Ifahamu Lilambo Kinaganaga

Pastor Achachanda

JF-Expert Member
May 4, 2012
3,023
1,315
Salaam,

Ni muhimu kupashana habari juu ya maeneo tunayoishi ili wageni wanapoingia waweze kujua namna ya kuishi na watu. Nakuletea uifahamu kidogo Lilambo.

Lilambo ni kata moja wapo kati ya kata za Songea njia ya kuelekea Peramiho. Tabia zilizopo ambazo utaziona na kuzigundua kadri unavyoishi na mambo kadhaa:

1. Watu wanafuga mbuzi na kuku lakini huwezi kukuta mazizi ya Mbuzi. Watu wanalala na mifugo hii ndani kuhofia wizi.

2. Wenyeji hupendelea sana uwape vitu lakini sio wao kutoa vitu.

3. Tofauti na maeneo mengine, wanaume husifika kwa wizi, lakini kwa Lilambo ni haki sawa yaani 50 kwa 50. Wizi huu ni pamoja na mifugo niliyotaja na wizi wa vitu vya ndani.

4. Si rahisi ukasikilizana na mtu na mkaelewana vyema kwa kupigiana simu kwani maeneo mengi yanasumbua mtandao. Kando kando ya barabara ya lami mtandao unashika vizuri.

5. Usijisumbue kutumia tigo kwa ajili ya ku dowload vitu.

6. Hakuna zahanati ya kijiji.

7. Kuna changamoto ya shida ya maji.

8. Unapoangalia video funga mapazia na mlango wa sebule vizuri kama hutaki kero ya watoto kuchungulia ndani. Kama utawakaribisha waangalie video uwe makini maana watoto wengi hutumwa kupeleleza.

9. Nyumba zenye umeme ni chache

10. Ni kawaida ukuiwa na mazao shambani ng'ombe wanaachwa huru kula mazao hivyo uwe makini.

Kwa anayejua anaweza kuongeza
 
natamani kupafahamu Tandahimba..
ahsante mleta uzi,
vipi hali ya uchumi?
eneo hilo liko sehemu gani ya nchi hii?
 
Haujamalizia..Lilambo kuna vilabu vingi sana vya ulanzi..wakazi wengi wa lilambo ni walevi kupindukia...kila mara hutokea ugomvi kati ya wakazi wa lilambo na wajeda wa kikosi jirani...lilambo imepakana na mlima litapwasi ambao ni sehemu kuu ya wakazi wa lilambo kutambika...wengi wa walevi wa lilambo ni wajeda waliostaafu...mengine ongezea
 
Umbali sijajua ila kwa nauli ya daladala ni jelo tu.Lilambo, songea,ruvuma kusini mwa Tanzania
 
Umbali sijajua ila kwa nauli ya daladala ni jelo tu.Lilambo, songea,ruvuma kusini mwa Tanzania

Pastor habari, kuna wakati nime-login in JF pale cafe za St. Augustine Songea, nikakuta akaunti yako ya JF haikuwa logged out nikakusaidia ku log out then nikaendelea na mambo yangu.

Nafahamu kile ni kijiwe chako, jitahidi kuzingatia hili next time mkuu ili kulinda privacy zako na usalama wako kwa ujumla.

Ni hayo tu mkuu, kuhusiana na mada nitarudi kuchangia baadae, Songea nimekaa sana hasa maeneo hayo ya Lizaboni, Ruhuwiko, Kigonsera n.k
 
Mm nimekaa sana Seedfarm bt Peramiho ndo kijijin kwetu, sema kitambo sana sijatimba maeneo hayo
 
Sasa wewe unaanza kuilezea lilambo kana kwamba kila mtu anajua,ilibidi uanze na introduction lilambo ni kitu gani kipo wapi ndo uanze mambo yako..
 
Pastor habari, kuna wakati nime-login in JF pale cafe za St. Augustine Songea, nikakuta akaunti yako ya JF haikuwa logged out nikakusaidia ku log out then nikaendelea na mambo yangu.

Nafahamu kile ni kijiwe chako, jitahidi kuzingatia hili next time mkuu ili kulinda privacy zako na usalama wako kwa ujumla.

Ni hayo tu mkuu, kuhusiana na mada nitarudi kuchangia baadae, Songea nimekaa sana hasa maeneo hayo ya Lizaboni, Ruhuwiko, Kigonsera n.k
Nashukuru mkuu ndugu yangu @chakii.Inaonesha wewe unanifahamu sana.Jitahidi tufahamiane.Labda unitoe lunch siku moja kwule kwenye kitimoto songea girls kamanda!
 
Nashukuru mkuu ndugu yangu @chakii.Inaonesha wewe unanifahamu sana.Jitahidi tufahamiane.Labda unitoe lunch siku moja kwule kwenye kitimoto songea girls kamanda!
umenikumbusha kitimoto ya kule,ilikuwa nikitoka pale nakuja kula bia magereza hapa then huyo nazama geto mahenge
 
Dah jamani huku kitimoto raha sana.Ila kuomba lunch sio noma kwani watanzania wote ni familia moja tunapendana
 
Lilambo njia ya kwenda mbinga,mbambabay. Umenikumbusha makaba na pitiku.
Nimeikumbuka Songea yangu.
 
Back
Top Bottom