Ifahamu taasisi ya ndoa kabla ya kuingia kwenye ndoa

Gerald Robert

JF-Expert Member
Jan 2, 2013
337
219
Usiwemwepesi wa kukimbilia kuingia kwenye taasisi ya ndoa kama haujui ni kwanini unataka kuingia kwenye ndoa.
Note: Kumbuka hapa nazungumzia Ndoa, na si tendo la ndoa.

Vijana wengi (hasa wakike) wameangukia kwenye ghafla bila ya wao kutarajia ba mwisho wa siku wanajikuta wamekuwa ni wahanga wa ndoa.

Swala la ndoa libahitaji san kumshirilikisha Mungu, lakini nilazima utumie akili zako ulizopewa na Mungu iliupate kufanikiwa.

Kumbuka kwamba, Nimesema Tumia akili zako ulizopewa na Mungu, sijasema Uzitumainie akili zako ulizopewa na Mungu.

Kutumia akili, na Kutumainia akili, haya ni mambo mawili tofauti.

Kwahiyo shida kubwa inayowasumbua vijana wa sasa (hasa vijana wakike) ni kuzitumainia akili zao badala ya kutumia akili zao pindi wanapohitaji kuingia katika ndoa.

Katika kila jambo tunapaswa kumtumaini Mungu na kumtegemea yeye na si kuzitumainia akili zetu wala kuzitegea hizo maana Mungu huwa hashindwi bali akili huwa inafika wakati zinashindwa kabisa kukupatia kile ulichokitarajia.

Unapohitaji kuingia kwenye ndoa hakikisha unazo nguvu za kutosha kukabili kile kilichomo ndani ya ndoa.

Ndoa ni tendo la kiimani (faith) ambalo ni muunganiko wa mtu Mume na mtu mke, kwahiyo mnapounganishwa kwa jinsi hiyo na zile tabia zenu za asili za kibinaadamu nazo huwa katika muunganiko huo, kwahiyo mnakuwa mmeunganisha tabia mbili tofauti na kupata tabia moja ambapo kila mwandoa anatakiwa awe na nguvu za kutosha kukabiliana na matokeo ya tabia hiyo moja baada ya muunganiko wa tabia mbili tofauti.

Mabinti wengi wanaangalia mafanikio ya kijana wa kiume kama kigezo cha wao kukubali au kukataa kuolewa na kijana huyo.hili ni jambo baya sana kwenye ndoa.

Tafsiri yake nikwamba wewe umepbda yale mafanikio ya yule kijana na wala sio huyo kijana ambaye ni chachu ya hayo mafanikio uyaonayo na hapa ndipo mabinti wengi hujikuta wako kwenye new oa na wanaume wasiowapenda wao ila tu kwakuzipenda mali. Mali zinapo o doka na hapo ndipo mwisho unakuwa ni mwisho hiyo ndoa.

Ndani ya ndoa kuna mambo mengi sana ambayo yanaweza kukuondolea amani , hata Sara mke wa Nabii Ibrahimu anafahamu haya mambo, au kama unabisha jaribu usome historia ya Mfalme Daudi na alivyomtenda yule Uria mhiti kwaajili ya mke wake.

Ndani ya ndoa kuna maudhi mengi sana, wasomi wa biblia wanafahamu kisa cha Mfalme Ahasuero kumuacha Vashti na kumuoa Esta. (sisemi kwamba muwaache wake zenu, hapana, bali mjifunze kukabiliana na tabia za ndani ya ndoa msifikili kwamba Ndoa ni lelemama hata muikimbilie. Mjipange kwanza na mumshirikishe Mungu kwa kila hatua ya kuelekea ndoa

Ni vizuri sana mafanikio yakukute wewe kwenye ndoa kuliko wewe uyakute mafanikio kwenye ndoa.

Pesa na mali ni kama mbolea tu kwa wanandoa lakini si kinga kwamba ndoa yako itakuwa njema na yenye amani na furaha .

JIFUNZE = FUNDISHIKA
 
Ujumbe mzuri uliobebwa na uandishi mbovu.
Ukimaliza kutype kazi yako ihariri kabla hujai-publish.

mada
Mkuu..! Happy Val's day.

Kwanza, nakupongeza kwa content yako ambayo kwa kiasi kikubwa imejazwa na msisitizo wa kumshirikisha Mungu katika suala zima la ndoa.
Changamoto; Katika hali ya kiuhalisia zaidi (sio kinadharia), watu wamekuwa wakifunga na kumuomba Mungu kuhusu suala la kumpata mtu sahihi wa maisha yake (wengine hutoa na vigezo kabisa ila wengine huwa hawavitaji ila wamevihifadhi tu moyoni).
Ugumu huwa unakuja pale, anapokutana na mtu baada ya maombi yake ( bila kujali wakati gani umepita), inapotokea amekuja mtu ambaye hakuwahi hata kumfikiria na hajakidhi hata kigezo kimoja (nazungumzia kimuonekano, maana ni vigumu kumtambua mtu wadhifa wake wa ndani mara tu mnapoonana) ambacho yeye huwa anakipenda, basi bila kutafakari huenda ndio jibu la maombi yake au sio yeye, moja kwa moja huwa tunajiaminisha kuwa sio jibu kabisa, "haiwezekani Mungu anipe mtu mbaya kiasi hiki", wengine husema.Na wengine hurudi nyuma tena au huendelea na maombi zaidi..( I miss you my Valentine espy ) .
Hapa ninachotaka kukwambia mkuu ni kwamba, imani ndio tatizo kuu.
Kumuamini Mungu kuwa ndiye anayekujibu maombi yako bado inahitaji imani pia.
 
Usiwemwepesi wa kukimbilia kuingia kwenye taasisi ya ndoa kama haujui ni kwanini unataka kuingia kwenye ndoa.
Note: Kumbuka hapa nazungumzia Ndoa, na si tendo la ndoa.

Vijana wengi (hasa wakike) wameangukia kwenye ghafla bila ya wao kutarajia ba mwisho wa siku wanajikuta wamekuwa ni wahanga wa ndoa.

Swala la ndoa libahitaji san kumshirilikisha Mungu, lakini nilazima utumie akili zako ulizopewa na Mungu iliupate kufanikiwa.

Kumbuka kwamba, Nimesema Tumia akili zako ulizopewa na Mungu, sijasema Uzitumainie akili zako ulizopewa na Mungu.

Kutumia akili, na Kutumainia akili, haya ni mambo mawili tofauti.

Kwahiyo shida kubwa inayowasumbua vijana wa sasa (hasa vijana wakike) ni kuzitumainia akili zao badala ya kutumia akili zao pindi wanapohitaji kuingia katika ndoa.

Katika kila jambo tunapaswa kumtumaini Mungu na kumtegemea yeye na si kuzitumainia akili zetu wala kuzitegea hizo maana Mungu huwa hashindwi bali akili huwa inafika wakati zinashindwa kabisa kukupatia kile ulichokitarajia.

Unapohitaji kuingia kwenye ndoa hakikisha unazo nguvu za kutosha kukabili kile kilichomo ndani ya ndoa.

Ndoa ni tendo la kiimani (faith) ambalo ni muunganiko wa mtu Mume na mtu mke, kwahiyo mnapounganishwa kwa jinsi hiyo na zile tabia zenu za asili za kibinaadamu nazo huwa katika muunganiko huo, kwahiyo mnakuwa mmeunganisha tabia mbili tofauti na kupata tabia moja ambapo kila mwandoa anatakiwa awe na nguvu za kutosha kukabiliana na matokeo ya tabia hiyo moja baada ya muunganiko wa tabia mbili tofauti.

Mabinti wengi wanaangalia mafanikio ya kijana wa kiume kama kigezo cha wao kukubali au kukataa kuolewa na kijana huyo.hili ni jambo baya sana kwenye ndoa.

Tafsiri yake nikwamba wewe umepbda yale mafanikio ya yule kijana na wala sio huyo kijana ambaye ni chachu ya hayo mafanikio uyaonayo na hapa ndipo mabinti wengi hujikuta wako kwenye new oa na wanaume wasiowapenda wao ila tu kwakuzipenda mali. Mali zinapo o doka na hapo ndipo mwisho unakuwa ni mwisho hiyo ndoa.

Ndani ya ndoa kuna mambo mengi sana ambayo yanaweza kukuondolea amani , hata Sara mke wa Nabii Ibrahimu anafahamu haya mambo, au kama unabisha jaribu usome historia ya Mfalme Daudi na alivyomtenda yule Uria mhiti kwaajili ya mke wake.

Ndani ya ndoa kuna maudhi mengi sana, wasomi wa biblia wanafahamu kisa cha Mfalme Ahasuero kumuacha Vashti na kumuoa Esta. (sisemi kwamba muwaache wake zenu, hapana, bali mjifunze kukabiliana na tabia za ndani ya ndoa msifikili kwamba Ndoa ni lelemama hata muikimbilie. Mjipange kwanza na mumshirikishe Mungu kwa kila hatua ya kuelekea ndoa

Ni vizuri sana mafanikio yakukute wewe kwenye ndoa kuliko wewe uyakute mafanikio kwenye ndoa.

Pesa na mali ni kama mbolea tu kwa wanandoa lakini si kinga kwamba ndoa yako itakuwa njema na yenye amani na furaha .

JIFUNZE = FUNDISHIKA
Mkuu nipe kifungu inapopatikana hadithi ya mfalme ahafuelo
 
ESTA 1: 10 Hata siku ya saba, mfalme alipofurahiwa moyo wake kwa divai, aliwaamuru Mehumani, Biztha, Harbona, Bigtha, Abagtha, Zethari, na Karkasi, wale wasimamizi-wa-nyumba saba waliohudumu mbele za mfalme Ahasuero,
11 wamlete Vashti, malkia, mbele ya mfalme, amevaa taji ya kifalme; ili kuwaonyesha watu na maakida uzuri wake, maana alikuwa mzuri wa uso.
12 Bali Vashti, malkia, alikataa kuja kwa amri ya mfalme kwa mkono wa wasimamizi-wa-nyumba; kwa hiyo mfalme akaghadhibika sana, na hasira yake ikawaka ndani yake.
13 Basi mfalme akawaambia wenye hekima, walio na elimu ya nyakati; maana ndivyo ilivyokuwa desturi ya mfalme kwa wote waliojua sheria na hukumu;
14 na karibu naye wameketi Karshena, Shethari, Admatha, Tarshishi, Meresi, Marsena, na Memukani, wale maakida saba wa Uajemi na Umedi, waliouona uso wa mfalme, na kuketi wa kwanza katika ufalme; akawauliza,
15 Tumfanyieje Vashti, malkia, kwa sheria, kwa sababu hakufanya kama vile alivyoamriwa na mfalme Ahasuero kwa mkono wa wasimamizi-wa-nyumba?
16 Basi Memukani akajibu mbele ya mfalme na maakida, Huyu Vashti, malkia, hakumkosa mfalme tu peke yake, ila na maakida wote, na watu wote pia walioko katika majimbo yote ya mfalme Ahasuero.
17 Kwa maana tendo hilo la malkia litajulikana na wanawake wote, hata waume zao watadharauliwa machoni pao, itakaponenwa ya kuwa mfalme Ahasuero aliamuru Vashti, malkia, aletwe mbele yake, bali hakuja.
18 Hata na leo hivi mabibi wastahiki wa Uajemi na Umedi waliokwisha kuzisikia habari za tendo lake malkia watawaambia vivi hivi maakida wote wa mfalme. Hivyo kutatokea dharau nyingi na ghadhabu tele.
19 Basi mfalme akiona vema, na itoke kwake amri ya kifalme, nayo iandikwe katika sheria za Waajemi na Wamedi isitanguke, ya kwamba Vashti asifike tena mbele ya mfalme Ahasuero; na umalkia wake mfalme ampe mwingine aliye mwema kuliko yeye.........endelea kusoma...
 
Asante sana
 
Sijamaliza kuisoma lakini umewaonea mabinti , mabinti kuwaambia watumie akili dah , umewapa shida sana. Yasmin wanawake wote hutumia akili kiduchu sana kwenye mahusiano na ndivyo walivyoumbwa, mwanamke anatumia hisia sana kuliko akili yake

Hata yule unayemdhania Yuko smart Kwa mambo yake ukimtongoza ukiwa mwanaume wa shoka lzm aiache akili pembeni na hulka yake ichukue nafasi

Cha msingi wanaume tumekuwa wapuuzi sana tunashindwa kuzicontrol hisia zao Hawa wanawake

Ndiyo maana shida inawakuta
 
Back
Top Bottom