Bwn mdogo, hiyo sentensi juu imenichanganya sana. Kwamba huyo binti ulimtokea miaka sita iliyopita na mwaka juzi ndo amemaliza form four. Maana yake kwa lugha rahisi, ulimtokea akiwa form one au form two, kweli mlikuwa watoto sana na bado ni watoto hata leo!
Majibu anayokupa huyo binti, yanaonyesha dalili za nataka sitaki, kwa watu wazima tumeshamuelewa! Ila kwa kutambua kuwa alimaliza form four mwaka juzi (na mwaka huu ndo kwanza Jan), nakushauri, muendelee kufocus kwenye masomo yenu ya elimu ya juu kuliko mliyonayo sasa maana mnaweza kujikuta mnapotezeana muda na kupoteza fursa za kujiendeleza kielimu ambazo ndo msingi wa maisha yenu yajayo.