Iandaliwe listi ya Watumishi na Wakandarasi wa kuwatumbua na kuwakaripia jukwaani ili kasi ya awamu ya tano ionekane haijapoa

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
11,996
20,647
Nashauri iandaliwe listi ya watumishi, hasa wa umma wakurugenzi wa halmashauri, ziara zipangwe, na muhusika abanwe kuelezea mambo mbalimbali, tunajua wana mambo mengi hawawezi kuyakariri yote, lakini walazimishwe kuyajibu mbele ya hadhara.

Wakionekana kujaribu kufanikiwa kuyajibu tusiwaruhusu, tupandilie swali jingine mpaka washindwe kujibu.

Akijibu la barabara, liulizwe swali Panadol ngapi zimeletwa kwenye vituo vya afya, ataje mabox, akiweza tusikubali ataje idadi ya vidonge akiweza tusikubali, aseme vingapi vimetumika, vingapi vipo, kwenye kituo kipi cha afya.

Lengo letu wananchi wafurahi, na waone watu tuliowaleta wawaongoze wanavyodhalilishwa na sisi.

Tunajua kwamba hatujapeleka hela kwa shughuli mbalimbali za maendeleo, na makusanyo sio mazuri lakini tuwalazimishe wasome bajeti iliyopangwa, wakijaribu kusema pesa iliyopelekwa, tuwakatishe katishe.

Hii itasaidia wananchi kutojua kama tulipeleka fedha kwa shughuli husika ama laa, tutamwachia mzigo wa lawama halafu chama kitaonekana kilitenda kwa kupeleka pesa ila watendaji ndio wa hovyo, japo tunajua sisi kama chama hatujawapa hata mia.

Hii iendelee kwa makandarasi, tunajua hatujawalipa, lakini iwe marufuku kusema hivyo jukwaani na tusiwape nafasi ya kuelezea kwa nini mradi umekwama, watatoboa siri, mkakati uleule, akitaka kuongea tumkatishe, tufoke sana kwamba hela ipo kwa nini hajengi.

Baadae wananchi watashangilia, watatupa kura, sisi tutaendelea kula wakati wananchi wakiendelea na sala ya kuombea chakula tunachokula ili kisitupalie.
 
Back
Top Bottom