Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
- Thread starter
- #21
Rev.Kishoka,
..mbona Kawawa aliendelea kupeta hata baada ya kuboronga ktk operesheni vijiji?
..mbona Sokoine aliendelea kupeta hata baada ya kumpa Mwalimu ushauri mbaya kuhusu matatizo ya uchumi/wahujumu uchumi? Waliompa ushauri mzuri wakina Mtei wakafukuzwa kazi?
..mbona yule Mkuu wa Mkoa aliyeshtakiwa na wananchi kwa kuzini na watoto wa shule hakufukuzwa kazi na Baba wa Taifa? halafu mnashangaa ya babu seya.
..mbona yule Afisa wa Polisi alipelekwa Ubalozini baada ya kubainika kwamba alikanyaga na kuua mtu kwa gari? leo mnashangaa ya Ditopile.
..Kassim Hanga alionekana kwa mara ya mwisho akiwa hai ktk mkutano wa hadhara ambapo Mwalimu alimtukana kama mtoto mdogo. Hanga ametoweka, inasemekana aliuawa. Kaburi lake liko wapi? Katika watu wote "waliopotelea" Zenj nadhani Mwalimu had to account for Kassim Hanga.
..Labda Kanisa Katoliki watueleze alipozikwa Kassim Hanga kabla ya kumsimika Utakatifu Mwalimu Nyerere.
Ukishapata majibu, utabadilisha msimamo?