike kabisa hutapata msaada polisi hawa jamaa wakivamia kiwanja chako na hii ni kwa sababu ya wanalindwa na baadhi ya viongozi wa polisi. Nadhani huu ni uonevu uliokithiri na swala hili lingefuatiliwa na usalama wa Taifa kwani linakua kwa kasi. Nawakilisha wakuu
ndoleha Unaweza kukutana na mimi kesho njoo makumbusho unipe data naweza kufanyia kazi kama kweli unayoyasema na ushahidi unao sitaki mambo ya udaku au umepata viroba
maswali ya msingi ya kujiuliza...........
1.hii taarifa ni nzito na inasikitisha kama ni kweli.
2.mbona mleta mada hajataja hata mtu mmoja katika hizo ofisi ambazo zinashiriana na hawa watu?mfano amtaje askari flani au afisa ardhi flani ili taarifa yake iwe na kitovu ie pahali pa kuanzia.
3.taarifa ni ya jumla mno kiasi kwamba inaelea,haina pakushika.
4.taja hata mwananchi mmoja alienyang'anywa ardhi/kiwanja chake ili asaidie hata kuwatafuta hao maafisa wa serikali wanaotumia ofisi zao kinyume na taratibu.
Sasa ushahidi si msearch hayo majina. Hebu nenda kwenye google usearch papa msofe au kama humfahamu kwa sura bofya hapa the eastafrica: PAPAA MSOFE ATUHUMIWA KUVAMIA KIWANJA MBEZI BEACH!
Pia Papa Msofe akamtapeli Mama Mjane na ITV walimuhoji Kamanda Kenyela RPC wa Kinondoni na huyo Tapeli na Kenyela akamtetea na kusema msofe sio tapeli ni mfanyabiashara. Baadae jamii forum na ITV wakaripoti kwamba huyu Papa Msofe ambaye RPC amemtetea kwenye vyombo vya habari ni tapeli na kwamba Wanaharakati wakiongozwa na mpiganaji Mama Ananelia Nkya walilisimamia kidedea mpaka Waziri Mkuu akingilia kati na kuamuru swala hili lishughulikiwe mara moja. Cha ajabu kuona hivyo tunaambiwa Polisi walimpa huyu tapeli siku saba kurudisha kiwanja na tapeli huyu hakuchukuliwa hatua yoyote. Nadhani ukisearch papa msofe au papaa msofe utapata skendo lukuki za huyu jamaa. Tunaambia polisi wanalipwa mshahara na huyu jamaa.
Mwingine ni Mr Mushi ambaye alikuwa ardhi. Naye ni hatari na anatetewa na maafisa wa Ardhi na Polisi.
Nasikia kweli ukienda Polisi ukataja jina la mtu wanayemfahamu na kusema amevamia kiwanja chako ndio umewaletea mtaji, kwanza wanakwambia hawahusiki nenda kapigane nae mwenyewe au nenda mahakamani na baada ya hapo wanampigia simu huyo jamaa wanamwambia Mkubwa naona umefanya kazi lete pesa yakulinda huku na jamaa fasta anawafikishia fungu lao.
HUU NI UKWELI SION MAJUNGU. hakuna mtu Tanzania anaweza kumdhulumu mtu Ardhi bila kushirikiana na Polisi - HAKUNA!
narudi tena mleta mada labda kachukuliwa demu wake na hao watu hakuna usibitisho hata moja tuamini vipi toa ***** wako
Kama unafahamu haki zako huwezi lalamika, namba ya simu ya huyo IGP ipo mpigie mweleze na ushahidi uwe nao
Utakaporudi na hiyo part 2 uje na majina ya hao wahalifu pamoja na hao makamanda
sinauhakika na mtoa mada nikupe simu ya igp said mwema au ya dci manumba mimi mwenyewe nipo kwenye system kama nikweli na ushahidi unao mimi naweza kusaidia
Makamanda wa polisi wawe wanachaguliwa na wananchi....