Hassan Mambosasa
JF-Expert Member
- Aug 2, 2014
- 3,358
- 4,518
Mtu uje kuniambia Trump ni ana nia nzuri, nitaomba ukapimwe akili kwanza. Nia ya Trump ni kurudisha nguvu ya Marekani iliyokuwa hapo awali na si kuongeza maendeleo, hivyo waafrika acheni kumshangilia huyu kiumbe akituponda kwa shida zetu ikumbukwe bila uwepo wa Marekani tusingekuwa hapa. Marekani hii hii katika mkutano wa Berlin wa mwaka 1884 hadi 1885. Wakiwa na miaka 108 tangu wapte uhuru walihudhuria kama mashahidi tu, hawakuwa na koloni lolote na walitamani haswa kulipata ila haikuwezekana. Alivumilia hadi mwaka 1945 kuisha vita ya dunia shida yake ayazidi nguvu mataifa ya Ulaya, kutimiza hayo hakuna vita ya dunia iliyoshiriki ardhini kwake.
Sasa wenzake walipofilisika na yeye akitajirika kwakuwa anawauzia silaha kipindi cha vita, aliwakopesha kwa masharti ya kuzipa uhuru nchi za kiafrika. Ilimradi atimize nia yake ya kuanzisha ukoloni mamboleo, Afrika hivyohivyo alifikia hatua hata kutoa silaha kwa vikundi vya wapigania uhuru ilimradi vimshinde Mzungu yeye apate ukoloni mamboleo. Sasa alifanikiwa ndiyo maana hatuendelei hadi leo, viongozi wa Kiafrika wengine wakawa vibaraka. Halafu Trump anawadharau waarabu, hivi anasahau kama nchi hiyohiyo ndiyo chanzo cha umasikini baadhi ya sehemu za uarabuni. Iraq iliingiza majeshi kwa kisingizio cha kuwepo silaha za maangamizi matokeo yake ni kuleta maafa makubwa. Mbalimbali na hapo hawahawa ndiyo chanzo cha kuwa masikini Iran kipindi cha nyuma, waliharibu utawala ule uliyokuwa ukisaidia wanyongea kisa umembana Mzandiki(Uingereza) akiwa chini ya kampuni ya Anglo presian oil company asiendelee kuwanyonya raia.
Nchi hii hii iliyoenda kuharibu Libya kisa ina maendeleo, hata Rais aliyekuwa madarakani(Obama) alikiri mwenyewe alifanya kosa. Libya iliyokuwa na serikali yenye kutoa huduma zote muhimu bure, kulipa wasiyojiweza hata wasipofanya kazi. Kaiharibu yote imebaki haina mbele wala nyuma. Marekani hii hii ndiyo chanzo cha machafuko ya Sudan ikawagawanywa na kuwa nchi mbili, chanzo ni kupigwa bao kwenye uwekezaji wa mafuta akaleta machafuko hayo wakose wote. Nchi hii hii ndiyo chanzo cha kuzuka machafuko Somalia, kaweka serikali vibaraka wake na watu hawataki ilimradi anyonye tu. Uzukaji wa vikundi vya upiganaji isingetokea isipokuwa nchi ile kuingilia serikali zingine.
Sasa huyu Trump aje kusimama na kuzikashifu nchi nyingine hazijajiendeleza angeacha unafiki walau kidogo maana hizo zote zimefanya juhudi ya kujisogeza ila nchi hiyo anayoiongoza hivi sasa ni kirusi mkubwa kwa kuzikwamisha. Wasingeingilia huenda Afrika ingekuwa mbali, mnamo karne ya 15 kwa wasomaji wa historia wanaelewa wazi kuwa Afrika na Ulaya zilikuwa sawa kimaendeleo. Kulikuwa na vyuo vikuu vikubwa hata kiwanda cha nguo kilichokuwa na nguvu kuzidi kilichopo Manchester England. Wavivu wa kusoma hawatajua haya watabaki kumuunga mkono huyo Mzungu mbaguzi. Hawajui hata kipindi hiko Marekani pale ilikuwa ni mapori tu hadi pale wazungu hao(mababu zao kina Trump) hawajawasili kutoka Ulya na kujitwaalia ardhi kinguvu ambayo ndiyo wanaiongoza hadi leo wakiamini ni ardhi ya wazungu.
Ukweli utabaki palepale kuwa wazungu waliturudisha nyuma kuanzia karne ya 15 na kuendelea. Kisha Mmarekani akaja kutuharibia mnamo karne ya 20(1900-2000) kipindi ambacho tunajiweka sawa kutokana na athari za mkoloni. Huyu Mzee (Trump) aseme tu shida yake ni kurudisha nguvu ya Marekani ambayo sasa hivi Urusi ndiyo anayo, vimebaki vyombo vya habari tu vikiisifia ni nchi yenye nguvu ila kiuhalisia imeshaangushwa. Ndiyo maana Trump alisema, "I will make America great again"
Kwanini iwe again(tena) yaani ataifanya Amerika kuwa na kubwa tena, hii inamaanisha si kubwa tena. Hivyo Waafrika wenzangu kabla ya kuanza kumshangilia huyu kisa chama chako hakijachukua nchi. Mwangalie kitu mnachokiunga mkono, yule ni mtu wa vita ni mojawapo wa sera zake. Hujiulizi hiyo kuiweka Amerika kuwa kubwa tena atatumia nini, maana maneno hayatoshi kuna njia mbadala. Ndiyo maana hata walipuaji wa nyuklia wa nchi ile mnamo mwaka jana walijiuzulu wakisema wanahitaji kuongozwa na Rais mwenye akili timamu si kama yule.
Ni hayo tu
Hassan Mambosasa,
Morogoro,
Januari 2017.