idd ninga=NASRA MVUNGI (shairi)

idd ninga=NASRA MVUNGI (shairi)

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,854
Habari MWANANCHI.
Jina langu ni Iddy Ninga ninaishi
Tengeru Arusha.
Nimetuma shairi hili kama
kumbukumbu ya mateso na ukatili
alofanyiwa
mtoto Nasra mvungi.
1>shairi naliandika,machozi
yanidondoka.
Ubaya nikikumbuka,jinsi
ulivyotendeka.
Mtoto aliteseka,mateso kama mateka.
Mungu mlaze peponi,mtoto nasra
mvungi.
2>miaka mingi kashani,mtoto
aliteseka.
Zaidi ya gerezani,machungu bila
kucheka.
Aliumia moyoni,hakupata kusikika.
Mungu mlaze peponi,mtoto nasra
mvungi.
3>mateso aloyapata,magumu
kusimulia.
Kama yangeja kupata,maishani
ungelia.
Magonywa yakampata,kafa huku
analia.
Mungu mlaze peponi, mtoto nasra
mvungi.
4>nasra hajafanya kosa,baya
akahukumiwa.
Hakuyafanya makosa,nakuwa
mtuhumiwa.
Bila hata ya makosa,leo ameshauliwa.
Mungu mlaze peponi,mtoto nasra
mvungi.
5>haki yake ipo wapi ,labda kaificha
nani ?.
Na sheria iko wapi,hukumu
mahakamani ?.
Watetezi mpo wapi,hamlioni jamani ?
Mungu mlaze peponi,mtoto nasra
mvungi.
Jina la shairi:NASRA MVUNGI.
Mawasiliano yangu:+255755519736/
email:iddyallyninga@Gmail.com
Reply
 
Wapo wengi kama Nasra Mvungi,wazazi wavuta bangi watoto kuwapa mirungi..........Kama kuna kitu kilichonishinda huku duniani ni kuandika shairi.
Rafiki yangu Idd Ninga, hiyo ndo reply yangu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom