IGP mstaafu Said Mwema utakumbukwa pamoja na mapungufu uliokua nayo

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Wadau nia yangu si kumsifia kachero huyu mustaafu aliyewahi kulitumikia taifa hili na kimataifa bali ni kuendelea kumkumbuka sana kwa mchango wake mkubwa aliokua nao katika jeshi la polisi. Huyu ni kachero ameacha pengo kubwa sana katika jeshi hilo ambalo kwa sasa linaonekana wazi kabisa kutokana na baadhi ya matukio yanaoendelea kulikumba taifa hili.

Tunashuhudia mauaji ya kinyama yanayofanywa nchini kwa kutolea mfano juzi kule Mwanza, Tanga na Dar,bado tuliona uvamizi wa vituo vya polisi uliokua ukifanywa na majambazi, uvamivizi katika mabenki unaofanywa na majambazi mchana kweupe, maalibino kwa sasa wanaishi katika hofu kubwa. Lakini wakati wa uongozi wa kachero huyu mstaafu matukio haya yalidhibitiwa kwa umakini mkubwa sana kitu ambacho ni tofauti kabisa na sasa tunavyoshuhudia.

Kuhusu masuala ya kisiasa pamoja na kachero huyu kua katika mitihani mizito ya mashinikizo ya wanasiasa lakini mahali ambapo aliona kuna upepo sio mzuri aliwaita wanasiasa pamoja na kutafuta suluhu kuhakikisha amani inaendelea kuwepo.Kwa sasa haya ninayoyazungumza hayapo, shinikizo lolote hata lenye harufu ya kisiasa likitolewa ni kutii amri tu bila hata kulichambua linaweza kuleta sintofahamu mbeleni.

Kuna wanaofikiria kua kazi ya jeshi hilo ni kutii amri tu, hawajui kua kazi kuu ya jeshi hilo ni kulinda raia na mali zao kwa kutumia weledi wa Maarifa zaidi ya nguvu, kutumia diplomasia kwanza kabla ya kuchukua hatua ya kutumia nguvu kulingana na aina ya tatizo.Sijawahi kuona wala kusikia maneno kwamba itelijensia imegundua kua na uvunjifu wa amani kwa sababu tu eti vyama viwili vya siasa vitashambuliana majukwaani, kwanini ukiona hivyo usiwaite viongozi wao uwakalishe waachane na dhamira hiyo wafanye mikutano yao kwa amani? kwanini ukiona hivyo usilinde mikutano hiyo uvunjifu huo wa amani usitokee?

Najua yatazungumzwa ya Lugumi na ubambikiziaji kesi uliokua umekithiri wakati wa Said Mwema lakini madhaifu haya hayawezi kamwe kufunika mema aliyokwishayaacha enzi la utawala wake.
 
Said Mwema ni level ya Kimataifa yule. Ni humble lakini alikuwa jembe. Mh. Magu hebu angalia hata kumpa mkataba wa mwaka mmoja anyooshe mambo wakati unatafuta jembe lingine!
 
Angalao alikuwa anatumia diplomasia, kwanza hata hii kashifa ya Lugumi nahisi wanataka kumchafua tu yeye sidhani kama anahusika
 
Acha mahaba ukajitoa akili kaka!! Mfumo mbovu kila mtu anaiba ndio maana inaharibu hata watu Wema! Wanaona itakuwaje atoke patupu? Nae anatengeneza deal hewa anapiga! Akiwa kama IGP ameona deal nyingi kubwa zikipita na wenzake wakitajirika....na yeye kajipigia hako kamoja akatulizana...na atalindwa tu hakuna namna maana amekula na wakubwa wenzake!
 
Wadau nia yangu si kumsifia kachero huyu mustaafu aliyewahi kulitumikia taifa hili na kimataifa bali ni kuendelea kumkumbuka sana kwa mchango wake mkubwa aliokua nao katika jeshi la polisi. Huyu ni kachero ameacha pengo kubwa sana katika jeshi hilo ambalo kwa sasa linaonekana wazi kabisa kutokana na baadhi ya matukio yanaoendelea kulikumba taifa hili.

Tunashuhudia mauaji ya kinyama yanayofanywa nchini kwa kutolea mfano juzi kule Mwanza, Tanga na Dar,bado tuliona uvamizi wa vituo vya polisi uliokua ukifanywa na majambazi, uvamivizi katika mabenki unaofanywa na majambazi mchana kweupe, maalibino kwa sasa wanaishi katika hofu kubwa. Lakini wakati wa uongozi wa kachero huyu mstaafu matukio haya yalidhibitiwa kwa umakini mkubwa sana kitu ambacho ni tofauti kabisa na sasa tunavyoshuhudia.

Kuhusu masuala ya kisiasa pamoja na kachero huyu kua katika mitihani mizito ya mashinikizo ya wanasiasa lakini mahali ambapo aliona kuna upepo sio mzuri aliwaita wanasiasa pamoja na kutafuta suluhu kuhakikisha amani inaendelea kuwepo.Kwa sasa haya ninayoyazungumza hayapo, shinikizo lolote hata lenye harufu ya kisiasa likitolewa ni kutii amri tu bila hata kulichambua linaweza kuleta sintofahamu mbeleni.

Kuna wanaofikiria kua kazi ya jeshi hilo ni kutii amri tu, hawajui kua kazi kuu ya jeshi hilo ni kulinda raia na mali zao kwa kutumia weledi wa Maarifa zaidi ya nguvu, kutumia diplomasia kwanza kabla ya kuchukua hatua ya kutumia nguvu kulingana na aina ya tatizo.Sijawahi kuona wala kusikia maneno kwamba itelijensia imegundua kua na uvunjifu wa amani kwa sababu tu eti vyama viwili vya siasa vitashambuliana majukwaani, kwanini ukiona hivyo usiwaite viongozi wao uwakalishe waachane na dhamira hiyo wafanye mikutano yao kwa amani? kwanini ukiona hivyo usilinde mikutano hiyo uvunjifu huo wa amani usitokee?

Najua yatazungumzwa ya Lugumi na ubambikiziaji kesi uliokua umekithiri wakati wa Said Mwema lakini madhaifu haya hayawezi kamwe kufunika mema aliyokwishayaacha enzi la utawala wake.
Vipi tuandae makala ya kumkumbuka Mangu?
 
Back
Top Bottom