Huyu mwanasiasa sio mnafiki?

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Kama alikuwa na takwimu kama hizi alikuwa wapi kuzitoa hapo awali?

Kwa nini hakutoa ushauri wa kiuchumi? Huu ni unafiki wa kisiasa.
Screenshot_20210401-215705.png
 
Zito hakuwahi kuwa mnafiki. Mtu pekee aliyechambua na kukosoa mwenendo wa kiuchumi Wakati wa hayati Magufuli bila ouga. Mpaka wakatunga sheria ya takwimu kumdhibiti.
Mbali na UFIPA ngoja waje GREEN
 
Zito hakuwahi kuwa mnafiki. Mtu pekee aliyechambua na kukosoa mwenendo wa kiuchumi Wakati wa hayati Magufuli bila ouga. Mpaka wakatunga sheria ya takwimu kumdhibiti.
Zitto kwa asili ni mnafiki mkubwa sana,yeye sehemu anapo ona pana ulaji au faida kwake yupo tayari kuuza utu wake ili afanikiwe
 
Huyu jamaa anakua kama hasomi vitabu bwana au ndio muendelezo wa chuki zake.

Haiwezekani mazingira yakabakia yale yale kwa kipindi cha miaka 20,

Anasahau kuwa sasa tunapambana na nini , ingawa sisi hatujajifungia ila wenzetu wamejifungia na hiyo imetuathiri sana.

Pamoja na kwamba tulikua tunafanya miradi mikubwa sana ya kimkakati tena katika wakati mgumu wa janga la korona lakini bado tulifanikiwa kuingia uchumi wa kati. Hilo ni jambo kubwa sana na la kujivunia.
 
Siamini kama leo hii bunge limewakosa watu kama Zitto Kabwe, Tundu Lissu, Mbatia. Cha kusikitisha ni kwamba waliopo huko ndani ya bunge wanashangilia kwa kukosekana kwa watu hao.

Uccm unaliangamiza na kulirudisha nyuma kimaendeleo hii nchi
 
Alikuwa wapi vipi,sema wewe ndio ulikuwa ufatilii.haya mambo yaliongelewa sana pale ilipotangazwa kuwa Serikali sasa ipo uchumi wa kati watu walijaribu kufafanua kwa kila namna watu waelewe kuwa ni kiini macho-lakini sijui Magufulialiwalisha watu vitu gani hata uonge hawakusikii.

Nakumbuka kwenye msiba was Mzee Mkapa Kikwete naye aliongelea vizuri sana,lakini watu bado wanatukuza maneno ya Magufuli.

Toka Mwaka 2016 uchumi wa Tanzania ulianza kudolola kukawa na matamko mengi kuhusiana na hali hiyo kutoka kwa Wanasiasa wa Upinzania hasa Zitto kabwe na Lissu wakielezea Hali ya uchumi kwenye vyombo vya kimataifa na vya ndani-hali iliyopelekea kutungwa kwa sheria ya Takwimu.

Au wewe mwenzetu ulikuwa USA kipindi hicho??
 
Back
Top Bottom