IGP, Mengi nao wakumbwa na mafuriko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IGP, Mengi nao wakumbwa na mafuriko

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mungi, Dec 23, 2011.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Dec 23, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Thursday, 22 December 2011

  [​IMG]
  Mkazi wa eneo la Kinondoni Shamba akihama na godoro lake kuelekea kwa wahisani eneo la jirani baada ya nyumba zao kukumbwa na mafuriko, jijini Dar es Salaam, jana. Picha na Joseph Zablon

  Boniface Meena na Keneth Goliama

  NYUMBA ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchin (IGP) Said Mwema na ile ya Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, ni miongoni mwa makazi ya watu yaliyokumbwa na mafuriko kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.

  Kwa siku tatu mfululizo Jiji la Dar es Salaam na viunga vyake limekumbwa na mafuriko makubwa yaliyovuruga mfumo wa usafiri, kuharibu makazi pamoja na kusababisha vifo.

  Nyumba ya IGP iko eneo la Upanga wakati ya Mengi iko Kinondoni, ambako pia ofisi za Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Ofisi za Ubalozi wa India zimekumbwa na mafuriko.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema makazi ya Mengi na IGP Mwema yalikumbwa na mafuriko kutokana na kuwa karibu na ofisi za UNDP.

  "Kwa IGP ni mkoa wa Ilala siyo Jurisdiction (eneo langu la uangalizi) yangu, lakini eneo hilo ambalo liko sawa na UNDP kulikuwa na mafuriko, lakini hakuna maafa na wingi wa maji unaendelea kupungua,"alisema Kenyela na kuongeza:,

  "Maji yalijaa sana, isingekuwa rahisi kuokoa watu, lakini waliotoa vyombo vya kuokolea walisaidia kufanikisha watu waliokuwa wamekwama kutolewa kwenye maeneo yao."

  Alisema hata kwa Mengi hali ilikuwa hivyo, lakini ilikuwa ni vigumu kujua watu wanaokolewa katika nyumba gani kutokana na kazi ya uokoaji kufanyika kwa haraka na mambo kuwa mengi kwa wakati huo.

  "Hata kwa upande wa Mengi ni hivyo hivyo, kila mtu aliokolewa na wote waliokuwa kwenye maeneo hayo waliokolewa,"alisema.

  Mbunge Shah apongezwa
  Katika hatua nyingine, baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam, wamempongeza Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shah kwa kujitolea boti kwa ajili ya kuwaokoa watu waliokuwa wamekwama katika Bonde la Msimbazi.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi hao walisema mbunge huyo ni mfano wa kuigwa na kwamba moyo wake wa uzalendo ni funzo kwa viongozi wengine wa kisiasa.

  Walisema hatua ya mbunge huyo kutoa boti ni kuonesha dhahiri kwamba ana mapenzi mema na wananchi hata wale ambao si wapiga kura wake.

  Walisema kauli ya mbunge huyo kwamba, jambo kama hilo halihitaji kusubiri vikao vya kamati za maafa kilionesha ukomavu mkubwa wa kujali wananchi na kutaka wabunge wengine kuiga mfano huo badala ya kuendekeza siasa tu.

  Mbunge huyo alikutwa eneo la tukio akishirikiana na waokoaji wengine kunusuru roho za wanawake na watoto, ambao walikwama katika mafuriko hayo ambayo yalianza juzi.

  Mkazi wa Tabata, Sulemani Mabuku alisema licha ya kuwa na machungu ya kupatwa na maafa yaliyosababisha kuwapoteza ndugu na jamaa zao, walipata faraja pale waliposikia hatua ya mbunge huyo wa Mafia kushiriki katika uokoaji.

  Walisema huo ni mfano wa kuigwa kwa wabunge wengine kuacha siasa kwenye mambo muhimu kama maafa na kutaka wote kushirikiana vizuri ili kuhakikisha jamii inawakumbuka kuwa wanawajali wananchi.

  Juzi Shah alifika katika eneo la Mto Msimbazi ambako kulikuwa na watu waliokuwa wakisubiri msaada wa wasamaria wema baada ya kukumbwa na mafuriko, na pale alipowasiliana na kikosi cha uokoaji cha Zimamoto, hakuweza kupata msaada wa haraka kutokana na watendaji wa kikosi hicho kutokuwa na vifaa vya kuwezesha uokoaji.

  Kutokana na hali hiyo, Shah alilazimika kwenda eneo la Kivukoni – Feri, ambako alikodi boti iliyosafirishwa kwa gari hadi eneo la maafa, hivyo kuanza mara moja kazi ya uokoaji.
   
Loading...