Idd ninga=KUMI KUMI (shairi)

Idd ninga=KUMI KUMI (shairi)

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,854
1>kila mmoja anajua,shida tulizozipata.
Tuliunguzwa na jua,tukafanywa si mabata.
Tena tusijeungua,na misiba tukapata.
Kumi kumi iwe vyema,mabadiliko ni sasa.
2>hutakiwi hutakiwi,mbona wajipendekeza.
Unang'ara kama kiwi,hilo mi nakudokeza.
Kamwe hausamehewi,anza leo jipunguza.
Kumi kumi iwe vyema,mabadiliko ni sasa.
3>mitume si hadhi yako,wewe damu ya farao.
Ondoka hauna chako,nitakunasa kibao.
Upi utakaso wako,huoshwi kwa malimao.
Kumi kumi iwe vyema,mabadiliko ni sasa.
4>weupe wako usoni,hautofika kichwani.
Na kama upo kichwani,hautofika rohoni.
Ulitwibia nyumbani,tukuweke ukooni ?
Kumi kumi iwe vyema,mabadiliko ni sasa.
5>haya sasa zindukeni,zimwi tulikataeni.
Tutambike mbuyuni,zimwi hili ni shetani.
Zimwi lipo hesabuni,moja tisa hesabuni.
Kumi kumi iwe vyema,mabadiliko ni sasa.
Shairi=KUMI KUMI.
Mtunzi=Iddy Ninga wa Tengeru Arusha.
0755519736 au 0655519736
 
Back
Top Bottom