Huyu Ndiye Mohamed O. Mchengerwa

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Huyu Ndiye Mohamed O. Mchengerwa

Teuzi Mpya za Baraza la la Mawaziri zimemuibua kijana Mzalendo na Mchapakazi Mohamed Omar Mchengerwa.
Mh.Mchengerwa ni Mbunge wa Rufiji toka 2015 akichukua nafasi ya aliyekuwa Waziri wa Afya wakati wa Mzee JK Dr Seif Rashid.
Mh.Mchengerwa ni Mwanasheria msomi na bobezi katika eneo la Mahakama alikofanya kazi kabla ya kuwa Mbunge.

Mchengerwa Ni Mwanafunzi wa Shahada ya Tatu (PhD) katika Siasa na Mahusiano ya Kimataifa katika Chuo Kikuu Cha "Girne America University" nchini Cyprus.

Ukiacha hayo amekuwa Msaidizi wa Jaji Mkuu wa Tanzania kwa miaka sita(2009-2015).

Bungeni kwa muda mrefu amekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria mpaka wakati huu Mh.Raisi anamteuwa kuwa Waziri.

Mh.Mchengerwa ni miongoni mwa Wabunge wenye kujenga hoja zenye maslahi makubwa kwa wananchi ya Jimbo la Rufiji na Tanzania kwa Ujumla.

Mfano hoja yake kwa nini tozo ya huduma inayopaswa kulipwa na Kampuni za kigeni zinazojenga Mradi wa Umeme wa Mwl Nyerere ilipwe halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni badala ya Rufiji kwenye Mradi imepelekea wilaya Rufiji kupokea mabilioni ya pesa kutoka kwenye makampuni hayo na kuchangia kwa kiasi kikubwa maendelo ya wilaya hiyo kongwe, (Rufiji ni Wilaya toka Mkoloni).

Michango yake Bungeni imechangia kiasi kikubwa kuanza kwa Mradi wa Umeme wa Mwalimu Nyerere uliokwama kwa zaidi ya miaka 60(Rejea Ansad Bungeni).

Wakati fulani aliamshra fulaha Bungeni alipokumbusha ahadi ya Mwalimu Nyerere ya kujenga Barabara Tarafa ya Mkongo wilayani Rufiji aliyoitoa 1955 wakati wa Kikao Cha Halmashauri kuu ya Tanu kikichofanyika Tarafa ya Mkongo Rufiji.

Kwa Jitihada zake Mh Mchengerwa, halmashauri sasa wanajenga Shule ya Upili Tarafa ya Mkongo yenye jina la Muaaisi na Mpigani Uhuru wa Nchi hii Bibi Titi Mohamed.

Kwa Jimbo lake hakika ni Mwanasisa wa kupigiwa Mfano na kwa wanaojua siasa za Rufiji huwa ni ngumu Sana kwa Mbunge kupenya awamu ya pili lakini kwake haikuwa kazi ngumu sana kutokana na aliyoyafanya ndani ya awamu yake ya kwanza.

Kuanzia katika Utatuzi wa migogoro ya wakulima na wafugaji,Changamoto za maji,Barabara na Umeme.

Hatma ya hekari elfu hamsini zilizotengwa kando ya Mto Rufiji baada ya kukamilika ujenzi wa mradi Mwalimu Nyerere.

Kutowajibika ipasavyo kwa Mamlaka ya uendelezaji wa bonde la mto Rufiji/Rubada(Kwa mujibu wa tafiti kilimo Cha mpunga katika bonde hili kinaweza kulisha nchi mzima ya Tanzania).

Mara Kadhaa akijenga hoja bungeni kuwa ufumbuzi wa tatizo la sukari Tanzania utapatikana katika Bonde la Mto Rufiji(Kuna wawekezaji zaidi ya watatu wa viwanda vya Sukari Rufiji) ndio kusema.

Mh.Mchengerwa ni Mbunge wa kuwasemea Watanzania.

Hakusita kuwa Mkali na Kusimamia alichokiamini wakati fulani alihoji Bungeni kwa lugha Kali kidogo ni Kwa nini Kampuni ya Sukari ya Kagera kukopa mabilioni ya Pesa na Kwenda kuwekeza DRC wakati nchi inashida kubwa ya Sukari,hayo na mengine mengi yenye Maslahi ya Tanzania yamekuwa ndio Kilio chake.

Jimboni kwake amefanya mengi huwezi kuweka yote hapa ila mawili yatakayomfanya akumbukwe na wana Rufiji ni Kuhakikisha kila Tarafa inakuwa na Shule ya A level(Mkongo,Ikwiriri na Shule pekee ya mabinti Mohoro)

Kutekeleza kwa asilimia 100% agizo la Serikali kuu kujenga madarasa mapya kuchukua wanafunzi waliokwama kuingia kidato cha kwanza(Madarsa 13 ya kisasa ndani ya Mwezi mmoja) na kufanya kuwa miongoni mwa halmashauri zilizofanya vyema katika zoezi hilo nchini.
Michango yake bungeni pia imepelekea Rufiji kutengewa fungu na Tamisemi kujenga jengo jipya halmashauri ili kuondokana na Boma wanalolitumia sasa lililorithiwa toka kwa Mjerumani.

Bila kusahau hoja yake Bungeni kwa nini Mradi wa Umeme wa Mwl Nyerere Rufiji utakaotoa ajira ya zaidi 6000 na serikali kuwekeza zaidi ya trilioni 6.5 unafanyika katika wilaya ambayo haina benki ya Serikali na hata binafsi imepelekea serikali kupeleka benki katika wilaya hio Kongwe.

Ndio kusema Mh.Mchengerwa anawasemea watu wake na taifa kwa Ujumla.

Ushauri wetu kwake aendelee kusemea wananchi wake na taifa bila kusahau Kilio chake cha muda mrefu juu ya ujenzi wa Barabara ya Kibiti Mloka kiwango cha lami.

Kwani asilimia kubwa Malighafi za mradi ya Mradi wa Umeme Mwl Nyerere hupita kwenye barabar hii ambayo haiko kwenye hali nzuri hasa kipindi Cha Mvua.

Pia asimamie ahadi na Ilani ya Chama Cha mapinduzi ujenzi wa barabara Nyamwage Utete ambapo wabunge kabla yake hawakufanikiwa kufanya hivyo.

Kwa uzalendo wako na uchapakazi tunaamini utatumikia taifa ipasavyo katika jukumu lako jipya la Waziri ofisi ya Raisi utumishi na Utawala Bora na Kumsaidia Mh. Rais katika kazi yake ya kuijenga Tanzania Tuitakayo.
 
Sawa. Ila nataka kukumbusha tu kuwa ilikuwa Rahisi kwake kupita awamu ya pili kwa kuwa mwaka 2020 hakukuwa na Uchaguzi zaidi ya Uchafuzi. Ni hilo tu. Tuweke kumbukumbu sawa.
🙏🙏🙏✔️
 
Back
Top Bottom