Huyu ndugu yangu alinidharau nimemsamehe bila kumwambia ila kwenda kwake naona hata uvivu

Hii nasimulia kama njia ya kupata relief mana ni kitu nilikwazika sana kwann ameongea maneno Yale.! Au alikuwa na chuki za ndani na Mimi mana yeye anajiweza kwa hali zote lakin Mimi sikuwai kumuomba chochote labda alikuwa akishangaa Mno.

Kipindi namaliza chuo alinitafutia kazi kwa rafiki yake ambae wanajua nikafanya Kila kitu na nikapata Ile kazi lakin mwisho WA siku nilichomoa nikachagua njia nyingine

Sio kwamba nlikuwa Sina uhitaji WA KAZI ni vile tu nlikuwa sitaki kusaidiwa na yeye kwa sababu ni mtu WA maneno maneno

Katika familia yeye ndio top lakin namuona tu ana maisha ya kawaida japo ana mali.!

Nikapambana kwa njia zangu hivyo siku zinasogea.

Sasa wakati nimeona ikapita kama miezi sita hivi Huwa tunasalimiana sana lakin Mimi ndio napiga simu yeye hajawai hata kukosea namba akasema ngoja nimpigie kijana wangu

Bwana siku nampigia swali la kwanza akaniuliza vipi mkeo alishajifungua.???? Mimi kuuliza kivip ?? Najiuliza moyoni inamaana hajui kama harusi imepita hata hiyo miezi ya kuzaliwa mtoto haijafika au ni mtoto njiti? Au ni DHARAU tu au andhani nimeoa mke ambae alikuwa na mimba tayari?? Kama amedhani alikuwa na mimba inamaana Mimi nilikuwa mzinifu au sio !??

MIMI MOJA KATI YA SERA YANGU NI KUTENGENEZA KIZAZI SALAMA .KWAHIYO SUALA LA KURUKA RUKA HALIKUWEPO KATIKA UJANA WANGU COZ NAAMINI BABA UKIWA MZINIFU KATIKA FAMILIA WANAOFUATA WATAKUWA WAZINIFU ZAIDI YAKO .ZINAAA NI DENI LA AJABU AMBALO HALIPI ANAEFANYA BALI WANALIPA WANAOKUJA

Nikajiwazia sana ila mwisho WA siku nikaona kuendelea kupiga simu ni kama kujipendekeza sasa mana sio kwa maswali haya

Sikupata majibu ya kutosha ila mwisho WA siku nikaona kama kaongea kinafki sana

Pia mwisho nika conclude kuwa familia ya upande WA baba ni miyeyusho sana watu wanakuwaga na vinyongo vyao bila sababu za kueleweka.!!!!

HIVYO
Pole Sana Kwa changamoto ambayo umekutana nayo, cha Msingi Kwanza msamehe Sawa Sawa na maandiko matakatifu tusipowasamehe wengine Mungu atatusamehe , kusamehe kuna Jenga ndani yako na Moyo wako unakuwa na Amani na watu wote , hakikisha unakuwa na Amani juu yake hii itakusaidia , kingine inawezekana kabsa kuna maneno ambayo umeskia juu ya ndugu yako au experience juu yake kutokana na upande wa Baba yako ukawa na mawazo tofauti na halivyo , karibu kutafakari kile unachoskia maana mazungumzo mabaya uharibu tabia njema na mwisho hata kama anatabia mbaya hauwezi kumbadilisha asipokupigia simu ni Sawa akikupigia pia shukuru Mungu na Maisha yaendelee
 
Una TATIZO LA KISAIKOLOJIA linaitwa Paranoid personality disorder (PPD) , nenda katafute TIBA … mwanao hana shida wewe ndio mgonjwa
 
Comment nyingi zinaonekana wewe mtoa mada ndo mwenye matatizo so chukua hatua jitafakari
 
Acha uvivu.....jaribu kuconclude vizuri mkuu
Yeye ndiye ana shida sio ndugu yake.
Hivi kwa mfano wewe ni mwanafunzi wangu nimekufundisha A Level, halafu ukaenda chuo.
Upo mwaka wa pili halafu nakuuliza, vipi umeshamaliza chuo?
Wewe binafsi utajisikia vibaya? si jambo la kawaida tu hili!

Mtoa mada ana unyonge dhalili kama watu walivyosema.
 
Yeye ndiye ana shida sio ndugu yake.
Hivi kwa mfano wewe ni mwanafunzi wangu nimekufundisha A Level, halafu ukaenda chuo.
Upo mwaka wa pili halafu nakuuliza, vipi umeshamaliza chuo?
Wewe binafsi utajisikia vibaya? si jambo la kawaida tu hili!

Mtoa mada ana unyonge dhalili kama watu walivyosema.
Kabisa
 
Ndoa haipita hata muda mrefu unauliza vip kujifungua kama sio uchawi
kuna kuwa na mimba kipindi cha ndoa, kuna kusahau pia mkuu usimuwazie tofaut
ama aliuliza ajue usha tia mimba usiwe unachelewa chelewa
 
Back
Top Bottom