Idadi ya mateja Zanzibar inatisha

Idadi ya mateja Zanzibar inatisha

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,992
Reaction score
12,029
Fighting heroin addiction in conservative Zanzibar

jackie.JPG
Jackie cradles her infant in a room at one of the sober houses

Jackie held her one month old child to her chest. If for no other reason, the new life pressed against her had to be why she stopped using. After eight years of heroin addiction, she'd been clean for three weeks.

"Let me be clear, this isn't my first time in a sober house," she said from a treatment centre in Zanzibar, an island off the coast of Tanzania where, according to the Revolutionary Government of Zanzibar,an estimated 7 percent of the one million residents are drug addicts.

This is one of the highest rates in the world. Jackie's determined that this will be her last time.

"The first fix is not the solution, I'm staying clean for myself and for my baby. I don't want to lose her, I can't stay sane if I know she's being raised by another person."

Jackie, whose surname has not been published to protect her privacy, has been in and out of treatment centres seven times.

Zanzibar has launched an aggressive campaign to deal with its drug problem but everyone is confounded by how to help female addicts such as Jackie, whose treatment always seems to end the same way - back on the streets using.

In the 1990s, international drug smuggling routes began moving heroin from Afghanistan through East Africa's poorly regulated ports on the way to the US and Europe.

It wasn't long before dirt-cheap narcotics leaked into the population - affordable even for the more than 40 percent of the population living below the poverty line.

The help available to addicts in Zanzibar is rare in the rest of Africa, where onlyone in 18 drug users have access to help services, as compared to one in three in North America.

This has drawn addicts from across East Africa and as far as Oman to seek help.
Zanzibar has a network of 11 sober houses that have treated more than 3,000 people, harm-reduction programmes for those still using, daily 12-step meetings around the island, and for the past two months, a methadone clinic.

But women are slipping through the cracks of these services. Only one of the methadone clinic's 30 or so patients is a woman, and while the men's sober houses range from 20 to 30 who recover, the two women's clinics have only three or four who kick the habit.

"Everywhere you go you see this phenomenon of women not getting to treatment, or they drop out of treatment, and if you ask them why they say they are uncomfortable, they say, 'we're stigmatised and we have no services that address our needs,'" saidNabila el-Bassel a professor at Columbia University who studies female drug use.

Globally, limited research exists on female drug addicts.

"There is a huge, huge gap in knowledge about women who use drugs everywhere," Bassel said. "We need to stop using women as variables."

Women constitute a minority of drug users, but they are likely under-reported and they also experience devastating consequences of addiction: female injection drug users face higher mortality rates, higher risks of HIV infection, and faster progression to dependency.

Female drug users are stigmatised around the world but particularly in conservative Zanzibar, where 99 percent of the population is Muslim.

"Traditionally, women are doubly stigmatised - being a woman and being an addict at the same time," said Abdulrahman Abdullah, the general secretary of Recovery Community Zanzibar.

"Women feel embarrassed, ashamed, they're dealing with religion, culture, tradition, prostitution, rape."

[TABLE="class: image"]
[TR]
[TD] mbaba.JPG [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: caption"]Abdulrahman Abdullah reads from Narcotics Anonymous during a 12-step meeting in Zanzibar[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Female drug users are likely to have been sexually assaulted in the past and sexually assaulted when they're using. Women often exchange sex for drugs, pairing two sins that make them irredeemable in the eyes of many of the island's residents.

"When I was using I'd go to Maskani, I wouldn't have anything, no money," Jackie said, referring to the place where she bought drugs.

"Don't worry Jackie,' they'd say, 'I have money,' they'd buy me drugs," she said recounting her conversation with male drug users.

"Are you going to sleep with me?" Jackie recounted saying as she balanced her baby on her lap, bottle-feeding her. Women are typically introduced to injection drugs by a male partner with whom they often share needles.

Injection drug user rates have ballooned to 16 percent, and among sex workers to 12.8 percent in the last decade.

"Anybody can find themselves into drug addiction [but it's more likely] with traumatic effects of domestic violence, sexual assault, physical abuse, single parents," said Abdullah. "You try to cover your feelings, you try to escape."

Hadija and Sandra sat outside Malaika Sober House, one of the island's two clinics for women. They had just finished a 12-step meeting and the women traded stories while smoking cigarettes.

[TABLE="class: image"]
[TR]
[TD] wadada.JPG [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: caption"]Sandra and Hadija outside Malaika Sober House, one of the island's two centres for women
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Stretched across the door step was a woman who periodically groaned as the pain of withdrawal rustled her consciousness.

This is Hadija's second time at Malaika, she relapsed a few months ago after staying sober for more than two years.

"We started to establish the women's programme in 2011 and very few have sustained recovery, more have collapsed along the way," Abdullah said of the women's sober houses. "Its been a good programme with very few clients."

Sandra misses her two children. It is illegal for children to be in sober houses in Zanzibar, a barrier for many women.

"For now, they're better off without me, especially the youngest one," Sandra said.

"Oh god, I used to take her with me to places where people smoked dope. I need to focus on my recovery, a year isn't a long time if I know it means I can have the rest of my life with them," she said.

Because of her baby and because in the past Jackie was caught with heroin at the sober house, she's left and is looking for an apartment of her own.

"My sister calls me every morning, 'Jackie please don't use today,'" Jackie said. "Sometimes I talk to myself when I'm thinking about using: 'Don't do this Jackie, don't do it.'"

Source: Aljazeera.com
 
Hii akili gani unatuletea hapa😡 kichwa cha habari kiswahili maelezo kikoloni!! shenzytype
 
Unategemea nini. Viongozi wa Zanzibar wanachaguliwa Dodoma sio Zanzibar, hivyo wakiingia madarakani wanasevu interest za wakubwa wao Dodoma, Nani anajali kama zanzibar hakuna hata kiwanda kimoja, ajira wanawetu watapata wapi ? hawawezi kuwa wachuuzi wote au wote wawe wavuvi. Matokeo yake ni kukaa vijiweni na kuanza umalay , ujambaz na madawa ya kulevya. Ni taifa la vijana walio kata tamaa.
Mnajua kwamba Zanzibar watu hula mlo mmoja kwa siku ? Tembelea siku moja uhakikishe.
 
Jambo hili haliwahalalishii ao vijana wa kizanzibar kua wabwiya unga....mbona hawabwi unga vijana wa kisiwani mafia...wamejiendekeza hawataki kufanya kazi wameishia ivo...

alafu ilo la kua zanzibar wanakula mlo mmoja ni uongo mkubwa...utafiti huu umefanyika lini..ripoti zipo wapi kama si uongo...mim mwenyewe ni mzanzibar nimeishi mwaka wa 26 sasa tangu nizaliwe ili jambo halipo..inawezekana kwa baadhi ya watu/kaya chache ambapo ni kawaida kwa jamii maskini zozote afrika na asia,..ila sio kugeneralize...ni uongo...ama labda iwe zama za miaka mimi sikuzaliwa.

vijana wa kizanzibar wakae wasome, wafanye kazi kujikwamua na maisha...sio kukaa vibarazani na maskani,..kuanza kujaribu jaribu kuvuta vilevi vya ajabu...na hii ndio tabia za kaka/wadogo zetu walio wengi..kufuata mkumbo na kutokuwajibika na ujana wao au walezi wao kutowajibika ipasavyo na vijana wao
 
Mkuu usiwe jazbar,kwa hali ya maisha ya sasa ya mzanibar ni mbaya kuliko kipindi chochote kilicho pita,kama huamini hilo njoo tukutane mtaa wowote hapa zanzibar kisha tupite mitaani na ikibidi tupite nyumba hadi nyumba tuwaulize wananchi juu ya maisha wanayo ishi,wazanzibar wamefungwa kamba za miguu baharini na mkoloni mweusi kisha mkoloni anamtaka mzanzibar aogolee kwenye bahari.
 
Jambo hili haliwahalalishii ao vijana wa kizanzibar kua wabwiya unga....mbona hawabwi unga vijana wa kisiwani mafia...wamejiendekeza hawataki kufanya kazi wameishia ivo...

alafu ilo la kua zanzibar wanakula mlo mmoja ni uongo mkubwa...utafiti huu umefanyika lini..ripoti zipo wapi kama si uongo...mim mwenyewe ni mzanzibar nimeishi mwaka wa 26 sasa tangu nizaliwe ili jambo halipo..inawezekana kwa baadhi ya watu/kaya chache ambapo ni kawaida kwa jamii maskini zozote afrika na asia,..ila sio kugeneralize...ni uongo...ama labda iwe zama za miaka mimi sikuzaliwa.

vijana wa kizanzibar wakae wasome, wafanye kazi kujikwamua na maisha...sio kukaa vibarazani na maskani,..kuanza kujaribu jaribu kuvuta vilevi vya ajabu...na hii ndio tabia za kaka/wadogo zetu walio wengi..kufuata mkumbo na kutokuwajibika na ujana wao au walezi wao kutowajibika ipasavyo na vijana wao

Umewahi kujiuliza hayo mada yanaingizwa na nani hapo zanzibar,kama yakulaumiwa c serekali unadhani ni nani wa kulaumiwa juu ya uingizaji wa madawa hayo?
 
Jambo hili haliwahalalishii ao vijana wa kizanzibar kua wabwiya unga....mbona hawabwi unga vijana wa kisiwani mafia...wamejiendekeza hawataki kufanya kazi wameishia ivo...

alafu ilo la kua zanzibar wanakula mlo mmoja ni uongo mkubwa...utafiti huu umefanyika lini..ripoti zipo wapi kama si uongo...mim mwenyewe ni mzanzibar nimeishi mwaka wa 26 sasa tangu nizaliwe ili jambo halipo..inawezekana kwa baadhi ya watu/kaya chache ambapo ni kawaida kwa jamii maskini zozote afrika na asia,..ila sio kugeneralize...ni uongo...ama labda iwe zama za miaka mimi sikuzaliwa.

vijana wa kizanzibar wakae wasome, wafanye kazi kujikwamua na maisha...sio kukaa vibarazani na maskani,..kuanza kujaribu jaribu kuvuta vilevi vya ajabu...na hii ndio tabia za kaka/wadogo zetu walio wengi..kufuata mkumbo na kutokuwajibika na ujana wao au walezi wao kutowajibika ipasavyo na vijana wao

Ustaadh inaelekea wewe ni mtoto wa wale wanaochaguliwa Dodoma, unahisi kijana wa Zanzibar anaweza kuomba kazi gani hapo Zanzibar ? kuna kiwanda gani hapo ? kwenye mahoteli watawala wame import wakenya nyie mmeachiwa uchangudoa kama hudma kwa watalii. Nchi yako ina import mpaka nyanya na vitunguu wewe unatetea uongozi. Kweli Zanzibar hamuwezi kuzalisha vitunguu kweli ?
Nimekaa Zanzibar na ni kweli watu hula mara moja tu saa tisa mchana, kuna nyie wachache ambao mnamudu hata kwenda forodhani kula mishkaki lkn sio wengi+
 
Unategemea nini. Viongozi wa Zanzibar wanachaguliwa Dodoma sio Zanzibar, hivyo wakiingia madarakani wanasevu interest za wakubwa wao Dodoma, Nani anajali kama zanzibar hakuna hata kiwanda kimoja, ajira wanawetu watapata wapi ? hawawezi kuwa wachuuzi wote au wote wawe wavuvi. Matokeo yake ni kukaa vijiweni na kuanza umalay , ujambaz na madawa ya kulevya. Ni taifa la vijana walio kata tamaa.
Mnajua kwamba Zanzibar watu hula mlo mmoja kwa siku ? Tembelea siku moja uhakikishe.

RAYUUUUUUUUUUUn,umemamilza
Ngoja nipige msumari kwa huyu mzushi.

Mleta mada kwanza upo sahihi kabisaaa,mateja Zanzibar wanatisha ni balaa.

Huyo anasema Zanzibar hakuna ajira,labda namie nimuambie.Visiwani umwinyi na usisi ndio unatia umaskini.

Zanzibar katika uwiano wa idadi ya watu na vijana na idadi ya Ajira zilizopo ni kubwa mno kwa vijana kuliko mkoa wowote Tanzania.
Zanzibar ina idadi ya Accommodations outlests(Hotels,Lodge,Bungalows)etc more than 100 zenye madaraja tofauti,kuna ajira direct na indirect.
Ukiangalia karibia 80% wafanyakazi wa Hotels ni kutoka bara.Ukiangalia sababu eti kazi ngum sana,na wengine kuingiza imani za dini kwamba unahudumia makafiri.Mbaya zaidi wengi hupenda kusema mishahara midogo na hao hao ukirudi mtaani wanakuomba miatano.Yaani kijana wa Kizanzibar wengi wao umaskini wanautaka wao wenyewe na wameukuta kwenye mfumo wa wazazi wao.Lakini Zanzibar ajira zipo kibaoooo kwenye Sekta ya utalii.
Almost 90% ya Suppliers kwenye mahotel ni watu kutoka Bara.

Tatizo ni kujitambua na kuwa Tayari.Nakumbuka mwaka 2002 wakati Chuo Cha utalii maruhubi kilitoa wahitim wengi pale.Na kuzuia trainees wa kutoka Dar kuja huku,basi huwezi amini trainees kutoka Chuo cha Maruhubi hapa Zanzibar walianza wote ila ndani ya mwenzi 70% wamekimbia.Hadi mwisho Hotels zikabakia na almost zero.Ikaona iachie sasa iwe huru.
Yakaja majembe kutoka Bara wakawa trained na wengi wakaanza kazi,yaani leo mtu akitoka Dar akia huku unasikia siku ya pili amepata ajira sehem fulani.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejitahidi sana tena sana kuhakikisha inalinda ajira za ndani lakini Vijana wake ndio wanaingusha.Sasa huwezi kubeba kitu kisichojibeba na wakati wewe unahitaji wawekezaji.Na wakati huo wawekezaji wanahitaji competents staffs wenye kujituma na kujitambua.

Kuhusu kula mlo mmoja,hii sio kigezo,nchi nyingi duniani hali hii ipo.Hapa ukileta Siasa ndio unapotea kabisaaa.
Maana hata hiyo Serikali ya umoja wa kitaifa ambayo wengi wenye mitazamo finyu waliona ndio nafuu,sasa wao wenyewe wameganda.Serikali hata ifanye juhudi vipi kama Kijana mwenyewe hujajitambua ni zero.

Mfano mwingine mdogo:Wakati Kampuni ya China inachukua Tender ya kujenga uwanja wa Ndege Zanzibar kwa awamu ya mwanzo,walitoa nafasi za kazi kwa vijana wa Zanzibar,nakumbua Waziri Samia Suluhu alikuwa kwenye nafasi.Basi Baada ya kuandikishwa wale Vijana wa kizanzibari,huwezi amini Kampuni iliganda ndani ya mwezi tu wafanyakazi wakasepa.Wanasema kazi ngum na mshahara mdogo.Ikabidi Waziri akatoa kibali watafute wafanyakazi wanapotaka.
Kampuni ikatoa offer hiyo Bara,vijana yenye kujua maisha kutoka Bara na wale Wazanzibar wachache waliobakia masugu wakapiga mzigo mwanzo mwisho.

Hapa ni kwamba ni kubadilisha mfumo,mambo ya watu kukaa pamoja kama kuku,hadi mtu unazeekea kwenu na kulishwa hadi unakuwa mkubwa ndio tatizo lake hili hata akili inakuwa imelala.Na ndio maana Zanzibar pia ukiulizia katika kila familia tano basi utakuta shoga au mtu anaesagwa.Maana kuna watu wanatumia mwanya huo wa vijana kutaka maisha rahisi sana na kwa wale watoto wa mama wasiojishulisha.

Kwa kujazi Jingine linalopoteza watu ni ndoa za kuoa na kuacha,ukweli kwa Zanzibar hii na Pemba,ndio sehem kwa Tanzania zinaongoza kwa kuoa na kuachana,unakuta mtoto wa miaka 19 au 20 anakuambia ameisha olewa ndoa ya pili au ya tatu.Sasa sikuelezi hao waliomzidi umri.
Hii yote bado ni msingi ya chini,mtu kuona na kuacha wala hushangawi kwa huku Zanzibar ni kitu cha kawaida sana.Malezi ya watoto wa kike na kiume katika kujitambua kiakili na kimaisha bado ni janga kubwa sana kwa huku kwetu.Maana wanarithi mfumo wameoukuta kwa wazee wao.
Wazanzibar wengi hupenda kuita watu wa bara kwamba wameshindikana na wazee wao kwa kuwaruhusu kuja kufanyakazi wakiwa peke yao,hasa wale wa kike.Sasa wanashindwa pia kujua kwamba Bara ukiishajitambua ni kwamba familia inatamani au mfumo wa familia utakulazimisha tu kujitoa kutafuta maisha bila kujalisha ni Jinsia gani.

Nasisitiza tena,kwamba ajira Zanzibar zipo,tusiishie kulalamika na kuchagua kazi kisa Imani zetu.
Sasa hata ije Serikali yoyote haiwezi kuwa na vyanzo mbadala zaidi ya Sekta ya Utalii.
 
Ustaadh inaelekea wewe ni mtoto wa wale wanaochaguliwa Dodoma, unahisi kijana wa Zanzibar anaweza kuomba kazi gani hapo Zanzibar ? kuna kiwanda gani hapo ? kwenye mahoteli watawala wame import wakenya nyie mmeachiwa uchangudoa kama hudma kwa watalii. Nchi yako ina import mpaka nyanya na vitunguu wewe unatetea uongozi. Kweli Zanzibar hamuwezi kuzalisha vitunguu kweli ?
Nimekaa Zanzibar na ni kweli watu hula mara moja tu saa tisa mchana, kuna nyie wachache ambao mnamudu hata kwenda forodhani kula mishkaki lkn sio wengi+

Wakenya wamajiriwa kwa Vyeti vyao na uwezo wao wa kazi.

Wewe jiulize mwenye kwanza unaishi maisha yepi,maaana Zanzibar kuna kizazi cha walalamika tuuu na wale wanaojitambua.

Yaani unadanganya UMMA kwamba Zanzibar hakuna viwanda?
We mtu wa wapi unaishi kwa kukaririshwa na viongozi wako,jitambue acha kuburuzwa kama jiwe.

Zanzibar ku import mazao,hili suala la ku import sio geni,hata ukienda UK unakuta ndizi za Brazil na nchi nyingine zipo pale,maana hawazalishi.Hilo Jiji La Dar wao wenyewe hawazalishi lakini utakuta mazo mengi yanaletwa hapo kuliko sehem yoyote Africa Mashariki.
Zanzibar ni kisiwa na uoto wake unategemea mazao maalum,na ndio maana kisiwa cha pemba kina uoto mzuri na kinazalisha mazao yanayokubali ikiwemo Ndizi,na hata mahindi pia.

Unguja mabayo huiita kwa ujumla kama Zanzibar mikoa ya kati na ukanda wa Magharibi ni maeneo yenye rutba nzuri na ardhi nzuri.Ikifuatiwa na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa kusini.Wakati huo Mikoa ya Mashariki mingi ni kame sana kulingana na ardhi yake kuwa Jiwe jingi na kame sana.

Sasa lazima uijue nchi yako kabla ya kulalamika.Viwanda Zanzibar vipo na kilimo kinafanyika.
Sasa suala la nani alime hilo sio Serikali,ni wewe kijana ujitambue.Na mashamba karibia yote vijana hakuna aneenda kulima.Wengi huwaachia Baba zao ndio walime wao wakiona mazao ndio wakavune tuu,na kuna kipindi hata kwendakuvuna hadi agombane na mzee wake ndio akubali kwenda.

Utejaa na uvutaji wa madawa ya kulevya sio kigezo cha kukosa shughuli ya kufanya.Ni Malezi na uvivu wa kufikiria
 
Please 'WE can add more supply, my wish to destroy the area completely! with people at large island
 
Zanzibar spices naona mpaka povu limekutoka. Mwezi ujao uje Dodoma huenda ukateuliwa kuwa kiongozi wa mkoa mmoja huko Pemba.

Karibu Dodoma
 
Zanzibar spices naona mpaka povu limekutoka. Mwezi ujao uje Dodoma huenda ukateuliwa kuwa kiongozi wa mkoa mmoja huko Pemba.

Karibu Dodoma
Kaka lazima tuwe wakweli,huku kwetu watu hatujitambui,sio kulaumu viongozi na kulumu watu wa Bara.

We tembelea nyumba ambazo kuna vijana wawili tu wakizanzibar wanafanyakazi hotel halafu uone kama wanalalamika kama wewe.Ni kwamba wanajituma na pesa yao inaingia kwenye mzunguuko wa familia.Sasa je kama vijana wengie tungechangamkia nafasi kwenye sekta ya utalii hali ingekuwaje.Si maisha yangekuwa bomba tu.
Ila kila unaemuuliza anataka kazi ya kuzunguuka na kiti.Bakhresa kafungua kiwanda cha Maziwa watu wanakimbia kwenda.Sasa wewe shule yenyewe kama mie unataka mshahara mkubwa.Sasa si ndio maana watu wanachukua wafanyakazi kutoka Bara.
 
Back
Top Bottom