Idd Azan akana kuomba radhi CCM! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Idd Azan akana kuomba radhi CCM!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 5, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Imeandikwa na Oscar Job;
  Tarehe: 4th June 2011  MBUNGE wa Kinondoni, Idd Azzan, amekanusha kuomba radhi kwa uongozi wa CCM Mkoa kutokana na kauli yake aliyowahi kuitoa, kutaka uongozi huo ujivue gamba kwa ajili ya kulinda maslahi ya chama hicho.

  Pia amemtaka Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kilumbe Ng'enda, kuthibitisha kama kweli anauza unga, vinginevyo atampeleka mahakamani kwa madai ya kumchafua yeye, familia yake, pamoja na wapiga kura wake.

  Azzan alitoa kauli hiyo jana katika ofisi za CCM tawi la Mchangani kata ya Makumbusho, wakati wa sherehe za kuwapongeza vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wa wilaya hiyo, walioibuka na ubingwa katika michezo mbalimbali iliyoandaliwa na umoja huo Mkoa wa Dar es Salaam.

  Alisisitiza kuwa viongozi hao wanapaswa wajivue gamba kwa ajili ya kulinda maslahi ya chama hicho.

  Katika sherehe hizo zilizohudhuriwa pia na baadhi ya vijana wa CCM kutoka wilaya za Temeke na Ilala, Azzan alisema malengo yake si kuleta mgongano wa maneno ndani ya chama hicho, isipokuwa kuna watu wana chuki binafsi na yeye.

  Alisema yeye kama mbunge aliyechaguliwa kwa kishindo na wananchi wa Kinondoni, anachokiangalia zaidi ni kujenga mshikamano ndani ya chama hicho ili kuendelea kukipa ushindi.

  Mbali na kukanusha taarifa hizo, Azzan pia alitangaza kuwania urais mwaka 2025, huku akiwafananisha watu wanaomchafulia katika nafasi yake kuwa ni sawa na ‘fisi anayesubiria mkono wake udondoke'.

  "Nitafuata nyayo za Rais Kikwete, yeye alikaa bungeni vipindi vitatu vya kuchaguliwa, na kingine kimoja cha kuteuliwa na baadaye akagombea urais, hiki ni kipindi changu cha pili, itakapofika 2025 nitawania urais kufuata nyayo zake," alisema Azzan.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Kinondoni, Aron Mwaikambo, aliwataka wanachama wa chama hicho kudumisha mshikamano kwa lengo la kukijengea heshima ya chama hicho tawala.
   
 2. k

  kiche JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hilo la kugombea urais naona umefika mbali!!
   
 3. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Nadhan utagombea urais lakini si kwa Tanzania!
   
 4. T

  Technology JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 733
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  he has never been serious
   
 5. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #5
  Jun 5, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Asijeakachukuliwa na marekani kama alivyochukuliwa Noriega wa Panama!! Marekani wametangaza vita dhidi ya wauza Unga.
   
 6. nkasoukumu

  nkasoukumu JF-Expert Member

  #6
  Jun 5, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 692
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 60
  Anauza unga wa namna gani sembe au dona
   
 7. kishoreda

  kishoreda Senior Member

  #7
  Jun 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 176
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Urais 2025??? Labda ahamie CDM tunaweza kumfikiria sio Chama cha Magamba
   
 8. Kwamex

  Kwamex JF-Expert Member

  #8
  Jun 5, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 378
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Anataka urais wa chama cha wauza unga...wa sembe 2025.
   
 9. mchapa shughuli

  mchapa shughuli JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 321
  Trophy Points: 80
  Urais wa chama cha ndondi au,kwanza aende shule akasome hatuwezi ongozwa na mtu wa kidato cha pili aache utani..
   
 10. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #10
  Jun 5, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Urahisi!!!!!!!!!!!!!!!
   
 11. CPU

  CPU JF Gold Member

  #11
  Jun 5, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hivi nani kamhakikishia 2025 atakuwa hai??
  Hata hili la kukanusha kuomba radhi mbona limechelewa sana?
  Sihasa bana . . .
   
 12. m

  malimamalima Member

  #12
  Jun 5, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  idd azam aliambiwa aidha athibitishe matamshi yake la sivyo aombe radhi, baada ya kushindwa kuthibitisha akaomba radhi lakini utaratibu wa kanuni unasema mtenda kosa akishapewa adhabu hata akiomba radhi basi suala hilo linajadiliwa baada ya miezi sita kupita. Hili limemchanganya iddd azam kwani itabidi adhabu aendelee kuitumikia mpaka miezi sita ipite na ndiyo maana ameona ngoja akanushe kwamba aliomba radhi!!!

  eti anataka kipindi cha tatu ubunge?? kweli anatania safari hii atastaajabu na nguvu ya umma...pia anadai alishinda kwa kishindo? mgombea wa cdm hakufanya kampeni kabisa na bado alimpelekesha idd azam sana na idd kujitapa kwamba alishinda kwa kishindo ni jambo la kuchekesha sana. Mwaka 2015 chadema wasimamishe mgombea aliyesimama bac jimbo litakuwa la chadema.
   
Loading...