I see the future and how it comes

I see the future and how it comes

KAUMZA

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2010
Posts
699
Reaction score
241
Huu ni uchambuzi wangu wa muelekeo wa kisiasa nchini katika kipindi hiki tukielekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na uchaguzi wa mitaa na vijiji mwaka 2014.

Pamoja na ukweli kuwa serikali ya CCM chini ya JK imetekeleza kwa kiwango kikubwa miradi mingi ya maendeleo tena kwa kiwango kikubwa mfano Chuo Kikuu cha Dodoma, Shule za seekondari karibu kila kata, barabara nyingi za lami na utoaji wa ruzuku kwa pembejeo za kilimo kwa wakulima wadogo wadogo, Kwa jinsi upepo wa kisiasa unavyovuma kwa sasa, Chama cha Mapinduzi kipo katika wakati mgumu sana kisiasa na kuna uwezekano mkubwa wa kupoteza kwa asilimia kubwa serikali za vijiji/mitaa. Na hiyo itakuwa ni ishara ya wazi kabisa kuwa Uchaguzi utakaofuata yaani uchaguzi mkuu 2015 CCM kuna uwezekano mkubwa kabisa wa kupoteza majimbo mengi na pia kata nyingi.

Kuna sababu lukuki za Chama Cha Mapinduzi kushindwa katika Chaguzi zijazo. Miongoni mwa sababu hizo ni:

(i) Upinzani nje ya CCM umekuwa ukipata nguvu kila kukicha. Wananchi wengi wameonesha kuchoshwa na
Chama kinachotawala sasa na kuvutiwa na hoja za wapinzani. Hoja zitolewazo na wapinzani wa CCM mfano
hoja za akina James Mbatia, Zitto Kabwe, John Mnyika etal zimekuwa zikikonga mioyo ya wananchi wa
kada zote wawe ni wakulima, wafanyakazi wa serikali wa kada za chini na kada za kati, wasomi na hata
wafanyabiashara wa kati. Na kama ilivyo kawaida (political culture), wafanyakazi na wasomi huwa
determinants wa nani mshindi

(ii) Migogoro isiyokwisha ndani ya CCM. Chama Cha Mapinduzi kimekuwa kikisakamwa na migogoro isiyokwisha
miongoni mwa makada wake. CCM ya sasa si moja na kuna uwezekano wa kuingia katika uchaguzi mkuu ujao
ikiwa vipande vipande. Mfano ni kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na mwenezi wa CCM- NAPE NAUYE ambaye
hivi karibuni alinukuliwa akisema ikulu si mahali kwa wagonjwa wanaotafuta urais makanisani. Hapa alikuwa
akimsigina hasimu wa kundi lake kisiasa Edward Lowassa ambaye anasemwa kuwa ni mgonjwa na ndiye
amekuwa akifanya harambee makanisani, ingawa hajawahi kuzungumzia siasa za kuelekea 2015 katika
nyumba hizo za ibada.

(iii) CCM kwa sasa imekosa nguvu ya kihimaya (Stronghold). Kwa miaka mingi CCM ilikuwa imejikita katika vijiji
na baadhi ya miji. Lakini kwa sasa CCM imefukuzwa takribani katika miji na majiji yote makubwa hapa nchini.
Na kwa sasa hata vijijini CCM imeanza kupoteza nguvu zake za asili. Katika chaguzi ndogo ambazo zimekuwa
zikifanyika, CCM imekuwa ikiingia kwa machale kwa kuwa huwa haina uhakika wa ushindi wa mteremko.

(iv) Mbegu ya udini ambayo kwa sasa imeanza kumea, inaweza kuwa msumari katika jeneza la CCM. Ingawa
inaonekana kutulia, vuguvugu la udini bado lipo na linazidi kushika kasi. Kauli ambazo zimekuwa zikitolewa
na viongozi wa CCM kuwa CHADEMA ni chama cha wakristo, zimekuwa zikiwapa nguvu zaidi Chadema.
Wakristo wengi wamekuwa wakiiunga mkono Chadema na huku Waislam wamegawanyika baadhi wakiiunga
mkono CCM na wengine CUF. Na ikumbukwe kuwa waislamu katika uchaguzi uliopita si kwamba waliiunga
mkono CCM, bali walimuunga mkono Kikwete kama muislamu mwenzao. Iwapo udini huu tutafika nao hadi
mwaka 2015 ni wazi kuwa utakuwa ni advantage kwa Chadema na hasara kubwa kwa CCM. Kwa nini
nimesema hivyo kuhusu udini..!! NITAFAFANUA


  • Tabia za waumini wa dini hizi kubwa kabisa hapa nchini ni tofauti sana. wakati wakristo ni watiifu sana kwa viongozi wao wa kiroho, wenzao waislamu wana utiifu kidogo sana kwa viongozi wao.
  • Wakati wakristo wana umoja wa hali ya juu, waislamu wamegawanyika katika makundi hivyo kukosa kauli ya pamoja. Msimamo wa Bakwata siku zote umekuwa tofauti na msimamo wa Taasisi nyingine za kiislamu.

(v) Ugumu wanaoupata CCM katika chaguzi mbalimbali za mabaraza ya madiwani ni ishara tosha kuwa CCM ipo
taabani. Mfano chaguzi za hivi karibuni za Halmashauri ya Uvinza, Kibondo na Buhigwe mkoani Kigoma
ambako CCM imeponea chupuchupu hadi kupelekeakuahirishwa kwa chaguzi hizo

(vi) Kwa upande wa visiwani, kilichotokea Zimbabwe Mugabe wa ZANU-PF Vs Tsivangirai wa MDC kinaweza
kutokea pia visiwani. Ndoa kati ya CCM na CUF kwa kiasi kikubwa inaweza kuwagharimu CUF na kuwa
advantage kwa CCM.
 
Uchambuzi mzuri na umekwenda shule. wachambuzi kama hawa ndo wanahitajika katka zama zetu hizi. ni vigumu kujua imani na itikadi ya mchambuzi. ni ccm au chadema ni muislamu au mkristo. nimependa
 
Back
Top Bottom