Huyu ndiye mwanamke wangu wa nguvu

mapanga3

JF-Expert Member
May 1, 2012
665
633
Happy woman day!
Wana Jf pamoja na ubize wa kudai vyeti vya Bwana Daudi lakini tusisahaau Leo ni siku ya wanawake.

Naamini kila mtu humu ana mwanamke wake wanguvu, yaani mwanamke ambaye ni mtu muhimu sana kwake. Ni vizuri kuitambua siku hii na kuwaonesha mama, Dada, shangazi, bibi wake, na wapenzi wetu thamani na michango yao ktk maisha yetu na mafanikio.

Kila mtu amefika mahali alipofikia kwa sababu kuna mchango wa mwanamke.
Kila mtu aweke wazi mwanamke wake wa nguvu ili kuthamini na kuwatia moyo.

Kwangu mimi mwanamke wangu wa nguvu ni mama yangu, ndiyo yeye ndiyo kanifanya Leo niwe wa thamani hii.
Asante sana mama.
 
Mwanamke wangu wa nguvu ni Dada yangu, Mungu aliwachukua wazazi wangu siku moja kwa ajali nikiwa bado Nina miaka 8, lkn Dada yangu alisimama kwenye nafasi ya wazazi alihangaika namimi mpaka nikawa moniccca kweli. Asante Dada yangu Winfrida Mungu akupe maisha marefu.
 
Pole sana...MOLA ampe maisha marefu Dada yako kwa kuku kuza ukawa mdada mzuri, mpole na muungwana.
 
images(3).png
 
Mmewapigia simu hao akina mama wa watu?? Mmewatumia hata pesa ya matumizi? Hata upande wa khanga tu
 
Mwanamke wa nguvu kwangu ni mama yangu kipenzi. Huyu mwanamke jamani ana upendo na uvumilivu wa ajabu.
Yaani nitamani niwe mwanamke, mke na mama kama yeye. Kwa mda mchache nnaokua nao tukiwa pamoja ananifundisha mengi sana! Nimefika hapa nilipo kwa maelzi yake na maombi yake kwangu.
I love her saana!!! Bila yeye baba yetu sijui angekua mwanaume wa aina gani.!
 
Mwanamke wangu wa nguvu ni Dada yangu, Mungu aliwachukua wazazi wangu siku moja kwa ajali nikiwa bado Nina miaka 8, lkn Dada yangu alisimama kwenye nafasi ya wazazi alihangaika namimi mpaka nikawa moniccca kweli. Asante Dada yangu Winfrida Mungu akupe maisha marefu.
Pole Monica
 
Mwanamke wa nguvu kwangu ni mama angu kipenzi ambae ndo rafiki yang mshauri wangu kipenzi changu na ndo kila kitu kwangu nakuombea kwa mwenyezi Mungu azidi kukujaalia umri mrefu mama angu niishie hapo maan siwezi kuyamaliza mema yako kwa kuyaandika maan ni mengi mnoo nakupenda sana mama angu
 
Nani kama mamaeee.....nanikamamamaeee, mama alikuja kunisalimia toka kijijini kwa kuwa leo ni siku yao nilichofanya bila yeye kujua ni kualika akina mama majirani ili waje wamsalimie nikaandaa kasherehe sasa wanaendelea kuburudika bila wao kujua nina maana gani, nipo katikati yao nawakodolea macho kodo kwa furaha, na hawajui ni kwa nini nina furaha, lakini kutokana na mahangaiko ya mama niliyoyaona nikiwa mdogo ndo mana nikaamua kukaa na mtoto wangu mwenyewe sitaki apate shida ningali nipo mzima.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom