Huyu ndiye Zitto mnayetaka aingie UKAWA?

Mhere Mwita

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
235
1,275
1. Kumekuwa na wimbi na msukumo wa Viongozi wa ACT kusukuma agenda ya ACT/Zitto kuingizwa UKAWA baada ya siku za karibuni kuonekana anapambana na serikali kwenye social media na badae kwenye kampeni za udiwani.

2. Swali muhimu katika ushirikiano wowote ni kama CHADEMA tunataka nini Zitto/ACT watuongezee ambacho hatuna na hatuwezi kukipata isipokuwa kwa kuwa nae?

Mwandishi mmoja nguli Ansbert Ngurumo amesisitiza chama kijielekeza kuunganisha watu wenye dhamira sio vyama.Nakubaliana nae!

Ebu tujikumbushe kidogo kuhusu mwaka1 tu wa siasa za huyu mtu;

1. Aliingia kwenye kampeni 2015 kwa kumtukana Lowassa na CHADEMA ili JK, mfumo na CCM ama impe pesa imbebe kujenga chama na wagombea wake. Akapata alichopata, akashinda kiti1 nchi nzima! akaanza kuhisi CCM sio wema lkn hakukata tamaa.

2. Akaingia bungeni kupingana na ukawa na akabaki bungeni ukawa ilipotoka kwa kutotambua matokeo ya Zanzibar na Shein kama Rais, ili CCM, Mfumo na JPM wamwamini kumpa PAC. akakosa.

3. Akaona njia pekee ni kupambana na JPM ili kumtisha. JPM pasua kichwa, hakutishika hivyo akatafuta njia nyingine.

4. Akaona CUFinapasuka akahisi anaweza kufaidika akamunga mkono Lipumba dhidi ya Maalim Seif akiamini nguvu ya Lipumba ni ya CUF bara anaweza kuunganisha akatengeneza UKAWA yake na bwana yule.

5. Alipoona hailipi sana kwani Lipumba hana nguvu zaidi ya kubebwa na utawala, akamua kurudi kwa nguvu UKAWA kutafuta ushirikiano kwa kasi kuanzia bungeni.

6. Akaona ukawa inamwona msaliti akamua kufanya mashambulizi kwa nguvu dhidi ya serikali na kutumia baadhi ya vijana wa CHADEMA kwenye mitandao ili aaminike kwa kusikika kila siku zaidi ya kiongozi yeyote na chama chochote. Hii ikazidisha mjadala wa kwann ACT ni muhimu kuwemo UKAWA, hoja inayochagizwa pia na wenye malengo tofauti.

7. Sasa kwenye udiwani juzi ameweka msuli wote kuonesha mabavu ili chadema imuone muhimu kumwingiza UKAWA na utetezi ukiwa ndio chama kilichofanikiwa kwa kupata kura nyingi ukilinganisha na vyama vingine ukiondoa Chadema na CUF.

SWALI LINABAKI KUWA KUUNGANA NA AKILI YENYE MATUKIO HAYO NDANI YA MIEZI12 TU USHIRIKIANO HUO UTAKUWA NA HAKIKA KIASI GANI? NA ZAIDI KUUNGANISHA ACT ILETE NINI AMBACHO HATUNA NA HATUWEZI?
 
Nishaona UKAWA mnamkubali sana Zitto, hataki usajili wenu wanafiki wakubwa. Nyie kwa unafiki wenu miaka yote mnamtukana Lowassa lakini sasa hivi ndiye mwenye sauti CHADEMA. Zitto atawatesa sana achaneni naye kabisaaaa.
 
Mkuu watu kama wewe mkiwa 50 ndio anapatikana Zitto mmoja.

Zitto ni jembe mlimfanyia fitina mkamtimua CDM sababu tu alionekana ana nguvu kuzidi Mwenyekiti wenu.

Watanzania tunajua na Dunia inajua.
Hivi kama kwa tishio la kukamatwa na Polisi mtu anakimbilia kusiko julikana viongozi wangapi wa Chadema wangesha potelea porini? Kuwa mpinzani wa kweli ni kutokuogopa unachosimamia. Ndivyo walivyo wanamageuzi wote mahiri Afrika. Hilo la Kahama limeonyesha wazi ni mtu muoga na muoga hana nafasi Ukawa? Sasa ukiwa kiongozi muoga wafuasi ambao hata kings hawana watakuaje?
Mchukulie mtu kama Lissu, unamkamata na kunuweka ndani weekend nzima na kumleta mahakamani kumsomea shtaka lakini akitoka nje ya mahakama anaita waandishi na kurudia kusema kilekile kilichomshtaki kwani ndio anacho kiamini.
Huyo hata wafuasi wake wanamuamini
 
Kama kweli upinzani hauogopi polisi kwa nini UKUTA iliahirishwa?.Siasa zinabadilika na ndio mana huwezi kumuona Mbowe anakashifu viongozi,ndio mana kipindi hiki cha Magufuli hajawahi wekwa ndani,kwa sababu ni muoga?.
 
Aina hii ya watu wanabahati tu na aina ya watu wanaowapa kura, lakini hawastahili kuwa hapo walipo!
 
Mleta mada wajisikiaje? hakuna alie kuunga mkono kwenye chuki zako binafsi,
N mtoto mdogo tu ambae haelew kitu ndie atakae stahili kuelezewa uwezo wa Zitto ,

Presidential material iliyopo upinzan n Zitto Kabwe peke yake, kama ulikua hujui huo muunganiko wa ukawa unakosa nn, basi hiki ndio unacho kosa
 
badala ya kuleta hoja ya jinsi gani wanachama na viongozi wa CHADEMA" wajikite katika kukijenga chama ili kujiandaa na uchaguzi 2020 unapewa porojo za zitto' kama aliondoka ni maamuzi yake mbona sumaye na Lowassa waliondoka pia! leta hoja za kukijenga chama ili lookalike sio unaongea taarabu!
 
Kama UKAWA inatamani kufa fasta basi Zitto ajiunge UKAWA.Hakuna cha kukamatwa wala nini,ZZK ni agent wa serikali hawezi wekwa ndani kama Lema kinachofanyika ni kiki ya kumkuza ili waje kumtumia tena akishapata mashiko kwa watanzania,Zitto sio mpinzani,Zitto ni CCM,ni serikali,NAJUA CHADEMA HAIWEZI KUBALI KUMUINGIZA NYOKA NDANI YA NYUMBA KISA ANAKULA PANYA.
 
We mleta uzi ni kihi.o aisee!!yaani unamlaumu zzk kwa kumtukana lowasa wakati viongozi wote wa chdm walimtusi au unabisha nikuwekee nukuu?acha ujinga zito sio level za kina lema,tukatae tukubali upinzani wa kina lissu umepwaya kwa kumkosa mtu kama zzk
 
Kama UKAWA inatamani kufa fasta basi Zitto ajiunge UKAWA.Hakuna cha kukamatwa wala nini,ZZK ni agent wa serikali hawezi wekwa ndani kama Lema kinachofanyika ni kiki ya kumkuza ili waje kumtumia tena akishapata mashiko kwa watanzania,Zitto sio mpinzani,Zitto ni CCM,ni serikali,NAJUA CHADEMA HAIWEZI KUBALI KUMUINGIZA NYOKA NDANI YA NYUMBA KISA ANAKULA PANYA.
Zitto ni ccm,Zitto ni serikali vipi Lowasa,Sumaye nao ni wapinzani?.
 
Kama UKAWA inatamani kufa fasta basi Zitto ajiunge UKAWA.Hakuna cha kukamatwa wala nini,ZZK ni agent wa serikali hawezi wekwa ndani kama Lema kinachofanyika ni kiki ya kumkuza ili waje kumtumia tena akishapata mashiko kwa watanzania,Zitto sio mpinzani,Zitto ni CCM,ni serikali,NAJUA CHADEMA HAIWEZI KUBALI KUMUINGIZA NYOKA NDANI YA NYUMBA KISA ANAKULA PANYA.
Kuna kaukweli fulani vile
 
Back
Top Bottom