Habari wana MMU.
Nina rafiki yangu wa karibu sana ambaye ni ME! sasa huyu jamaa ana mpenzi wake! wamedumu katika mapenzi takribani mwaka mmoja na nusu.
Nikiri penzi lao limekua na misukosuko mingi, mara zote mimi ndo niliekua nawaunganisha pale wanapotofautiana.
Kilichonileta hapa ni kwamba jamaa yangu ameachana na huyu dada kwa sababu ya tabia zake za michepuko!(tabia za jamaa) Ugomvi wa kipindi hiki ulikua mkubwa hadi nikashindwa kusuluhisha!
Sasa huyu shem(mpenzi wake jamaa) tulikua tunawasiliana mara moja moja pindi wakiwa na jamaa! Lakini tangia waachane amekua akipenda tuwasiliane sana, kiasi kwamba nisipomtafuta kidogo tu,mara nsipopokea simu yake ni matatizo.
Huu ukaribu naona unapitiliza mara vimeseji vya kunchokoza! Mara ananitumia picha zake pasipo kumuomba, na pia kuomba zangu.
kilichonifanya nije hapa leo kanitumia meseji hii
"nakupenda sana sana kuliko nafsi yangu"
Hii meseji imeniacha na maswali mengi, huu upendo ni upendo gani?
kumbuka kwamba ni mtu wa dini sana, nkajiuliza pengine anamaanisha huu upendo wa kawaida hata kwenye dini zetu tunafundishwa?
maswali ninayojiuliza; x- wake anajua tunavyochati? na kama akijua atachukuliaje? Binafsi sitaki kutengeneza uadui na rafiki yangu.
Wana jamvi nisaidieni, je nimwambie rafiki yangu au nikaushe?
Msaada wenu tafadhali