Idara ya Uhamiaji inafanya zani gani?

Idara ya Uhamiaji inafanya zani gani?

bullet proof

Member
Joined
Sep 19, 2012
Posts
57
Reaction score
35
Zoezi linaloendelea nchini, la kuwakamata na kuwafukuza nchi wahamiaji haramu, limenifanya nifikiri juu ya ufanisi na hata uhalali wa idara hii nchini.

Taarifa zinaonyesha idadi kubwa ya wahamiaji haramu waliokamatwa katika msako unaondelea. Hili limenifanya ni hoji uhalali wa kuendelea kuwa na idara hii nchini, kwanini isivunjwe tu na shughuli za idara hii zifanywe na idara au vikosi vingine kama ilivyokuwa mwanzo katika jeshi la polisi?

Taarifa nyingi za uhamiaji hutolewa na jeshi la polisi nchini. Ukisikia sehemu wamekamatwa wahamiaji basi huwa wamekamatwa na polisi. Wale wanaokamatwa na Uhamiaji hufanywa "deal" tu na ndo maana tunaona rundo hili la wahamiaji haramu nchini.

Nashauri shughuli za idara hii zihamishiwe ofisi nyingine hasa ya usalama wa taifa au polisi kama zamani shughuli hizi zilivyokuwa zikifanywa na jeshi la polisi. Ulinzi wa mipaka utafanywa na jeshi la wananchi ambao ndio wenye dhamana ya kulinda mipaka na utoaji wa vibali mbalimbali vya uhamiaji kama vile passports, resident permits nk zitolewe na (kitengo) cha uhamiaji ambacho kitakuwa ndani ya usalama wa taifa/polisi hii ni kama ilivyo katika nchi nyingi duniani i.e huduma za uhamiaji na uraia ziko katika idara ya usalama wa taifa/polisi
 
suala la ulinzi na usalama ni la kila raia,kuanzia wewe ukimuona mhamiaji haramu na sio mhamiaji haramu tu hata jambazi au kibaka anaye ibia watu kariakoo toa taarifa kwa proper authority,jamaa uhamiaji nawakubali wanafanya kazi vizuri.na pia tz we are bordering with countries in rich of problems.the solution is to tell heads those countries to live in peace.if we will succed there will be no more irregular immigrants
 
Back
Top Bottom