I need a wife not a girlfriend.

I need a wife not a girlfriend.

Bobsinbady

Member
Joined
Oct 30, 2012
Posts
13
Reaction score
5
Nilipokuwa kidato cha pili nilimpa binti ujauzito tukapata mtoto wa kiume ambaye sasa yupo Sec.Hatukuweza kuendelea na mahusiano kwa sababu mbalimbali.Yule binti aliolewa na kupata mtoto mwingine na anaendelea na maisha.

Badadae nikawa na mahusiano na binti mwingine tukiwa kidato cha tatu hadi tulipomaliza na kuendelea elimu ya juu.Mahusiano yetu yaliingia mushkeri baada ya kugundulika ni ndugu wa familia upande wa Mama,hivyo tusingeweza kuendelea na mahusiano hayo.

Baada ya mwaka mmoja nikawa na mahusiano na binti mwingine ambaye alikuwa anasoma chuo fulani IRINGA tulipendana sana.Hata familia zetu ziliafiki mahusiano yetu.Nilijitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu kutiza wajibu wangu kama mwanaume na kama mwenza wangu mtarajiwa.Hakuna jambo nilifanya pasipo yeye kujua au kumshirikisha.Ilibidi nichelewe kufanya mambo yangu mengine ili yeye kwanza amalize chuo.Nilipata habari zake nyingi ambazo hazikunipendeza lakini nilipuuza na kumsihi mwenzangu kuwa mwangalifu ili penzi letu lisije ingia taflani.Akiwa mwaka wa tatu,uvumilivu ulinishinda hasa pale aliponidanganya kuwa yupo nyumbani na asingeweza kutoka kwa kuwa wazazi wake wapo na kuna mahali wataenda kama familia.Na kweli usiku mida ya saa tatu alinipigia na kunialifu kuwa amerejea yupo nyumbani na muda huo anajiandaa kulala.Ilipofika saa nane usiku nilipigiwa simu na rafiki yangu kwa kuwa alimuona girlfriend wangu ilhali mimi anioni.Nilimjibu kuwa nilimruhusu aende kukutana na rafiki zake.Niliamka nikaenda hadi MZALENDO ambapo ndo walipokuwa kweli nikamuona yupo na rafiki zake pamoja na kijana ambaye nilishapata habari zake hapo awali na akamkana.Nilimpigia simu,nikiwa namuangalia kutoka kwenye parking akawaonyesha rafiki zake kisha hakupokea.Nilipopiga mara ya pili akanyanyuka na kwenda maeneo ya maduka ndani (kwa wanaopajua MZALENDO) akaanza kuongea kwa sauti ya usingizi kama vile amelala kweli.Akaniambia nimemkatisha usingizi wake.Nilimtuma paparazi mmoja akampiga picha pale alipo na badae akawapiga akiwa na rafiki zake kisha nikaondoka kwenda kujiandaa kwenda kazini.Alikuja jioni akiea tayari amejiandaa kwenda chuo,hivyo alikuwa amekuja kuchukua pesa kwa ajili pocket money.Kweli nilikuwa na hasira sana,ila niliomba nguvu ya ziada ya Mungu nisije kufanya kitu cha ajabu.Siku hiyo nilikunywa pombe sana kama kujiliwaza na nilataka kumwambia usiku huo kwamba mimi nayeye basi.Ila nikahisi ataona kuwa ni pombe,tukalala hadi asubuhi.Nilipoamka asubuhi alikuwa tayari ameamka kaandaa chai.Nikamuita,ndipo nikamuonyesha zile picha.Alifadhaika sana na hakuwa na la kusema.Huo ukawa ndio mwisho wetu.

Nilijiapia kuwa sitopenda tena.Ila nadhani sikuwa sahihi kwani kama binadamu na rijali nilishindwa.Baada ya muda nikaanzisha mahusiano mengine na binti wa kabila yangu.Huyo ikawa yeye anawivu wa kupindukia,hakutaka hata kumuona mdogo wangu wa kike akiwa karibu yangu.Alidiriki hata kuwapigia rafiki zangu wa kike walio kwenye simu yangu na kuwatusi sana.Aliponikuta sehemu nimekaa na rafiki zangu kama ingetokea kuna mwanke yeyote,basi yeye akifika bila kuuliza,ataanza kumshambulia huyo dada bila kujali wale niliokaa nao ni akina nani.Kwa kweli nidhamu ilikuwa hakuna kabisa.Tulidumu kwa miezi minne tu,lakini timbwili lake utadhani tumeka miaka minne.Tulikubalina tuachane kwani sikuwa tayari kuendelea kudhalilika.

Baadae nikawa na mahusiano mengine na binti mmoja ambaye tulikutana kwenye harusi ya ndugu yangu.Yeye alikuwa akiishi Uganda kwa wakati huo.Mahusiano yetu yaliendelea vizuri sana.Wakati fulani alikuja DAR nami nikaomba likizo kazini.Tulienda Bagamoyo na ZNZ.Badae tulienda kwao kijijini ambapo alinitambulisha kwa jamaa zake (Mama,mama wadogo,binamu zake n.k).Tukiwa ktk maongezi ya kujuana.Tukajikuta sisi ni ndugu kwa baba zetu...Tulijaribu kuwa shawishi tufanye mambo ya kimila ili tuweze kuwa wote,ila Mjomba wake na binti alikataa katakata.Ikabidi tukubaliane na mwenzangu kusitisha mahusiano yetu japo mwanzo ilikuwa ngumu ila badae tulikubali matokeo na kila mtu akaendelea na ishu zake.Hii ilikuwa ni miaka miwili iliyopita.

Mwanzoni mwa mwaka huu,nilianza mahusiano mengine.Ila ya sasa ndo kiboko.Kwani tangu nimeanza mahusiano haya sijawahi hata mara moja kukaa na mwenzangu kujadili juu ya mahusiano yetu na mustakabali wake.Mara zote anasababu za kufanya tusikutane.Nashindwa kuelewa kama kweli ana nia ya kufanya mahusiano yetu yakue.Sasa nimekata tamaa ya kuwa na yeye na nadhani sihitaji tena kuwa nae.
Sasa muda umefika wa kukata shauri na kuwa na mahusiano na mtu sahihi kwa wakati sahihi.Sihitaji rafiki wa kike ila nahitaji mmke.Najua kuna wana JF waliopitia makubwa zaidi ya haya pia wako tayari kwa kufanya maamuzi yaliyo sahihi kwa wakati sahihi.
Napenda M/ke mwenye umri wa kuanzia 25 - 30.Awe na elimu ya wastani.Awe mweusi wa asili pasi kutumia vipodozi vikali.Awe mrefu wa wastani na pia asiwe mnene sana.Awe mwenye msimamo na mwenye mchango wa mawazo kwenye mambo ya msingi.
GOD BLESS YOU ALL.
 
duh umekumbana na mikasa ya mapenzi!!!!!!!!!!!!!!!
mi nakutakia kila la kheri lakin inabidi uwe makini
sana don't fall in love cos of pressure just let the
your heart fall in love when ur ready and not because your lonely
 
Back
Top Bottom