I think tutoe kwenda jeshini

Rebeca 83

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2016
Posts
15,669
Reaction score
33,691
Hello JF,

Leo nilikua na wazo kwa nini tusitoe mfumo wa kwenda jeshini?

Tusave hela inayotumika jeshini kuwapa waajiri wa makampuni mbali mbali waemploy watu wanaotoka vyuoni, ili wapate experience kabla ya kupata kazi rasmi...

Haina mantiki kupoteza muda kushika mambunduki , wakati umetokea kwenye marketing background!

Sijui km lishawahi kufanyika hili duniani, km bado tunaweza kuanza nalo,,,,

What do you all think?

Becky
 
Wanatumia kigezo cha 'uzalendo' kwenda jeshini lakini sio sahihi kabisa.
Ukiangalia mafisadi wengi walioitafuna nchi walipitia haya mafunzo ya JKT tena kwenye kipindi cha Uongozi wa mwalimu.

Mafunzo haya na Mwenge ni matumizi mabaya ya rasilimali

Naunga mkono hoja kwa wazo mbadala ulilotoa.
 
Kuna kipindi cha tangu rais Ali Mwinyi, waliacha kupeleka watu jeshini, imerudiwa tena kwenye awamu hii.
Kwa jinsi wanasiasa wa Tz walivyo, ni vigumu kuwapa pesa sekta binafsi kufanya kitu kama hicho (apprenticeship). Hiyo no moja.
Pili, sina uhakika kama hiyo sekta binafsi yenyewe wana ujuzi (skills) na pia nafasi/ utayari wa kuwachukua hawa vijana.
Report za UNESCO zinadai wahitimu wetu wako chini ya viwango, sijui huko sekta binafsi kama wana waliofuzu katika viwango vinavyotakiwa.
 

Umeeleweka mkuu,kama ilivyopitishwe kuwe na jeshi,walitoe,na hela ambayo ilikua ina fund jeshi, ndio itumike kuwapa waajiri ili watu wapate employment skills,nitashangaa sana kama hao wanasiasa watapitisha jeshi,halafu wazo la kuwapa wahitimu skills walipinge!...

Uko right,hoja yako ya pili,kuna uwezekano watu wasipate right skills,kutokana na waajiri wenyewe kuwa makanjanja but I think huwezi kukuta katika kampuni nzima wote wewe makanjanja lol(mwenyewe atachanganya na zake,lol, kwa kweli hili, sijui tutalizuiaje?)

Tatu, graduates wetu wako below standards first tunahitaji mabadiliko km ni English then tutumie English throughout,km ni kiswahili throughout kindergarten,primary and secondary and university kote tuweke lugha moja,sio primary ambako ndio foundation tunasoma kwa Kiswahili kwa masomo machache,then secondary masomo meeeengi halafu kwa lugha ya kiingereza,hapa unamvmchanganya mtoto anakuwa forced ku cramm,sasa mtu aliyevuka kwenda chuo kwa kucramm,unategemea huyu mtu akifika chuo atumie njia nyingine ya kujifunza zaidi ya kucramm??tunatoa graduates wana ma theories kichwani, wakati practical/real life situation anachemka...

Mie nataka hii programme ya kuondoa jeshi badala yake wahitimu wapewe skills at least for one year or two, Iwe part of learning package,na nadhani tukitilia mkazo elimu yetu ibadilishwe,wanafunzi wewe encouraged to do independent learning,pamoja na hii program ya kupata skills tutakuwa better equipped kushindana kwenye soko la wahitimu duniani...
 
Jeshi, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ni wastage of taxpayers money.
 
Serikali inaweza kuwafanya sekta binafsi kufanya hili kwa kutoa punguzo la kodi kwa kampuni itakayofanya hivyo badala ya kupeleke pesa sekta binafsi.

Ungefanya vyema ku-share ripoti hiyo ya UNESCO mkuu
 
Serikali inaweza kuwafanya sekta binafsi kufanya hili kwa kutoa punguzo la kodi kwa kampuni itakayofanya hivyo badala ya kupeleke pesa sekta binafsi.

Ungefanya vyema ku-share ripoti hiyo ya UNESCO mkuu
Kodi ya Tz inapaswa kupitiiwa na kuwekwa wazi, ilivyo sasa unahisi kuibiwa, sasa hata hilo punguzo inawezekana lisieleweke na kuwakatisha tamaa wenye nia.
Nilisikia mwakilishi wa UNESCO akiripotiwa juu ya hayo, sikuiona ripoti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…