Labda tu nikushauri:
1) Hakuna kitu kibaya kama kusema unatafuta kazi ili uweze kutimiza mahitaji yako(unataka kazi ili upate pesa).
2) Unapoweka tangazo kama hili lazima usema una elimu gani au/na uzoefu wako ili tujue aina gani ya kazi itakufaa, pia unaweza kusema kazi zipi unaprefer. Hakuna mtu anayeweza kufanya kazi YOYOTE.
3) Mawasiliano ni muhimu, sio wote wana muda wa kuPM,mwenye shida ni wewe hivyo usinipe kazi tena mimi boss kukutafuta. Kuna watu sio member wa Jamii Forums hivyo hawawezi kukutumia msg lazima uweke mawasiliano.
ALL THE BEST