IGP Ernest Mangu, Zanzibar huiwezi itakuelemea

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Kama kweli unajiamini na cheo chako basi WaZanzibari wanataka ukawatembelee wahanga wa mazombi ,wapo waliopigwa risasi,minyororo ,kupofuliwa,kuvunjwa viungo na mengine mengi.

umezuka na kauli za kumkamata Katibu Mkuu wa CUF,sio vibaya kwa madai uliyoyaeleza hilo lipo kwenu na ushahidi mliokusanya ,maalim Seif kishatamka mara nyingi tu,kuwa haogopi polisi kwa maana hatokimbia nchi kukimbia polisi kumkamata,wakati wowote anawakaribisha kumkamata kwa hizo tuhuma.

Kubwa umesema uchaguzi wa mwanzo ulikuwa wa amani na wa pili kadhalika sasa,kamkamate Jecha ambae aliufuta uchaguzi ambao wewe na Cheo ilichonacho umesema ulikuwa wa amani,maana ya kuwepo amani wakati wa uchaguzi inajulikana kuwa kila kitu kilienda kama kilivyopangwa kiasi ya kufikia huyo Jecha kuwakabidhi washindi wa viti vya uwakilishi na ubunge, iweje leo afute uchaguzi mzima bila ya shaka anayokesi ya kujibu kwani amepora haki ya wananchi na kuchochea hasira zinazoendelea hadi leo ,jeshi lako liende likamhoji jecha kwa kina.

Jengine sio siri watu waliokuwa wanajifunika nyuso maarufu kama mazombo wakitumia magari ya vyombo vya dola wakizuka katika sehemu ya miji ya Zanzibar na kupiga watu bila ya sababu huku wakiwa na silaha za moto sio wamebeba bali hata kuzitumia pia vikiwemo vitu vyenye ncha kali nondo na minyoororo ,wahanga wa matukio hayo wapo watembelee kuwahoji na kupata ushahidi na ushahidi upo tena sio kwa kusimulia hata picha na kideo zipo,na namba za magari pia zipo,tembelea wahanga uwafariji na wakupe ushahidi wenye vielelezo tosha,watakuelewa.

Sasa kumkamata maalimu hakutakusaidia kitu,kwani ndani ya damu za WaZanzibari walio wengi hawana imani na CCM,serikali yao viongozi wao na hata wanachama holela walio mitaani na wanawajua kwa majina kwa ufupi hawaitambui serikali mbali ya CUF kama chama kutoitambua serikali hata wananchi wa kawaida hawatoi ushirikiano ipasavyo.

Utawaona wanakwenda huku na kule ila waarabu wa Pemba wanajuana kwa vilemba na ,hisia zako zinakupa kwa ssasa nchi ipo kwenye amani hilo sio kweli,hakuna amani pale ambapo serikali haitambuliwi na wananchi walio wengi.Na hilo halina mbadala viongozi wa CCM wote wameshachujuka ndani ya mioyo ya WaZanzibari walio wengi walio baki ni wale pangu pakavu tia mchuzi.

Kuna sakata la mashehe kama ni cheche basi hili ni jinga la moto wa jehannam ,Nenda kamhoji Jecha kwa nini alikimbia kwenye kituo na hakuonekana na simu alizifunga ,aliekuwa chini yake alipokuwa akiendeleza matangazo na matukio ya awali alikuja kuchukuliwa mzobemzobe ,tuambie ni akina nani waliofanya yale,si una wachunguzi na ni mahodari wa kukusanya uchunguzi basi wapeleke wakakusanye uchunguzi kisha uje juu na kutuhabarisha.

Ikiwa aliekupa cheo kasema hana mamlaka ya mambo ya Zanzibar iweje wewe ulie chini yake uwe na mamlaka na kutaka kuvalia njuga,jikune ujipatapo ya Zanzzibar bora ukayaepuka au kama unayaingilia basi onyesha uwiano uliotukuka na sio kufuata mkumbo,yatakumwagikia.

Unajua kuna viongozi ni kama miti uwendako upepo nao huelemea hukohuko usiweko huko.
 
Maalim atakamatwa tu kama anavunja Sheria. Zanzibar tulishamchagua kwa kishindo DR Shein. Uchaguzi ni 2020 na tutashinda tena!!!
 
Cuf wana matatizo sana,lete picha na majina ya walioathirika na mazombi
 
Maalim atakamatwa tu kama anavunja Sheria. Zanzibar tulishamchagua kwa kishindo DR Shein. Uchaguzi ni 2020 na tutashinda tena!!!
Kwa mujibu wa IGP Maalim Seif amevunja sheria za nchi na hivyo anastahili akamatwe na hatimaye afunguliwe mashtaka.Lakini matamshi na dhamira ya kumkamata kila siku yanaishia kwenye vyombo vya Habari na maskani ya Kisonge na Lumumba tu!

Yeye huku bukheri wa hamsa'uishirini,akiendelea kutamba na kudunda,anasafiri atakako na anasema atokalo kwa jumuiya atakazo1.

La ajabu ni kuwa akikohowa tu,London, Washington au the Hague huku Kanga watu hazikai viunoni, ni mtafaruku wa Juma Mbaruku. Wafuasi wake wanatolewa kiziwizini bila masharti ya awali kutekelezwa kana kwamba kuna zilzala imekikumba kisiwa. Hii si aibu! Tukisema kuwa anaogopwa mtuhumiwa huyu tutakosea? Hii si kwereche kwereche msumeno, alia-kweche.......
 
Mangu......tuliza mzuka na povu! Maalim sio size yako!! Hata Magu analijua hilo! Ameshapambana na JKN na wote ccm wanamtambua! Wewe sio size yake! Utulie! Lugumi tu anakushinda sembuse Rais wa mioyo ya wazanzibar? Maalim ni kama imani kwao! Huwezi kuvunja Imani ya watu kwa bunduki! Kamweee
 
sijui lini Zanzibar itakua huru kutoka mikononi mwa mkoloni mweusi na vibaraka ????!!!!
 
Alishindwa mahita .kama suluhisho la zanzibar ni kumkamata maalim sefu basi tusubiri tuone
 
Cuf wana matatizo sana,lete picha na majina ya walioathirika na mazombi

mazombi.jpg
mazombi.jpg
 
Back
Top Bottom