HUYU KIJANA ASAIDIWE KUPATA ELIMU YA JUU

CALMAN

Senior Member
May 23, 2013
190
54
MH MBUNGE ZITTO ZUBERI KABWE ALIKIRI KUSHIKWA MKONO KTK ELIMU YAKE NA MAREHEMU SAMWEL SITTA (R.I.P) LEO WEWE UKO WAPI? MSHIKE MKONO KIJANA.
WABUNGE WOTE NA WADAU MBALIMBALI MSAADA WENU NI MUHIMU SANA.

[HASHTAG]#WATANZANIA[/HASHTAG] NIMEONEWA#bado nina ndoto ya kusoma*
*#NishikeMkonoKatikaSafariYanguYaChuo*

Mficha maradhi kifo humuumbua, huu ni msemo es-tu. Naam msemo wa kiswahili. Siku niliyopokea barua ya kukatishà masomo yangu kwa mara ya pili katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) Pamoja na pole nilizopewa kutoka kwa watu mbalimbali, ni uongo na dhambi kubwa kama nitasema nipo sawa. Siko sawa ndugu zangu.

Moyo wangu umejaa majeraha na uchungu mkubwa wa manyanyaso ya kubaguliwa kupata Elimu katika nchi yangu. Katika taasisi iliyojengwa na kodi za Wavujajasho na rasilimali za taifa hili.

[HASHTAG]#Ndoto[/HASHTAG] yangu ya kuwa Mwanasheria Imepepeswa.

Najiuliza, kwanini ninyimwe haki ya kusoma katika vyuo vya umma.?

Hata kama ilikuwa ni kosa mwaka 2011 kuwatetea watoto wa masikini kama mimi kupata mikopo na kupigia kelele udhalimu wa bodi ya mikopo wa kupoka fedha za masikini kupitia majina hewa, mbona nimeshatumikia adhabu ya kukaa nje ya chuo mika 6 ( deterrence theory).

Adhabu hii licha ya kutokuwa halali, ni adhabu kubwa sana inayozidi hata kipimo cha sheria ya udahili kifungu cha 43(1) kinachotaka mwanafunzi aliyefukuzwa kuruhusiwa kuendelea na masomo yake baada ya miaka 2 kupita. Uongozi wa UDSM umekataa kuniruhusu niendelee na masomo yangu.

Nimeumia sana kuona haki yangu ya kupata elimu ya juu ikifungwa na wenye funguo bila kujali, wasinioneshe funguo licha ya jitihada za zaidi ya miaka mitano kuipigania haki hiyo kwa njia za kidiplomasia na kisheria (mahakamani).

Sitakiwi kusoma kwenye vyuo vya umma Tanzania.

Licha ya kuwa na matumaini ya kupata haki yangu ya kupata elimu, nguvu yangu hasa ya kiuchumi imekuwa ndogo kwani vyuo vya binafsi ni gharama kumbwa kidogo. Nahitaji kiasi cha million 7.6 kuwa na uhakika wa kupata elimu yangu.

kama mdau wa elimu, mtetezi dhidi ya uonevu, udhalimu na ubaguzi... Nisaidieni kutetea ndoto yangu. Natambua ukarimu wenu watanzania. Natambua mnavyothamini elimu. Pia natambua mnavyochukia vitendo vya ukandamizaji na vile vya watu wachache kuamua maisha ya wengine kwasababu tu hawapendi mawazo yao. Nimekuja kwenu mnisaidie ndugu zangu.

Tumia njia zifuatazo kunisaidia kadri utakavyojaliwa.

MICHANGO ITUMWE:

CRDB a/c No. 0152436033400

M. Pesa: +255 765 443 728

T. Pesa: +255 718 221 535

Airtl.M: +255 683 528 675

Namba zimesajiliwa (Alphonce Lusako M.)

Shukrani.

Alphonce Lusako.

[HASHTAG]#Mytake[/HASHTAG]
Tushirikiane kwa namna yoyote kumsaidia kijana huyu mwenye kiu ya kuendelea na masomo yake. Very touching
3201bd44706b3a84776cd1a8d6f4f6b5.jpg
 
Aende kwa wanasiasa waliokuwa wanamsaidia kuratibu migomo pale udsm,sasa hivi wamemsusa,hivi CHADEMA waliomtumia kisiasa hawawezi kuchota hela ya ruzuku wakampeleka hata UGANDA hapo MAKELELE akasome SHERIA?Mbona CHADEMA kinatoa mamilioni kulipia kesi za upuuzi za kina LEMA NA LISSU.

NA HUYO DOGO AJIFUNZE , WANASIASA SIO WATU WANAKUTUMIA KAMA KONDOMU, ASHUKURU HATA HIVYO , ajiulize yupo wapi BEN SAA8?

JUZI KATI KINA MALISSA WALIMPELEKA LANDMARK HOTEL HAPO RIVERSIDE KUIPINGA NA KUICHAFUA SERIKALI,

Hizo pesa za kukodi hapo LANDMARK HOTEL zinatoka wapi kama si kwa wanasiasa wanaotaka kumtumia kama daraja kuitukana serikali ,anayoililia sasa hivi.
 
Aende kwa wanasiasa waliokuwa wanamsaidia kuratibu migomo pale udsm,sasa hivi wamemsusa,hivi CHADEMA waliomtumia kisiasa hawawezi kuchota hela ya ruzuku wakampeleka hata UGANDA hapo MAKELELE akasome SHERIA?Mbona CHADEMA kinatoa mamilioni kulipia kesi za upuuzi za kina LEMA NA LISSU.

NA HUYO DOGO AJIFUNZE , WANASIASA SIO WATU WANAKUTUMIA KAMA KONDOMU, ASHUKURU HATA HIVYO , ajiulize yupo wapi BEN SAA8?

JUZI KATI KINA MALISSA WALIMPELEKA LANDMARK HOTEL HAPO RIVERSIDE KUIPINGA NA KUICHAFUA SERIKALI,

Hizo pesa za kukodi hapo LANDMARK HOTEL zinatoka wapi kama si kwa wanasiasa wanaotaka kumtumia kama daraja kuitukana serikali ,anayoililia sasa hivi.
Hata hela ya kulipia masaburi yako wanatoa
 
Mchuma janga hula na wakwao.

Waliokua wakimshabikia na kumuita shujaa leo wamemkimbia
 
Zitto alisaidiwa na Sitta kupata shule aliyoitaka akiwa na sifa zote, hakusaidiwa kufanya siasa akiwa shuleni.
 
Back
Top Bottom