Ifahamu sayari ya Jupiter

samsun

JF-Expert Member
Feb 9, 2014
7,386
5,954
Habari zenu wakuu.

Leo nataka tuifahamu kwa undani hii sayari ya Jupiter.
Naanza wewe utaongezea au kurekebisha.

1. Ni sayari ya 5 kwa umbali kutoka jua letu (star).

2.Ni sayari kubwa kuliko zote ktk mfumo wa jua letu.

3.Ina miezi (moons) mingi 67 kuliko sayari zote ktk mfumo wa jua letu.

4. Ni ya 4 kwa kuwa na uangavu (brightest) wa kuweza kuonekana na binadamu bila kutumia chombo cha kuonea.

5. Mwezi wa Jupiter uitwao Ganymede ni mwezi (moon) mkubwa kuliko yote ktk mfumo wa jua letu.

6.Kati ya miezi 4 (moon) mikubwa ya Jupiter, Io,Calisto,Europa na Ganymede ni ktk mwezi Europa ndiko kunakoonekana kuwa na maisha kwa mwanadamu kwani kuna maji ya kutosha na pia viumbe hai vya kwenye maji vimegundulika kuwepo kama samaki.

7. Jupiter kwa ukubwa wake ilitosha kuwa jua (star) lakini tendo la kuwa linalizunguuka jua letu ndio limefanya likose sifa ya kuitwa jua(star)

8. Ukiwa Jupiter uzito wako ni mara 2 na nusu ya duniani,hii inamaanisha kuwa, kwa mfano kuku na kanga wetu hawawezi kuruka wakiwa Jupiter.

9. Siku (day) ndani ya Jjupiter ni fupi mno ndani ya saa 9 siku imekwisha.

Haya mwenye kuongezea aongezee au arekebishe ili tupate kulijua zaidi hili bonge la dude ambalo huku duniani tunakiona kama kikombe cha kahawa tu.
 
Mkuu namba 7 hapo

Ukubwa tu ndio unafikiri Jupiter imepoteza hiyo sifa?

Vipi kuhusu namna ya upatikanaji wake na uzalishaji wa nishati...jua linatoa nishati lupitia mfumo wa fussion baada ya kuchoma helium ndipo tunapata mwanga (mwanga).

Kuna tofauti kubwa sana kati ya jupiter na jua
 
Inaelezwa kuwa ili haya madude yawe na sifa ya kuitwa jua (star) basi sifa ya kwanza ISIWE INAZUKUUKA JUA (STAR) NYINGINE ZAIDI YA KUIZUNGUUUKA GALAXY,kwani si STAR zote zenye kutoa nishati kama jua (star) yetu. Japo hiyo nayo ni moja ya sifa kwa hapo zamani kabla hawajagundua ma -jua (star) yasiotoa nishati. Lakini pia mimi sikusema kama Jupiter ni ndogo ya kukosa sifa ya kuwa jua (star) ila nimesema sifa iliyokosa ni kitendo cha yenyewe kulizunguuka jua(star) yetu. Kama nimepotoka ruksa kunisahihisha.
 
Kingine Jupiter inasifika kwa kutupa mionzi ya usumaku(electromagnetic radiations) yenye nguvu ya hali ya juu sana kuliko sayari yoyote.

Wanasayansi wanadai sababu hii ndio inayozilinda sayari nyingine za mfumo wa jua kutogongwa na bodies nyingine ambazo huacha njia zao na kuelekea wenye sayari za mfumo wa jua.

Kama ikitokea kimondo kikubwa kinaelekea kuigonga dunia mfano, Jupita hukivuta fasta na kikanasa kwenye Jupita, hivyo mfumo wa juna unabaki salama.

Generally ni kwamba Jupiter ikiondoka kwenye mfumo wa jua sayari nyingine zitagongwa sana na bodie nyingine huko angani ambazo zinaacha njia zao.
 
Hapafai kama kuku tu watashindwa kuishi
Sio kuku tu hata binadamu hawezi kuishi huko, kuna upepo unaofikia spidi ya 600 - 1200km/ph + hali ya hewa yake na pia inaelezwa kuwa upande mmoja wa hii Sayari inachukua hadi miaka 62 kuona mwanga wa jua na pia inakuwa hivo hivo kuona usiku. Na ndio maana wanaanga wanauchunguza mwezi wake unaoitwa Europa ambao unaonekana kusapoti mazingira ya binadamu kuishi kwani umegundulika kuwa na maji mengi na baadhi ya viumbe wa kwenye maji wamegundulika.
 
Kingine Jupiter inasifika kwa kutupa mionzi ya usumaku(electromagnetic radiations) yenye nguvu ya hali ya juu sana kuliko sayari yoyote.

Wanasayansi wanadai sababu hii ndio inayozilinda sayari nyingine za mfumo wa jua kutogongwa na bodies nyingine ambazo huacha njia zao na kuelekea wenye sayari za mfumo wa jua.

Kama ikitokea kimondo kikubwa kinaelekea kuigonga dunia mfano, Jupita hukivuta fasta na kikanasa kwenye Jupita, hivyo mfumo wa juna unabaki salama.

Generally ni kwamba Jupiter ikiondoka kwenye mfumo wa jua sayari nyingine zitagongwa sana na bodie nyingine huko angani ambazo zinaacha njia zao.
Sawa kabisa mkuu hebu endelea kujazia nondo za hili dude ambalo inasemekana dunia (earth) 1,000+ ndio zinaweza kufiti ndani yake.
 
Kingine Jupiter Ni sayari inayotulinda sana na vitu kama vimondo mana ina gravity pull kubwa huvivuta vitu toward ktk centre yake
Ukanda wa asteroids belts hupatikana kati ya Jupiter na mars licha ya kuwa jupiter ni kubwa haina sifa ya kuwa star mana haina uwezo wa kuzalisha energy zaidi inategemea jua kupata nishati
 
No 9 ina ukakasi hasa ukizingatia iko mbali zaidi na jua, ni kubwa kuliko dunia.nilitegemea iwe kinyume.

Mkuu nafikiri inaweza kuwa sawa.Hapa inategemea na kasi ya Jupiter kujizunguusha yenyewe kwenye mhimili wake.Kama itakuwa na kasi kubwa kuliko dunia basi hata siku ya huko Jupiter itakuwa fupi kulinganisha na hapa duniani.
Mkuu kutoka gugo kuna hii kitu nimekuja nayo..."Wakati dunia inajizinguusha kwenye mhimili wake kwa kasi ya Km 1675 kwa saa moja,Jupiter inajizunguusha kwa kasi ya Km 43,000 kwa saa",na hivyo kukamilisha mzunguuko/siku yake kwa saa 9.9 tu.
 
Back
Top Bottom