Idd Ninga= MLEVI KUHAMA BAA

Idd Ninga= MLEVI KUHAMA BAA

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,854
Ifuatayo ni shairi liitwalo MLEVI KUHAMA BAA lililoandikwa na Idd ninga.
Tutiririke sote.
1>yapasa kutafakari,ufikiri kimakini.
Mtindo usikariri,udadisi akilini.
Namba moja si sifuri,hito shinda duniani.
Mlevi kuhama baa,siyo kaacha kulewa.


2>pombe nyingi alokunywa,imeingia damuni.
Harufu ya chake kinywa,jadilini mzimuni.
Ukweli wabinywa binywa,uongo u kabatini.
Mlevi kuhama baa,siyo kaacha kulewa.


3>tangu wake udogoni,alikunywa pombe kali.
Amechafuka rohoni,ukweli we si kamili.
Aibu yake machoni,haipimwi kwa ramli.
Mlevi kuhama baa,siyo kaacha kulewa.


4>imekanywa vitabuni,pombe jambo la haramu.
Msimwoshe hadharani,eti yeye wa muhimu.
Ila kweli duniani,ni rahisi siyo ngumu.
Mlevi kuhama baa,siyo kaacha kulewa.


5>gongo ni chake kinywaji,soda kwake siyo togwa.
Anachukia ulaji,kama vile amelogwa.
Mama muza si mpaji,ila sikio katogwa.
Mlevi kuhama baa,siyo kaacha kulewa.


Shairi=MLEVI KAHAMA BAA.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0755519736 Au 06555197361
 
Back
Top Bottom