Inaelezwa kuwa ili haya madude yawe na sifa ya kuitwa jua (star) basi sifa ya kwanza ISIWE INAZUKUUKA JUA (STAR) NYINGINE ZAIDI YA KUIZUNGUUUKA GALAXY,kwani si STAR zote zenye kutoa nishati kama jua (star) yetu. Japo hiyo nayo ni moja ya sifa kwa hapo zamani kabla hawajagundua ma -jua (star) yasiotoa nishati. Lakini pia mimi sikusema kama Jupiter ni ndogo ya kukosa sifa ya kuwa jua (star) ila nimesema sifa iliyokosa ni kitendo cha yenyewe kulizunguuka jua(star) yetu. Kama nimepotoka ruksa kunisahihisha.Mkuu namba 7 hapo
Ukubwa tu ndio unafikiri Jupiter imepoteza hiyo sifa?
Vipi kuhusu namna ya upatikanaji wake na uzalishaji wa nishati...jua linatoa nishati lupitia mfumo wa fussion baada ya kuchoma helium ndipo tunapata mwanga (mwanga).
Kuna tofauti kubwa sana kati ya jupiter na jua
Mkuu nafikiri inaweza kuwa sawa.Hapa inategemea na kasi ya Jupiter kujizunguusha yenyewe kwenye mhimili wake.Kama itakuwa na kasi kubwa kuliko dunia basi hata siku ya huko Jupiter itakuwa fupi kulinganisha na hapa duniani.No 9 ina ukakasi hasa ukizingatia iko mbali zaidi na jua, ni kubwa kuliko dunia.nilitegemea iwe kinyume.
Hiyo point yako ingekuwa sawa kama mtoa post angesema ni mwaka mfupi kuliko wa dunia , ukubwa wa jupita unaifanya iwe na na speed kubwa na momentum kuwbwa kwenye mhimili wake ,No 9 ina ukakasi hasa ukizingatia iko mbali zaidi na jua, ni kubwa kuliko dunia.nilitegemea iwe kinyume.
Hapafai kama kuku tu watashindwa kuishi
Sasa unataka aruke aende wapi
Sio kuku tu hata binadamu hawezi kuishi huko, kuna upepo unaofikia spidi ya 600 - 1200km/ph + hali ya hewa yake na pia inaelezwa kuwa upande mmoja wa hii Sayari inachukua hadi miaka 62 kuona mwanga wa jua na pia inakuwa hivo hivo kuona usiku. Na ndio maana wanaanga wanauchunguza mwezi wake unaoitwa Europa ambao unaonekana kusapoti mazingira ya binadamu kuishi kwani umegundulika kuwa na maji mengi na baadhi ya viumbe wa kwenye maji wamegundulika.Hapafai kama kuku tu watashindwa kuishi
Sawa kabisa mkuu hebu endelea kujazia nondo za hili dude ambalo inasemekana dunia (earth) 1,000+ ndio zinaweza kufiti ndani yake.Kingine Jupiter inasifika kwa kutupa mionzi ya usumaku(electromagnetic radiations) yenye nguvu ya hali ya juu sana kuliko sayari yoyote.
Wanasayansi wanadai sababu hii ndio inayozilinda sayari nyingine za mfumo wa jua kutogongwa na bodies nyingine ambazo huacha njia zao na kuelekea wenye sayari za mfumo wa jua.
Kama ikitokea kimondo kikubwa kinaelekea kuigonga dunia mfano, Jupita hukivuta fasta na kikanasa kwenye Jupita, hivyo mfumo wa juna unabaki salama.
Generally ni kwamba Jupiter ikiondoka kwenye mfumo wa jua sayari nyingine zitagongwa sana na bodie nyingine huko angani ambazo zinaacha njia zao.
No 9 ina ukakasi hasa ukizingatia iko mbali zaidi na jua, ni kubwa kuliko dunia.nilitegemea iwe kinyume.
Mkuu kutoka gugo kuna hii kitu nimekuja nayo..."Wakati dunia inajizinguusha kwenye mhimili wake kwa kasi ya Km 1675 kwa saa moja,Jupiter inajizunguusha kwa kasi ya Km 43,000 kwa saa",na hivyo kukamilisha mzunguuko/siku yake kwa saa 9.9 tu.Mkuu nafikiri inaweza kuwa sawa.Hapa inategemea na kasi ya Jupiter kujizunguusha yenyewe kwenye mhimili wake.Kama itakuwa na kasi kubwa kuliko dunia basi hata siku ya huko Jupiter itakuwa fupi kulinganisha na hapa duniani.
Kumbe kila sayari ina mwezi wake? Hivi dunia ina miezi mingapi?