Jimmy George
JF-Expert Member
- Nov 28, 2016
- 1,733
- 1,648
Habari za asubuhi wana JF !!
Ni mwaka na miezi kama mitatu sasa imepita tangu Mheshimiwa Rais mstaafu JK akabidhi hatamu ya uongozi kwa Mheshimiwa Dr Magufuli,katika kipindi chake mengi yaliongelewa yaliyokuwa ya kweli na hata ya kutunga na pia alitukanwa sana na kuandamwa (binafsi sijawahi kumsema vibaya wala kumchukia kwangu ni kama role model).
Nimesikiliza na kuangalia mahojiano kati ya Ridhwan na Millard nikapata kujua machache kuhusu Kikwete(katika video hiyo kuanzia dakika 15:30 na kuendelea)
Nimegundua haya:
1. Aligundua nguvu yake kama Rais na kufanya lolote kwa wanaomtukana lakini hakutaka kufanya lolote baya aliwahurumiwa watu wake akijua wakati unafika watajua thamani yake.
2. Alipokuwa na hasira au mambo kumuendea vibaya aliacha muda uamue wala hakukurupuka kutoa maamuzi.
3. Si kweli kwamba Membe ni ndugu yake kama wengi tulivyokariri.
4. Hana ugomvi wowote na Lowassa na bado wanawasiliana kwa mambo mbalimbali.
5. Ni mfuatiliaji wa mambo mbalimbali ya mtandaoni.
6. Alipenda wengi waamue jambo wala si kufanya jambo kwa ajili ya faida yake
-uchaguzi wa ndani wa CCM 2015 ulithibitisha hilo kwa kutopitisha majina au kuwatetea marafiki zake Lowassa au Membe
7. Hupenda mtu aamue kile anachokitaka na si kumpangia kwa kuwa yeye ni mkubwa.
Kikwete