Idadi ya wabunge wanaoaga yazidi kuongezeka

Idadi ya wabunge wanaoaga yazidi kuongezeka

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,793
Reaction score
7,165
Kama kawaida yao Wabunge ambao wameaga rasmi inaongezeka, hii inatoa na msukumo wa kuwania nafasi za juu.

Tunataka wengine waliozeeka, waliochokwa kujipima mapema waagwe kwa amani na cheleko, wasisubiri moto wa vijana wakaja kuumiza pension zao.

Hatutaki tena wabunge njaa kujaza ofisi wakiomba.ref. Makinda mpaka sasa walioaga kwa hiari ni Mwandosya, Zitto, Mahanga, Sitta huyo anapima upepo wa UKAWA
 
ha ha ha ha raha tupu, maana kila kukicha kuna habari mpya na motomoto. 6 anapima upepo au? amekuwa kama kanguchiro kanachungulia kwa mbaaaaali kwenye kashimo
 
ha ha ha ha raha tupu, maana kila kukicha kuna habari mpya na motomoto. 6 anapima upepo au? amekuwa kama kanguchiro kanachungulia kwa mbaaaaali kwenye kashimo

6 anatumia kick ya mabehewa feki ya mwakyembe🙂 tayari lowasa kaaga pia
 
Nasikia TLP wamemvua mzee nanihii uanachama. Si naye atamke kungatuka tu?
 
Kuna tetesi kuwa Richard Ndasa wa Sumve naye ameona upepo wa UKAWA .

Jimboni kwake ni mkali sasa anajiandaa kuaga ili asipate aibu kwenye matokeo.
 
Tuna wakaribisha mtaani yaani juzi nilipopata ajali na kupasukapasuka asee nimezidi kuichukia Serikali ya ccm. Maana bila ule mgomo nisingetimbuliwa hivi.
 
Naambiwa Dj nae anampango wa kuachia ngazi....Hai pamekuwa pagumu
 
Kama vipi tuorozeshe majina ya wabunge waliopoteza mvuto, tuwakumbushe waage mapema maana badae wasije sema hatukuwaambia.
 
Babu 6 kama kweli hupendi kufedheheshwa jimboni kwako, nawewe njoo uage Ntakamulenga hajakaa vizuri upande wako wala kwa mtu yeyote anayetoka kwenye malango yako!
 
Pro. MARK JAMES MWANDOSYA mbunge wa Rungwe mashariki ameaga sio kuwa kapoteza mvuto bali ni kwa hiyo nafasi ya juu kwani hakuna mbunge mwenye mvuto katika jimbo lake huyo mzee na alipowaaga wananchi wake wabunge 11 wa CCM mpaka sasa wanaiwania nafari hiyo.
 
Shibuda yeye amesema haigi mpaka aone mwisho wake.

Sasa hivi anaimarisha TADEA huko Maswa/Malampaka
 
Naye mbunge wa Rungwe magharibi Pro. David Mwakyusa naye pia anajiandaa kuachia jimbo hilo na tayari mtu ameandaliwa na CCM anaitwa Saul Pataya mwenyeji wa Ushirika Tukuyu japo wanasema upepo unavuma vizuri kwa UKAWA kama atasimama mzee wa UPAKO.
 
Kama kawaida yao wabunge ambao wameaga rasmi inaongezeka, hii inatona na msukumo wa kuwania nafasi za juu. Tunataka wengine waliozeeka, waliochokwa kujipima mapema waagwe kwa amani na cheleko, wasisubiri moto wa vijana wakaja kuumiza pension zao. Hatutaki tena wabunge njaa kujaza ofisi wakiomba.ref. Makinda mpaka sasa walioaga kwa hiari ni mwandosya, zitto, mahanga, sitta huyo anapima upepo wa ukawa.

Zitto amesema anagombea ubunge tena!
 
Huku geita mjin mbunge wa ccm ndugu max .alipoona matokeo ya serikali za mitaa aliaga rasmi.
 
Back
Top Bottom