LopoLopo
JF-Expert Member
- Feb 16, 2025
- 229
- 135
Chini ya Rais Samia Wanachama wapya 900,000 wamejiunga na Mifuko ya Kinga ya jamii.
Kutokana na usimamizi na maelekezo ya Rais Samia utekelezwaji wa Sera ya Taifa ya Kinga ya Jamii ya Mwaka 2023 ambayo imeweka utaratibu madhubuti na kuimarisha utekelezaji wa afua stahiki za kinga ya jamii. Utekelezaji wa sera hiyo pamoja na afua nyingine umesaidia kuongeza idadi ya wanachama wachangiaji kutoka 849,886 mwaka 2021, hadi 1,758,018 mwaka 2025.
Rais Samia ameongeza na kuboresha mfumo wa ulipaji wa mafao kwa wastaafu , hii ni baada ya kufanya mabadiliko ya kikokotoo kwa wastaafu. Maboresho hayo yameongeza wigo wa malipo ya mkupuo kutoka asilimia 33 hadi asilimia 40 kwa waliokuwa wanalipwa asilimia 50 kabla ya kuunganisha mifuko mwaka 2018, na kutoka asilimia 33 hadi asilimia 35 kwa waliokuwa wanapata asilimia 25, Serikali yake pia imeongeza imeongeza kima cha chini cha pensheni kutoka Shilingi 100,000 hadi Shilingi 150,000 kwa mwezi na kuhuisha pensheni ya kila mwezi kwa kiwango cha asilimia mbili kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizopo .