NDESSA
JF-Expert Member
- May 2, 2013
- 1,946
- 1,800
Ndugu wahitimu wa Ifunda kwa miaka yote tangu shule ilipoanzishwa napenda kuwajulisha kuwa tunao Umoja wa wahitimu wa Ifunda unaotambulika kama Ifunda Technical Alumni Association(ITAA) na tulipata usajili kutoka mamlaka ya usajili wa vyama Wizara ya mambo ya ndani mwaka jana,Tumekuwa na utaratibu wa kukutana wanachama kujadili mambo mbalimbali yanayohusu kuendeleza shule ya Ifunda lakini pia kuweza kuwaleta watu pamoja na kufahamiana ili kupanua mtandao wa wanaifunda popote walipo,kuna mipango mingi ambayo iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji hususani mradi wa kuwapatia Ifunda kisima cha maji safi tayari kuna michango ya wanachama na wadau wengine wanaendelea kuchangia mpango huu uliozinduliwa mapema mwaka jana mwishoni DSM na msukumo mkubwa wa kufanya mradi huu ni kutokana na kilio cha wanaifunda cha kuwa na chanzo cha maji kisicho cha uhakika yani Lyandembela,Kutokana na ratiba ya vikao vya umoja kwa mujibu wa katiba yetu tuliazimia kukutana jumapili ya tar 01 sept 2013 na Uongozi umependekeza kikao hiki kiwe tofauti kidogo yani iwe Get together part ambapo tumepanga kufanyia pale Msasani Beach Resort ya JKT kuanzia saa 6 mchana kutokana na utofauti wa mahali husika kila mmoja atatakiwa kulipa kiingilio kiasi ya sh Elfu tano tu (5,000) pia utapata na kinywaji,WOTE MNAKARIBISHWA SANA, Nimetoa maelezo japo kwa ufupi kwa sababu kuna ambao hii ni habari mpya kwao tumekuwa tukitumia vyombo vya habari kutangaza shughuli zetu hususani TBC1,Couds,Capital,Blogs mbalimbali na fb, wakati mwingine nitaandaa maelezo marefu sana kwa sababu ni vigumu kwa jiografia yetu wote kuweza kukutana pamoja ikizingatiwa kuwa tumekuwa tukikutana sana DSM,
mnaweza pia kutembelea page yetu ya facebook IFUNDA TECH, ALUMNI ASSOCIATION(ITAA)
Imetolewa na DAMACENT MICHAEL (KATIBU MKUU MSAIDIZI ITAA)
BOX 35935
DSM
Mob; 0752 513 154
mnaweza pia kutembelea page yetu ya facebook IFUNDA TECH, ALUMNI ASSOCIATION(ITAA)
Imetolewa na DAMACENT MICHAEL (KATIBU MKUU MSAIDIZI ITAA)
BOX 35935
DSM
Mob; 0752 513 154