Idara/Kitengo cha Sheria kifanyiwe mabadiliko

Peramiho yetu

JF-Expert Member
May 25, 2018
5,304
14,913
Habari wanabodi,

Kama mnavyoona kukuru kakara za usajir za mchezaj wa Yanga bwana Feisal Salum (Fei Toto) kwenda Azam zinavyowatesa wana Yanga na hii ilianzia toka kwa mtukutu Bernad Morrison kwenda Simba.

Inaonesha wazi idara ya sheria au kitengo cha sheria kinapwaya sana pale Jangwani, hawako makini juu ya mikataba ya wachezaji wao.

Mchezaj kama Fei Toto kuuzwa kwa mil 100 ni aibu sana, pesa hii ina thaman ya Kibu Denga pale Msimbaz au Sadala Lipangile na si Fei Toto.

Sjui wanawaza nn hawa wanasheria wa Yanga nadhani wapo pale kwa vimemo vya baba kanituma.

Hawa mabwana hawajawah kishinda hata kesi ya kuku lakn wapo pale Yanga wakilipwa mamilioni ya pesa.

Ni muda sasa wakukimulika hiki kitengo ili kilete tija.
 
Umewaza Kama Mimi. Hawa Jamaa wa kitenge Cha Sheria hawako serious
 
Jamaa wa mchongo sana hao. Kama si wanasheria. Yaan mikataba kama ya nyumba za kupanga.

Mm niljua baada ya sakata la bm33wangeamka kumbr laah. Mbona wasomi wako wengi tu wanakwama wapi viongozi?
 
Ukweli anayeangaika Ni Fei na Azam,wanayanga wanaaminishwa na wachambuzi mchongo na wamakolo kuwa Yanga inaangaika hakuna kitu Kama hicho.kwa maslahi aliyoahidiwa Fei toto angekuwa Chamanzi Kama mkataba unamruhusu.katika mikataba unapoongeza thamani ya mchezaji inaendana na ongezeko la mshahara,wengi mnasahau Yanga 2020 hiyo hela ilikuwa nyingi Sana kwa thamani ya Fei wa 2020.kama Fei ataondoka kwa milioni 112 Ni kweli kitengo Cha sheria na hata uongozi utakuwa umekosea.alipaswa kuboreshewa maslahi na kuongeza thamani yake kwenye mkataba.kama wanaweza kumuuza kwa Bei nzuri auzwe tu
Asilipwe kuliko thamani yake ikaathiri majadiliano ya wachezaji wengine.Aziz ki anatosha kila shuti watatapika Ni kuwahi.
 
Kwa hiyo ameshaondoka? Au tumtarajie kutambulishwa kwenye mashindano ya Mapinduzi?
Maana kama rais wa klabu ameshatoa tamko la kutokuwepo kwa shida yoyote ile ya kimkataba na huyo mchezaji! Na hao Azam wenyewe nao wameshakanusha kuhusu huo usajili!


Sijui ni kwa nini bado kuna watu mnaendelea kukaza shingo.
 
Moderators naomba heading.isomeke IDARA YA SHERIA YA KLABU YA YANGA IFANYIWE MAREKEBISHO
Wamerekebisha.Lakini,mara nyingine usitolee mifano ya mchezaji mmoja kwa thamani kumlinganisha na mwingine wa timu nyingine.Umgeishia tu kuandika Feisal ana thamani kubwa na hata ungeitaja hiyo thamani.Yale ya jana siyo leo!
 
Back
Top Bottom