Cesar Saint
JF-Expert Member
- Nov 18, 2016
- 423
- 727
wakwanza ndo weweKuna watu watakuja kusema anapewa info na Aliens
Najua ni raia wa Africa Kusini mzaliwa wa Pretoria. Ambaye alikimbilia Canada baada ya serikali ya makaburu kumtaka ajiunge na jeshi ili awe anatekeleza sera za kibaguzi za serikali hiyo.
Kwake yy aliona hiyo ni kero akaenda kutafuta maisha Canada na baadae USA ambako amekuwa mbunifu na mwekezaji.
Ukiacha kampuni yake maarufu ya magari yanayoendeshwa kwa umeme ya Tesla na ile ya anga ya Space X, Elon Musk pia ndiyo mbunifu wa technolojia ya usafiri wa kasi "hyperloop" ambayo bado ipo kwenye design stage.
Hyperloop - Wikipedia
SpaceX - Wikipedia
https://en.m.wikipedia.org/wiki/Tesla,_Inc.
Huyu ni mzungu mzaliwa wa Africa kusini kwa sasa ana uraia wa Marekani ni kati ya ma 'genius' watu wenye akili nyingi waliopo duniani kwa sasa ni mtu ambaye anataka kubadilisha kabisa baadhi ya mambo hapa duniani kutokana na ugunduzi wake, kwa mfano kutoka kutumia magari ya mafuta na kuanza kutumia magari yanayotumia umeme na nishati ya jua hii ni pamoja na magari ya kujiendesha yenyewe bila dereva, ana 'project' nyingine kubwa ya kupeleka binadamu kuishi kwenye sayari ya Mars. Ana project nyingine ya 'HYPERLOOP' hii ni teknolojia ya treni yenye kasi zaidi na salama ambayo itakuwa inatumia mwendo kasi wa kilomita 1200 kwa saa, treni hii itakuwa inapita ndani ya 'tunnel' ambalo halina hewa 'vacuum' na kuifanya ikimbie zaidi kwa kutumia umeme kidogo sana. Project nyingine kubwa anategemea kurusha 'satellite' 4425 kwa ajili ya mawasiliano ya simu na 'internet' na atafanya mawasiliano yapatikane kokote ulipo duniani kwa gharama nafuu zaidi kuliko sasa. Hizo ndizo baadhi ya project zake chache na ndiye anayetegemewa kuja kuwa tajiri namba moja duniani siku zijazo.
Yaani umeweza tafuta info zote hizo halafu bado humjui Elon ni Nani?
Salamu wakubwa
Kila mara katika pitapita zangu kwenye mitandao na majarida ya ugunduzi wa teknolojia na habari za mambo ya “space” nimekuwa nakutana na jina la huyu jamaa ELON MUSK
Nimemwona kwenye project nyingi za NASA kama vile Falcon 9 project
Pia katika Red Dragon Space mission on mars
Kitu kingine anachofanya hivi karibuni ni SpaceX/Tesla hyperloop pusher pod project akiwa kama Tesla Shareholder na pia sina uhakika lakini nadhani anamiliki The boring company ambayo ndio inafanya mambo yote haya niliyosema juu
Kwa anayefahamu kuhusu huyu jamaa tafadhari anijuze kuhusu huyu Elon Musk .