Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,539
- 4,854
-----kufuli-----
=nyumbani alipofika,mke wangu
kamusia.
Kwa maneno ya hakika,baba
akamuambia.
Mumeo atapofika,usiache
mgusia.
Kufuli abadilishe,nyumba ije
kupendeza.
=mke nae kaneleza,baba
alichomwambi.
Nyumba itaja pendeza,tena itaja
vutia.
Ila nikija kucheza,maisha
nitajutia.
Kufuli yanitatiza,bado
sijaielewa.
=nyumba yangu ya kitasa,wala
haina kufuli.
Nimewaza hadi sasa,najihisi
nimefeli.
Napata majibu tasa,yaumizayo
akili.
Kufuli yanitatiza,bado
sijaielewa.
=nawaomba washairi,mnipe jibu
makini.
Nisije kupata shari,nikaumia
nyumbani.
Baya likaja kujiri,nikalia
maishani.
Kufuli kufuli gani,mimi
linanitatiza.
~ ~ ~ ~ ~ ~ ~ ~ ~ ~
=nyumbani alipofika,mke wangu
kamusia.
Kwa maneno ya hakika,baba
akamuambia.
Mumeo atapofika,usiache
mgusia.
Kufuli abadilishe,nyumba ije
kupendeza.
=mke nae kaneleza,baba
alichomwambi.
Nyumba itaja pendeza,tena itaja
vutia.
Ila nikija kucheza,maisha
nitajutia.
Kufuli yanitatiza,bado
sijaielewa.
=nyumba yangu ya kitasa,wala
haina kufuli.
Nimewaza hadi sasa,najihisi
nimefeli.
Napata majibu tasa,yaumizayo
akili.
Kufuli yanitatiza,bado
sijaielewa.
=nawaomba washairi,mnipe jibu
makini.
Nisije kupata shari,nikaumia
nyumbani.
Baya likaja kujiri,nikalia
maishani.
Kufuli kufuli gani,mimi
linanitatiza.
~ ~ ~ ~ ~ ~ ~ ~ ~ ~