Siku ya ndoa yao.
Mwanamke mmoja (Adriana Ford-Thompson) ambaye ni graduate wa Chuo Kikuu cha Cambridge na lecturer katika Chuo Kikuu cha York nchini Uingereza amemtetea mumewe mbakaji kwa kumwambia kuwa "I still love you" pamoja na mume huyo kudai kuwa alibaka kwa sababu alikuwa hapati mgegedo ya kutosha kutoka kwa mkewe.
Mark Thompson (37), ambaye ni mtoto wa mchungaji wa kanisa, amehukumiwa kifungo cha miaka 11 jela kwa makosa ya kumteka na kumbaka mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu na kufanya shambulio la aibu dhidi ya wanawame wengine watatu. Wakati anambaka mawanafunzi huyo, Mark Thompson alimwambia "sipati mgegedo kutoka kwa mke wangu, kwa hiyo nautafuta kwingine". Mwanafunzi huyo (21) anasoma kwenye chuo hicho hicho anapofundisha mke wa mbakaji. Hata hivyo, haujulikana kama denti huyo alikuwa mmoja wa wanafunzi wake.
Katika hukumu yake, judge amesema kuwa Mark Thompson ni mwanaume hatari sana kwa wanawake. Hata hivyo, mkewe amemtetea mumewe kwa kudai kuwa ni mwanaume ambaye ni "kind, sensitive and gentle". Akiwa mahakamani hapo, lecturer huyo alisendelea kumwambia mumewe mbakaji kuwa "I love you" and "stay strong".
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Mark Thompson alimteka mwanafunzi huyo mida ya saa kumi za asubuhi wakati (mwanafunzi huyo) akirudi nyumbani kutokea club. Alimkamata na kusukumizia ndani ya van yake na kumbaka mara tatu na kisha kuzunguka nae mjini. Mwanafunzi huyo, anayesomea shahada ya kwanza, alidai mahakamani hapo kuwa wakati anambaka, Mark Thompson alimwambia kuwa "I don't get sex from my wife, so I go to get it elsewhere".
Lakini lecturer huyo aliendelea kumtetea mumewe akidai kuwa amemfahamu kwa miaka 10, ni rafiki yake wa karibu na kuwa ataendelea kusimama naye kwa lolote lile. Aliongeza kwa kusema "Mark and I will face this challenge ahead together with courage, love and patience."
Wapendwa hao walikutana mwaka 2006 nchini Tanzania. Mark alihamia London kutokea Jamaica akiwa na umri wa miaka 16 na kuanza kujifunza boxing. Mwaka 2005 alikuja Tanzania kufundisha marital arts. Akiwa Tanzania alikutana na mke wake ambaye alikuwa akifanya utafiti wa misutu kama sehemu ya masomo yake ya Ph.D. Mwaka 2007 walirudi wote Uingereza na wakawa wanaishi wote wakati mkewe akiwa anamalizia Ph.D yake. Walioana mwaka 2009.
Hapo akiwa Chuo Kikuu cha York with her "gentle, kind and sensitive" man.
"I still love you"
Beach holiday.