I can see future so bright if we change our minds

I can see future so bright if we change our minds

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Posts
608
Reaction score
1,658
Kwa mzalendo yeyote yule hamu yake kubwa ni kuona Taifa lake likipiga hatua. Mabadiliko haya sio mabadiliko ya mali tu bali total transformation of human being.

Binadamu akibadilika kiakili na kiroho.

Ukiniuliza mimi mabadiliko haya mawili yaani ya kiakili na kiroho ni muhimu zaidi ya material transformation.

Kwasababu mabadiliko ya kiakili na kiroho ndio yanayopelekea mabadiliko mengine.

Kama binadamu wote tungekuwa na hekima na maarifa ya kutosha matatizo mengi ambayo tunakabiliana nayo katika dunia hii tusingekuwa nayo.


Mabadiliko ya binadamu ya kiakili ni muhimu. Kama Taifa hili lingekuwa na viongozi mature enough kukaa pamoja na kuamua baadae ya Taifa hili tungekuwa tumeendelea zaidi.

Tatizo tunafikiria maendeleo ya ki mali zaidi kuliko maendeleo ya kiakili ya watu wetu ambayo ingesaidia ku transform jamii yetu.

Ni muhimu sana kuangalia upya jambo hili. Elimu yetu hatotusaidia chochote kama haitazalisha watu wenye fikra sahihi na wazalendo.

Dhumuni la Taifa hili kuwasomesha watu wake ni maendeleo ya Taifa hili. Tujiulize watu wetu wanatumia akili zao ipasavyo kwa maendeleo ya Taifa hili?

Tusijidanganye wale wenye hekima na akili ndio wenye kuendelea na walio wapumbavu lazima watabaki nyuma. Watu wetu hawafikirii hata wale miongoni mwao wanajiita wasomi.


We can only measure your education by positive impact you brings in society.


Hili Taifa linahitaji watu watakao badilisha maisha ya watu wengine. Tunahitaji watu wetu wabadilishe mitazamo yao kuhusu Taifa hili, tuje kwa pamoja na tulijenge Taifa letu. Nina uhakika kama tutazikusanya akili zetu kwa pamoja na kufikiri juu ya ujenzi wa Taifa hili tutafika sehemu fulani.

Jambo la muhimu sana ni fikra za watu wetu ni jinsi gani tutazibadilisha na kuleta uzalendo na wajibu kwa Taifa hili. Jinsi gani tutawafanya watu wetu walipende Taifa hili na kuleta matumaini kwa watu wote. Kuwafanya watu wetu wote watambue wana share katika Taifa hili na wajibu wa kulijenga. Ni muhimu kuangalia fikra za watu wetu wote. Kama tutakuwa na watu wenye hekima na maarifa watafanya maamuzi ya busara ambayo yataleta positive impact katika jamii yetu. Adui mkubwa wa binadamu ni ignorance ni muhimu sana kupambana nae. Ni hatari kuliko kitu chochote ni afadhali uishi kwenye nyumba ya matope lakini uwe na akili.

Maono yetu lazima iwe ni jinsi gani tutalijenga Taifa hili sio ubinafsi ambao hautasaidia Taifa hili. Ni lazima tutambue tuna kitu cha kujenga kwa faida ya wote. Lazima tutambue tuna wajibu binafsi lakini kuna wajibu kwa jamii na kwa Taifa. Ndugu zangu mataifa hujengwa kwa conscious effort hayakui kama uyoga au kujengwa kwa mazoea. Mataifa yanajengwa na watu wanaofikiri na wenye busara.


Ili tujenge Taifa hili lazima tujenge upya mahusiano yetu na uaminifu miongoni mwetu. Tuna Taifa ambalo limegawanyika vipande vipande na lisilo kuwa na discipline. Huu ni ukweli na hatuwezi kukataa ukweli huu. Ni lazima tulete upya ORDER katika Taifa hili kama tunataka kuendelea. Tutengeneze vijana wenye maarifa na uelewa. Ni lazima tujenge Taifa la watu wenye kufikiri kama tunataka kutoka hapa tulipo. Ni lazima tujenge Taifa la watu wanaowajibika kwa familia na kwa Taifa. Ni lazima tujenge Taifa la watu wanao value familia na kulea watoto katika misingi ya maadili imara.

Vitu vinavyoendelea katika Taifa hili haviwezi kulifanya Taifa hili li move forward. Ubinafsi hauwezi kufanya Taifa hili lisonge mbele. Umoja katika wajibu utafanya Taifa hili lisonge mbele. Furaha yetu kama taifa itatokana tu na mafanikio ya pamoja kama nchi. Umoja wetu tu ndio utaleta furaha ya pamoja. Katika Taifa hili ni muhimu tukaheshimiana. Tunahitaji maridhiano ya kitaifa. Ni muhimu kuleta akili zetu pamoja katika ujenzi wa Taifa hili.

Sijawahi kumuona mpumbavu mkubwa kama mtu anayeliibia Taifa lake mwenyewe. Maendeleo ya mtu hayatokani na wizi that is self deception. Maendeleo ya kweli yanatokana na bidii na maarifa yake. Huwezi kujipongeza kwa mali inayotokana na wizi. Bali mtu anayefanya kazi kwa bidii kupata anachotaka ana cha kujipongeza na kujisifu. Ana kila namna ya kufurahia maendeleo yake. Mtu mwizi ni mtu aliyeshindwa kutumia akili zake na nguvu zake kuleta mabadiliko binafsi. Ni mtu asiye na thamani.

Kwahiyo wajibu wa kwanza kwetu ni kubadilisha fikra za watu wetu. Ni hatua ya kwanza na muhimu kwa Taifa hili kusonga mbele. Ubora wa Taifa lolote lile duniani unatokana na ubora wa mawazo ya watu wao. Kama sisi ni maskini mawazo yetu sio bora sana hivyo inatubidi tutie juhudi.


Ni muhimu kutambua maendeleo yetu kama watanzania ni jukumu letu wenyewe sio jukumu la Taifa lolote lile. Ni juhudi zetu ambazo zitatukomboa. Sio juhudi za wawekezaji wala Taifa lolote la kigeni. Kwahiyo ni lazima tuamke sasa. Tumaini langu ni kwamba kizazi hiki kitaibua viongozi ambao wataleta imani ya wananchi kwa Taifa lao na kwa viongozi wao.

Kwamba kitaibua changamoto mashuleni, kutia juhudi katika kutafuta maarifa na uelewa ili kwa pamoja tujenge Taifa hili. Ni muhimu kutambua heshima ya Taifa hili ni muhimu kuliko kitu kingine chochote. Ni lazima tujenge heshima hiyo miongoni mwa mataifa. Ndugu zangu ni lazima tufikirie kuhusu mambo haya ninayoandika ni muhimu kwa mustakabali wetu.


Nitasema na nitaendelea kusema Taifa hili linauwezo wa kuwa Taifa kubwa kama Taifa lolote lile i can see possibility it is clear in my mind without any doubt. All we need to do is to change. To change our thinking. Tuwe wamoja na wenye kushirikiana. Tuweke mbele Taifa letu na kulipenda. I can see the future is so bright. I can see in my imagination cheering the unity of the Nation, progress and good fortune. God bless Tanzania.
 
I will be glad to answer any question.
 
Great thoughts are sweet and loving like honey. Great thoughts impress the spirit of men an women. great thoughts sways and move the spirit of the people. Great thoughts change minds of the people.
 
Thanks. well said. but one thing, who can cause the changing of our mindsets and attitude? my common sense tells me that this can be through informal and formal education. the worst thing with education, especially formal one, it's highy corrupted, starting from kindergaten to higher education. my view is that in our current setting of mediocracy, evolutional pace to bring about change will take generations even centuries. revolutional approach could be the best thing. here one question remains: are we ready to take the plunge? do we have thinkers who will craft and oversee the mission with very minimum sacrifice? it is about me and you and them. let's keep thinking, not dreaming. thanks.
 
Asante Mkuu wangu Shayu:
Leo Jf imenionesha tumaini jipya na bora kabisa!
Nitarudi. Ila niseme hili tu kwako Mkuu Shayu...."Kichwa chako kimebeba Johari kuu na ya thamani kubwa kabisa" usiiache ipotee, ipiganie hata kwa tone lako la mwisho la damu!
Nimeipenda sana kauli hii "I can see possibility it is clear in my mind with no any doubt" AMINA.
Ubunifu haujawahi kufika mwisho, nguvu yetu ni UMOJA na KUTHUBUTU, TUNAWEZA.
Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani.
Anaita sasa!
 
Wana JF , tunaweza kuwekeza katika fikra mpya za kuibua taifa la wa tu wanaofikiri, na kutumia falsafa ya mawazo chanya kuleta maba dilko , big up mkuu shayu.
 
Thanks. well said. but one thing, who can cause the changing of our mindsets and attitude? my common sense tells me that this can be through informal and formal education. the worst thing with education, especially formal one, it's highy corrupted, starting from kindergaten to higher education. my view is that in our current setting of mediocracy, evolutional pace to bring about change will take generations even centuries. revolutional approach could be the best thing. here one question remains: are we ready to take the plunge? do we have thinkers who will craft and oversee the mission with very minimum sacrifice? it is about me and you and them. let's keep thinking, not dreaming. thanks.

Najua tatizo la elimu ni muhimu sana na bila ya hilo ukombozi wa kweli hautawezekana. Jambo tulilo nalo kwa sasa ni tatizo la leadership na mengine hayo yote yatarekebishika tukiwa na uongozi mzuri. Tukiwa na uogozi mzuri tutaweza kuweka dira yetu na kuifuata.

Tunaweka mipango lakini hatuiamini hiyo mipango wala hatuna courage ya kuifuatilia na kuhakikisha kile ambacho tume plan kinatokea tena kwa ufanisi mkubwa.

Tunaweza ku mobilize watu wetu na ku induce national purpose ndani yao. Watu lazima wajue malengo ya taifa lao na mwelekeo wao kama Taifa. Kama tuta organize watu wetu hakuna tutakachoshindwa.

Lakini pia National consciousness ni muhimu. Fikra zetu ni lazima tuzihamishe tufahamu tuna kitu cha kukijenga kwa pamoja. Uhusiano kati ya wajibu binafsi kwa jamii na kwa Taifa lazima uwe defined and harmonized. Wajibu na haki lazima uwekewe mstari. binadamu ana haki ya kuangalia familia yake as well as Taifa lake. Uhusiano kati ya mtu na Taifa lake ni muhimu. Hapa tunaona elimu finyu ya uraia. Elimu inayoenezwa ya uraia ni ile ya kupiga kura na sio itakayo jenga uzalendo kwa watu wetu.

Elimu yetu imekuwa ya kibinafsi zaidi ya kuwa planned kwa malengo ya ujenzi wa Taifa. Ni lazima tuwasomeshe watu kulingana na aina ya Taifa tunalotaka kulijenga. Tukisomesha watu kwa malengo ya kibinafsi kusudi mtu apate ajira tutakuwa tumekosea. Ni lazima tu shape upya thinking za watu wetu katika uzalendo na wajibu. Mtu atapewa mshahara sawa ili awe na maisha mazuri lakini ajue kwamba kitu cha muhimu ni Taifa lake. Asifikirie kuhusu mshahara zaidi ya kile kitu ambacho tunakijenga. Tukifikiria vinginevyo elimu yetu itakuwa ''corrupted'' Ni lazima tujue kama Taifa ni wapi tunataka kwenda na aina gani ya elimu tuwape watu wetu. Tusipojenga structure nzuri Taifa letu hatutafika mbali. Haya mambo mengi haya yanahitaji kufikiri sana. Kama tutakusanya akili zetu pamoja katika ujenzi wa Taifa hili kwanini tusiendelee?


Hatutabadilisha chochote kama mfumo wetu wa elimu hatutaubadilisha na kumwezesha mwanafunzi kuwa mtu mwenye kufikiri zaidi na anayejitegemea. Iam not dreaming naelezea na plan, logical ''plans'' ambazo kila mtu anayefikiri anaona possibilities kwa taifa hili kutoka hapa lilipo kama mambo fulani tutayafanya na mengine kuayaacha.

Ni muhimu kujenga Taifa la watu wenye kufikiri zaidi. Intellectual development haitokani na kusoma tu darasani inatokana na kufikiri kwa muda mrefu. Lakini pia sacrifice ni muhimu hatutaweza kufika tunapotaka kufika pasipo kujitolea. Kwahiyo elimu yetu lazima ilenge kwenye intellectual development na sio tu kuwa elimu ajira. Ngoja nikupe definition ya education ambayo mimi naamini.

'' Education is the training of mental and moral powers as by the system of study and discipline'' kwahiyo ni muhimu kuzingatia hili. Elimu yeyote ni lazima izingatie mambo hayo ambayo yako kwenye hiyo definition bila ya hayo hatutaweza kuwa productive au kuleta mapinduzi katika Taifa letu. Ukombozi wa kweli katika Taifa letu utakuwepo tu kama tutazingatia umuhimu wa elimu na kumwezesha kijana kuwa mwenye kufikiri na kukuza intellectual powers na moral powers zake. Lakini pia kuwa mwenye nidhamu ambaye atakuwa na uwezo wa kuangalia nyumba yake vizuri na mwenye kuwajibika kwa jamii yake.

Tunategemea kwamba mwenendo wa mtu aliyesoma na yule asiyesoma uwe tofauti kwa jinsi anavyoona mambo na maarifa yanayotoka kinywani mwake. Tukielimika tutakuwa na uwezo wa ku discipline watoto wetu na tutakuwa na viongozi bora. Bila discipline hatutaweza kujenga chochote.
 
Shayu,Umenena iliyo kweli tupu, uwezo wa kuendelea kama taifa tunao,tatizo kubwa sana linakabili nchi zetu za kiafrika ni uoga wa watu wenye uwezo wa kuongoza kiasi kwamba,wale wanaotakiwa kupongoza wao ndiyo wanaongoza,huku viongozi hasa wakibaki kunung'unika tu.
Tatizo linalotukabili kama taifa ni kubwa sana,kama taifa hatujajitambua, hatua ya kwanza kwa mtu au taifa kuelekea maendeleo ya ukweli ni KUJITAMBUA. Tukijitambua sisi kama taifa ni nani, tuna nini na tunahitaji nini, kati ya tunavyo hitaji kipi ni Muhimu na haraka au kipi sio muhimu lakini ni cha haraka, ili tupange namna ya kupangua hitaji moja baada ya jingine kulingana na umuhimu wake na uharaka wake.
Kama taifa inabidi tuwe na NIA moja,wote katika ujumla wetu na tuelewe nini NIA yetu kama taifa,ni kipi tunatakiwa tukifanye leo, wiki ijayo,mwezi ujao na mwaka ujao,ikibidi hata miaka mia moja ijayo. Kama tutaendelea na maisha ya kuchangua viongozi kutegemea kile wakiitacho sera za vyama,eti mbunge huyu anasema mimi nitafanya elimu bure,huyu anasema matibabu bure, mwingine anasema atajenga barabara fulani, huku mwingine anazungumzia daraja fulani kwenye eneo lao la uchaguzi,maendeleo ni ndoto, Wakati umefika ambapo watanzania pale walipo wajue kwa uwazi kwamba kwa muujibu wa mpango wa maendeleo tusema wa miaka mitano ijayo,jilmbo fulani la uchaguzi linatakiwa kujengwa shule kadhaa za primary/sekondary ikiwa inajulikana hata eneo,hospital,barabara na madaraja pia, kazi ya wagombea kwa wapiga kura iwe namna ambavyo wanajieleza jinsi ya kufanikisha miradi ambayo tayari inajulikana,kama ni kwa kupunguza gharama na kuokoa wakati, wapiga kura wachague kiongozi wanayeamini atafanikisha ,malengo yanayojulikana lakini sio kila mmoja anaeleza kwa mbwembwe vitu ambavyo havipo hata kwenye mpango mkakati wa taifa.
Namna nzuri ya matumizi ya kile tulichonacho kama taifa, Huwa nasikitika sana nionapo ma V8 yamejazana barabarani yakiwa na namba za ST... na zingine yakionesha kuwa ni matumizi ya kodi zetu. Hapa panahitaji uinjilishaji mpya kwa viongozi wetu, kiongozi anaishi kiasi cha 10Kms toka Ofn kwake bado anatumia v8,for what ? kwani Vitz haiwezi kumfikisha ofcn, I mean toyota Vitz,ambayo gharama za mafuta ni ndogo hata za service ni ndogo,safari za mikoani watumie USAFIRI WA UMMA, hawa watu kabla ya kuwa na vyeo wanavyotunukiwa huwa ni watumiaji wa usafiri wa umma kwa hela zao hawko tayari kutumia magari ya kifahari hata kama wanayo,lakini kwa fedha za kodi za masikini hawaoni tabu kufuja,tunahitaji mabadiliko makubwa sana kifikra juu ya jambo hilo.
Yapo mengi sana lakini kubwa kuliko yote ni watz tujitambue na tubadilike tupende taifa letu...
 
Shukurani mtoa mada, Mkuu Shayu:
Umezungumzia mambo mengi nyeti sana, naungana nawe kwa zaidi ya 100%. Ngoja nami nichangie...
"Sasa tutabadilishaje Fikra za watu wetu kuwa CHANYA? Jinsi gani watapenda Taifa lao na kuleta matumaini kwa watu wote"
Hapo ndipo linapoibuka hitaji la kupata FALSAFA KUU YA TAIFA! Falsafa hiyo ndio itakuwa Dira ya kila kitu chetu, Msingi na Mpaka wa kila tutakalo kutenda, iwe kama Kioo cha kila siku kujitazama! TUSIACHWE HURU TU, NI LAZIMA TUFUNGWE NA KITU FULANI! Na si kingine ila Falsafa ya Taifa, nayo ndio itakayokuwa IMANI YA TAIFA LETU, tangu kichanga kinazaliwa kifundishwe kuishi IMANI hiyo!
Swali ni wapi hasa tunakoweza kuipata Falsafa hiyo kama Imani yetu na iwe na Tija kwetu? "TUKUSANYE AKILI ZETU KWA PAMOJA KUFIKIRIA UJENZI WA TAIFA LETU TUTAFIKA SEHEMU FULANI BORA" ndio! Na haya ni mawazo yangu juu ya wapi hasa tunakopasa kuitoa Falsafa Kuu ya Taifa letu, na kuifanya IMANI YETU! Mambo matatu muhimu sana katika kuunda Falsafa yetu, MAZINGIRA, NYAKATI na MANTIKI naita UTU!
1. Mazingira, ni WATU na SURA Ya NCHI yao(vilivyomo ndaniye)
2. Nyakati, ni mahusiano yaliyopo baina ya watu na Sura ya Nchi yao na baina ya wao wenyewe, mtu na mtu!
Kwa mfano, kama tunaishi milimani, na tunaamini mlima ni sehemu ya maisha yetu, basi hiyo falsafa inatakiwa izingatie hilo, isije ikaruhusu kuvunjwa kwa mlima wakati fikra na imani zetu haziafikiani na hlo!
Ili falsafa undwa isifanye mahusiano hayo baina ya watu na sura yao ya nchi, na yale baina ya mtu na mtu yasiKINZANE, hapo ndipo ndipo kiungo muhimu kabisa huitajika kukamilisha IMANI SAHIHI, nacho ni 3. MANTIKI, yaani UUWIANO SAHIHI/KUTOKINZANA/KUFIKIRIANA...naita UTU/HUMANITY!
Lazima falsafa hiyo izingatie MANTIKI, yaani UTU. Yaani, kwanini watu mahusiano ya watu na watu yawe hivi na si vile...kigezo kiwe KUFIKIRIANA, kwanini mahusiano ya watu na sura yao ya nchi yawe hivi na si vile, kigezo kiwe KUFIKIRIANA na si KUJIFIKIRIA! Kutokinzana kwa MAHUSIANO JENGWA!
Hapo tutakuwa tumepata Falsafa bora kabisa itakayopaswa kusimikwa AKILINI MWA WATU WETU na kuifanya IMANI KUU JUU YA MUNGU WETU!
Baada ya hapo kazi itakuwa ni KUISIMIKA imani hiyo kwa watu wetu. Kwanza nitoe ANGALIZO, hatua hii si ya miaka 10 au 20 ni zaidi ya hapo, hasa kuanzia miaka 50 mbele kama tungeifikia leo, kwahiyo hapa yote nayosema ni Dhambi kubwa kufikiri sisi tutayaona matunda yake, ni vizazi vyetu vijavyo ndivyo lengwa wa falsafa hiyo! Hivyo tunapotaka kuisimika imani hiyo yenye kutafuta Logical Relationship between people and their environment, and among themselves, ni lazima tutambue kuwa si drastic changes bali ni gradual changes. Sehemu kuu tatu za kusimika imani hii kwa watu wetu,...kupitia SHULE/Taasisi za elimu(kuanzia kubadili mtaala), kupitia tasnia ya HABARI, na kupitia SANAA zetu! Sehemu hizo zote tatu zibebe misingi na maadili ya IMANI hiyo, taratibu watu wataanza kubadili mitazamo yao juu ya kila kitu, hapo unaweza sasa kuwaambia hiki na hiki sicho na wenyewe wakatafakari vichwani mwao na kuona kweli. Automatically, utajenga "taifa bora kutokana na ubora wa mawazo ya watu wake"
ANGALIZO: Adui mkubwa kabisa wa kufikia malengo haya ni maneno mawili tu ambayo ni 'UHURU' ambao unarasimishwa na kuitwa 'HAKI', hizo ni dhana mbili adui kabisa katika Ukombozi wa Mtu Mweusi, ole ukafungwa nazo! Zenzewe zinakiuka MANTIKI, zinakumbatia ubinafsi mama wa MATATIZO YOTE DUNIANI. "Furaha yetu kama Taifa itatokana tu na mafanikio ya pamoja kama nchi" na huo ndio usahihi mkuu wangu Shayu.
Maisha ni Furaha, na Hakuna Furaha ya mtu ila WATU...UTU. UTU ni kipimo cha maendeleo kwa mtu mweusi, na si mali.
Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani.
Anaita sasa!
 
Aisee nimewasoma ndugu zangu mmenipa moyo.
Mambo mengi mliyozungumzia ni mambo ya msingi sana kwa mustakabali wa Taifa letu. Ni kweli Taifa lazima liwe na falsafa kuu ambayo itaendesha imani ya watu wake. Ili watu wajitambue wao ni kina nani na wanataka nini. Kwahiyo wanataka kujenga Taifa la namna gani. Bila kujua tunataka kujenga Taifa la namna gani tutakuwa tunapotea. Ni lazima tujue tunataka kujenga Taifa la namna gani. Lazima tutengeneze National spirit. Ili watu wa nje watujue watanzania ni watu wa namna gani na wana amini katika nini. National induviduality ni mihimu. Tukizungumza kuhusu induviduality ni Taifa ambalo lina exist without outside influence ambalo liko tayari kuunda culture zake na tradition zake na kujua mwelekeo wake kama Taifa. Taifa ambalo linajiunda lenyewe kutokana na mawazo ya watu wake sio mawazo watu wengine wowote. TAIFA LINALOJITEGEMEA.
 
Aisee nimewasoma ndugu zangu mmenipa moyo.Mambo mengi mliyozungumzia ni mambo ya msingi sana kwa mustakabali wa Taifa letu. Ni kweli Taifa lazima liwe na falsafa kuu ambayo itaendesha imani ya watu wake. Ili watu wajitambue wao ni kina nani na wanataka nini. Kwahiyo wanataka kujenga Taifa la namna gani. Bila kujua tunataka kujenga Taifa la namna gani tutakuwa tunapotea. Ni lazima tujue tunataka kujenga Taifa la namna gani. Lazima tutengeneze National spirit. Ili watu wa nje watujue watanzania ni watu wa namna gani na wana amini katika nini. National induviduality ni mihimu. Tukizungumza kuhusu induviduality ni Taifa ambalo lina exist without outside influence ambalo liko tayari kuunda culture zake na tradition zake na kujua mwelekeo wake kama Taifa. Taifa ambalo linajiunda lenyewe kutokana na mawazo ya watu wake sio mawazo watu wengine wowote. TAIFA LINALOJITEGEMEA.
 
Aisee nimewasoma ndugu zangu mmenipa moyo.Mambo mengi mliyozungumzia ni mambo ya msingi sana kwa mustakabali wa Taifa letu. Ni kweli Taifa lazima liwe na falsafa kuu ambayo itaendesha imani ya watu wake. Ili watu wajitambue wao ni kina nani na wanataka nini.Kwahiyo wanataka kujenga Taifa la namna gani. Bila kujua tunataka kujenga Taifa la namna gani tutakuwa tunapotea. Ni lazima tujue tunataka kujenga Taifa la namna gani. Lazima tutengeneze National spirit. Ili watu wa nje watujue watanzania ni watu wa namna gani na wana amini katika nini. National induviduality ni mihimu. Tukizungumza kuhusu induviduality ni Taifa ambalo lina exist without outside influence ambalo liko tayari kuunda culture zake na tradition zake na kujua mwelekeo wake kama Taifa. Taifa ambalo linajiunda lenyewe kutokana na mawazo ya watu wake sio mawazo watu wengine wowote. TAIFA LINALOJITEGEMEA.
 
HAKIKA, ni lazima tupate IMANI mama wa kila kitu chetu!
Imani hiyo ianzie tangu kuzaliwa mtoto, nini AONE/ASIONE, nini ASIKIE/ASISIKIE, nini ATENDE/ASITENDE, na nini AFUNDISHWE/ASIFUNDISHWE ili kumjengea uwezo wa KUFIKIRI na Kutambua nini ni sahihi kutenda na nini si sahihi kutenda!
Our Daily experience determines our thinking capacity to the degree of conciousness we have! Sasa tujiuliulize...
1. Elimu tutoayo inamjenga mtu wa aina gani? Kwangu ni mtumwa wa kila kitu! Leo hadi ngazi ya chuo kikuu kigezo cha ufaulu ni JINSI GANI UMEWEZA KUPEKUA VITABU VINGI "REFERENCES", unapojibu swali ni lazima useme "nani kasema hivyo na wapi umetoa" ole ukajibu swali kwa fikra zako tu, NI KOSA! Hapo ni vipi tunajenga CREATIVITY YA MWANAFUNZI, WAPI INNOVATIONS HAPO? Ni NDOTO!
Unamfundisha mtu kwa lugha ngeni, kesho unataka athamini kiswahili chake, wapi na wapi? Hatuoni KASUMBA YA UDUNI TUNAYOJIJENGEA? Je, si kikwazo kwa FIKRA ZETU JUU YA MAENDELEO YETU? Hakuna Falsafa inayotukataza hayo, ndio maana yanatendeka!
2. Rudi kwenye HABARI na SANAA!
Watoto wetu wanaona nini kwenye TV stations na wanasikia nini maredioni? Kila unako-tune unakuta kipindi kinachotukuza umagharibi, aiza kwa kuonesha yanayoendelea huko live, au kuoneshwa wazungu weusi wanavyo-behave kama wazungu! Nguo fupi, starehe nyingi, fuja pesa, ufuska, n.k watoto wetu wanapata wapi muda wa kufikiria mataifa yetu na magumu yake? TUNAWAJENGA WATU WA NAMNA GANI?
Kosa ni kukosa Falsafa inayozuia hayo! Tutafakari Cultural Revolution ya China, ni mfano bora sana!
3. Je, watu wetu wana-experience nini katika jamii? Tunafundishana nini tunapoweka kigezo cha Fedha/mali ndio Heshima/busara/hekima? Ni vipi utamfanya mtu huyu aliyekosa thamani kutokana na umasikini wake akalipenda taifa lake? Atakuwaje na mawazo chanya kwa taifa lake wakati jamii haimfanyi kuwa hvyo?
Kila ofisi utakayoenda, KITU KWANZA! Hata mahospitalini, HOSPITALI MOJA, WAGONJWA WAWILI WA UGONJWA MMOJA WANALAZWA WODI MBILI TOFAUTI KABISA! Na wote ni WATANZANIA, wanaodaiwa kumiliki Serikali moja na aridhi moja! FIRST CLASS HADI HOSPTALI? Pumbavu!
Ona mitaani nako, watu wanamajumba ya ajabuajabu magari ya thamani lukuki uwani, dada yangu anakufa njiani juu ya machela km. 25 kwenda kituo cha afya, HAKUNA GARI YA WAGONJWA hospitali, lakini wewe una magari kumi ya thamani uwani kwako! FIKRA GANI ZITAJENGEKA KWANGU?
Chanzo ni kukosa imani ya pamoja inayozuia hayo!
TUNA SAFARI NDEFU SANA, LAKINI HAISHINDIKANI!
TUANZE NA HATUA MOJA KWANZA!
Mungu wetu anaita sasa!
 
HAKIKA, ni lazima tupate IMANI mama wa kila kitu chetu!


Imani hiyo ianzie tangu kuzaliwa mtoto, nini AONE/ASIONE, nini ASIKIE/ASISIKIE, nini ATENDE/ASITENDE, na nini AFUNDISHWE/ASIFUNDISHWE ili kumjengea uwezo wa KUFIKIRI na Kutambua nini ni sahihi kutenda na nini si sahihi kutenda!
Our Daily experience determines our thinking capacity to the degree of conciousness we have! Sasa tujiuliulize...
1. Elimu tutoayo inamjenga mtu wa aina gani? Kwangu ni mtumwa wa kila kitu! Leo hadi ngazi ya chuo kikuu kigezo cha ufaulu ni JINSI GANI UMEWEZA KUPEKUA VITABU VINGI "REFERENCES", unapojibu swali ni lazima useme "nani kasema hivyo na wapi umetoa" ole ukajibu swali kwa fikra zako tu, NI KOSA! Hapo ni vipi tunajenga CREATIVITY YA MWANAFUNZI, WAPI INNOVATIONS HAPO? Ni NDOTO!
Unamfundisha mtu kwa lugha ngeni, kesho unataka athamini kiswahili chake, wapi na wapi? Hatuoni KASUMBA YA UDUNI TUNAYOJIJENGEA? Je, si kikwazo kwa FIKRA ZETU JUU YA MAENDELEO YETU? Hakuna Falsafa inayotukataza hayo, ndio maana yanatendeka!
2. Rudi kwenye HABARI na SANAA!
Watoto wetu wanaona nini kwenye TV stations na wanasikia nini maredioni? Kila unako-tune unakuta kipindi kinachotukuza umagharibi, aiza kwa kuonesha yanayoendelea huko live, au kuoneshwa wazungu weusi wanavyo-behave kama wazungu! Nguo fupi, starehe nyingi, fuja pesa, ufuska, n.k watoto wetu wanapata wapi muda wa kufikiria mataifa yetu na magumu yake? TUNAWAJENGA WATU WA NAMNA GANI?
Kosa ni kukosa Falsafa inayozuia hayo! Tutafakari Cultural Revolution ya China, ni mfano bora sana!
3. Je, watu wetu wana-experience nini katika jamii? Tunafundishana nini tunapoweka kigezo cha Fedha/mali ndio Heshima/busara/hekima? Ni vipi utamfanya mtu huyu aliyekosa thamani kutokana na umasikini wake akalipenda taifa lake? Atakuwaje na mawazo chanya kwa taifa lake wakati jamii haimfanyi kuwa hvyo?
Kila ofisi utakayoenda, KITU KWANZA! Hata mahospitalini, HOSPITALI MOJA, WAGONJWA WAWILI WA UGONJWA MMOJA WANALAZWA WODI MBILI TOFAUTI KABISA! Na wote ni WATANZANIA, wanaodaiwa kumiliki Serikali moja na aridhi moja! FIRST CLASS HADI HOSPTALI? Pumbavu!
Ona mitaani nako, watu wanamajumba ya ajabuajabu magari ya thamani lukuki uwani, dada yangu anakufa njiani juu ya machela km. 25 kwenda kituo cha afya, HAKUNA GARI YA WAGONJWA hospitali, lakini wewe una magari kumi ya thamani uwani kwako! FIKRA GANI ZITAJENGEKA KWANGU?
Chanzo ni kukosa imani ya pamoja inayozuia hayo!
TUNA SAFARI NDEFU SANA, LAKINI HAISHINDIKANI!
TUANZE NA HATUA MOJA KWANZA!
Mungu wetu anaita sasa!

Umenena vilivyo sina cha kuongezea hapo kila kitu ulichosema hakika kiko sawa. Hasa hiyo ya ''reference'' naamini kusoma au ' 'study'' is not merely absorption of the material written on the books but is the act of the investigation of the truth written on the books. Mtu anaweza kuandika kitabu kisicho kuwa na ukweli ndani yake ni lazima tuchunguze tusikubali kila kitu ni lazima tu challenge. Ni lazima tuanzisha ''new age of reasoning'' ndiye atakuwa mkombozi pekee kwetu. Elimu yetu imfanye mwanafunzi awe mwenye kudadisi na kufikiria. Ni lazima tutengeneze fikra za watu wetu upya. Kwa kuhubiri upya kuhusu uzalendo ili kujenga mawazo chanya ya watu wetu kwa Taifa. Ni lazima turudi katika utaifa. Ni lazima tuwe wenyewe na tusiwe copy ya watu wa magharibi. Ni lazima tujenge Taifa letu kwa mitazamo yetu na maono yetu.
 
Hakika mkuu wangu Shayu, "NI LAZIMA TUWE WENYEWE NA TUSIWE COPY YA WATU WA MAGHARIBI"
Leo mtu ukimwambia mtanzania kwamba tunapaswa kuishi Uafrika wetu, atakataa na kudai umepitwa na wakati eti NI LAZIMA TUENDANE NA WAKATI "UHALISIA WA DUNIA" dunia inavyotaka, hivyo ni lazima tuendane TUBADILIKE VILE WANAVYOTAKA WAO "TIME FACTOR". Lakini binafsi huwa najiuliza mara nyingi, "KWANINI KILA SIKU NI SISI TU WA KU-BE SHAPED? Why don't We Shape them? Kwanini mara zote NYAKATI zao ni bora tu tuziige ila zetu ni duni tuzitupe? Kwanini NYAKATI ZETU SISI ZISI-SHAPE THE WORLD? Kwanini zisiwe ndio UHALISIA WA DUNIA na sio uongo wao?" How long should we wait to proove their nonesence?
Wametuletea dawa za uzazi, matokeo yake ni kuongezeka kwa kuzaa kwa kisu.
Wameleta Private Ownership, matokeo yake ni uwepo wa Manzese na vibaka wake dhidi ya Masaki na Mafisadi wake kuongezeka!
Wametuletea dini, uislamu na ukristo matokeo yake UPENDO amani na Utulivu umepotea.
Wameleta Demokrasia, matokeo yake ni haya Hisia kuongaza Akili, ni upuuzi. Siku 5 za kazi watu wanajishughulisha na vyama, KAZI zimedoda.
Wameleta HAKI za BINADAMU, wanawake wanataka waoane, wanaume nao, wengne wanataka watembee uchi, kazini anataka afike anavyotaka, n.k
KWANINI NYAKATI ZAO NDIO ZIWE BORA WAKATI WOTE KUZIIGA, NA ZETU DUNI? Tulishatafakari MANTIKI ya yote tuyaigayo? Je, tulishatafakari MANTIKI iliyomo kwa yale yetu asilia tuyatupayo? Kwanini Africanism isiwe ndio UHALISIA WA DUNIA?
Minyororo tuliyofungwa inakazwa kila tunapoonesha imani ya mashaka kwao! Ni MITEGO, lazma tuumize vichwa, si kazi ndogo kuinasua!
NI LAZIMA TUISHI KULINGANA NA MAZINGIRA NA NYAKATI ZETU! Tutavunja makanisa na misikiti, majumba yao tufugia kuku! Tutasimamisha msingi mkuu wa maisha ya mwanadamu UTU kuwa muamuzi wa kila kitu chetu!
NO MORE SLAVERY-IMETOSHA! Sema HAPANA kwa Ukoloni mamboleo! Sema HAPANA si kwa maneno, bali ni kwa imani kwanza kisha matendo! Usimuache mtoto wako akaingia kwenye Utumwa uliomo baba, mfundishe ukweli ya kwamba "SISI NI WATU WEUSI TUNAOPASWA KUWA NA NAMNA YETU YA KUENDESHA SIASA ZETU, UCHUMI WETU na TAMADUNI ZETU kulingana na MAZINGIRA NA NYAKATI ZETU MAHUSUSI" Mtume kupigania hilo na ndio iwe HAKI YAKE YA KWANZA YA MSINGI! Wangu na wako wataungana hawatakuwa moja tena!
Tuambizane kweli, nyeupe ni nyeupe na nyeusi ni nyeusi.
UBUNIFU HAUJAWAHI KUFIKA MWISHO, TUKIAMUA TUNAWEZA. Nguvu yetu ni UMOJA na KUTHUBUTU.
Mungu wetu yu hai, tayari kutushindia vitani.
Anaita sasa!
 
Nimekusoma mtu wangu. Na nimekuelewa vilivyo. Ni kweli kila wakati wazungu wamekuwa ni watu wa kufungua kurasa za vitabu na kuzifunga kisha kusema sasa muelekeo ndio huu. Sidhani kama hii ni sahihi. Sisi tuna haki na uwezo wa kujenga jamii zetu kulingana na mawazo yetu wenyewe bila kuingiliwa. Hii inahitaji muda na jitihadi nyingi ili kufungua watu mawazo yao ili wafikirie upya na kujitambua kuwa wao ni kina nani na muelekeo wao ni upi. Tusipojitambua sisi ni kina nani tutaendelea kutawaliwa.
 
Wana JF , tunaweza kuwekeza katika fikra mpya za kuibua taifa la wa tu wanaofikiri, na kutumia falsafa ya mawazo chanya kuleta maba dilko , big up mkuu shayu.
Tuko pamoja mkuu.
 
Aisee nimepitia michango yenu tena nimeona uzalendo mwingi sana ndani yenu.
 
Back
Top Bottom