Haya jamani, nashukuru sana kwa mawazo yenu kufuatia mchango wangu kwenye mada hii. Kwanza mtoa mada naomba usinielewe vibaya kwa nilichochangia, maana nilichoandika nakielewa! na naendelea kukisapoti ingawa "the boss"aliona nimekurupuka, na wengineo. Lakini Noname ni hivi......
KAMA WEWE UMEONA HIVYO NA UMEAMUA KUWAPA HONGERA SAWA MIMI SIPINGI, na huenda mumeo ama BF wako yuko hivyo pengine, lakini mimi nilifikiria kwa uelewa wangu wa maisha na ndoa nyingi zenye matatizo nilizozishuhudia, ndio maana nikatoa mawazo kuwa kama kwa upande wako kuzuri kwa jinsi ulivyochambua basi hongera sana.
Lakini sio kwa wote, jamani kila kitu kina negative na positive zake, mimi nafahamu kuwa wapo wanawake wanaolia kila kukicha kutokana na visa na mikasa ya waume, au wanaume zao! Alafu kuna watu waliuliza mimi mke ama mume mimi sydney ni mke!
Asanteni. Again;;;; huu ni mtizamo tu jamani, haina haja ya kuwa na jazba kama za the boss! looh!