Huyu baba mwenye nyumba ni muuaji, hakika anatuua

A JUSTMAN

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
439
555
Heri sana ya mwaka mpya!

Nyumbani kwetu tulipatwa na maafa makubwa ya tetemeko la ardhi, kwa uzito wa tetemeko lile nyumba yetu ilianguka na kuharibika vibaya na tulipoteza baadhi ya ndugu kwenye familia yetu hawa ndugu zetu walifariki dunia.

Wakati wa tetemeko baba yetu alikuwa kazini ni mbali kutoka pale nyumbani kwetu hivyo yeye hakufikiwa na janga hili la tetemeko.

Aliporudi nyumbani kwetu alikuta hatuna tena makazi yani nyumba imeshabomoka hivyo tunalala tu nje hata chakula hatuna pia tunalala tu na njaa ajabu ni kuwa ametuambia yeye akiwa kama baba wa familia yetu hawezi kutujengea tena nyumba eti tujijengee wenyewe, hata chakula hatoi tena baba yetu kasema yeye eti hana shamba.

Anasema eti kila mmoja katika upande wake abebe msalaba wake mwenyewe.

Sasa familia nzima tunalia jamani baba huyu ni muuaji, hakika anatuua kwa makusudi tena bila huruma.

Huyu Baba sijui kama kwenye kamusi yake kuna neno linaloitwa "UTU WA BINADAMU."

Anayesema tuache kulialia na tusimame wenyewe jibu anatoa Dr. Martin Luther King JR. ni hivi,
MLK: A Bootless Man Cannot Lift Himself By His Bootstraps.
 
Huyo baba yako ni baba mzuri anakufunza kujitegemea ili kesho na keshokutwa akiwa hayupo uwe mwanaume ngangari.Hivi siku zote ulikuwa unamsubiri bila hata kufanya chochote kweli?Asingerudi je?Jiongeze mkuu
 
Ni wajibu wake kuitunza familia mkuu halafu King anatufundisha kuwa
MLK: A Bootless Man Cannot Lift Himself By His Bootstraps.
 
Heri sana ya mwaka mpya!

Nyumbani kwetu tulipatwa na maafa makubwa ya tetemeko la ardhi, kwa uzito wa tetemeko lile nyumba yetu ilianguka na kuharibika vibaya na tulipoteza baadhi ya ndugu kwenye familia yetu hawa ndugu zetu walifariki dunia.

Wakati wa tetemeko baba yetu alikuwa kazini ni mbali kutoka pale nyumbani kwetu hivyo yeye hakufikiwa na janga hili la tetemeko.

Aliporudi nyumbani kwetu alikuta hatuna tena makazi yani nyumba imeshabomoka hivyo tunalala tu nje hata chakula hatuna pia tunalala tu na njaa ajabu ni kuwa ametuambia yeye akiwa kama baba wa familia yetu hawezi kutujengea tena nyumba eti tujijengee wenyewe, hata chakula hatoi tena baba yetu kasema yeye eti hana shamba.

Anasema eti kila mmoja katika upande wake abebe msalaba wake mwenyewe.

Sasa familia nzima tunalia jamani baba huyu ni muuaji, hakika anatuua kwa makusudi tena bila huruma.

Huyu Baba sijui kama kwenye kamusi yake kuna neno linaloitwa "UTU WA BINADAMU."

Kwa kwlei poleni sana na hilo janga. Ni kubwa mno na halielezeki. Mungu atusaidie. Lakinin naomba unisaidi kidogo kwa ajili ya ufahamu. Hilo tetemeko lilitokea likaangusha nyumba na miundo mbinu kiasi cha uharibifu mkubwa. Zaidi sana kinachotia huzuni ni maisha ya watu yaliyopotea, maumivu na mateso mengine. Je chakula cha familia kiliathirikaje na hilo tetemeko? Kilifunikwa kabisa na hapakuwa na uwezo wa kukiokoa? Poleni sana!.
 
Ni wajibu wake kuitunza familia mkuu halafu King anatufundisha kuwa
MLK: A Bootless Man Cannot Lift Himself By His Bootstraps.
Ni wajibu wake kuitunza familia lakini akiwa hayupo na familia lazima iendelee sio kubweteka tu kisa wanamsubiri baba .....nope
 
Kwa kwlei poleni sana na hilo janga. Ni kubwa mno na halielezeki. Mungu atusaidie. Lakinin naomba unisaidi kidogo kwa ajili ya ufahamu. Hilo tetemeko lilitokea likaangusha nyumba na miundo mbinu kiasi cha uharibifu mkubwa. Zaidi sana kinachotia huzuni ni maisha ya watu yaliyopotea, maumivu na mateso mengine. Je chakula cha familia kiliathirikaje na hilo tetemeko? Kilifunikwa kabisa na hapakuwa na uwezo wa kukiokoa? Poleni sana!.
Asante sana yani mali zote za familia zimeharibika na hata chakula hakikusalimika sasa tumekata tamaa ya kuendelea kuishi.
 
Watu tuna matatizo hapaa tukianza kuyaelezea matatizo yetu hapaa utakimbia
We vaa uhusika tu kwanza wa janga hilo la tetemeko halafu nambie unajiskiaje?
Hivi unafikiri majanga kama tetemeko, mafuriko, baa la njaa ni vitu vya mchezo mchezo eti!
Kiasi kwamba yule mhanga anaeza akasimama peke yake haraka haraka tu tena kwa urahisi sio, omba sana yasikukute ndugu sikia tu kwa wenzako.
 
Ni wajibu wake kuitunza familia lakini akiwa hayupo na familia lazima iendelee sio kubweteka tu kisa wanamsubiri baba .....nope
MLK: A Bootless Man Cannot Lift Himself By His Bootstraps.
 
Una smart phone mkononi unapost JF halafu bado unamlaumu babako yule ni mwanaume nwenzako man wenzio tulianza kufikiria kujitafutia kama kinda enzi sana huyo mzee anawakuza akaze tu
 
Duh...poleni halafu nasikia Huyo baba yenu kaomba na kupewa misaada na vijiji jirani...nadhani jatia ndani yote...mbaya saana....
 
Asante, huyu baba misaada mingi alipewa na wasamaria waloguswa na janga hili lakini yote ameibinafsisha.
Eti tukihoji anakuwa mkali kama mbogo.
 
Tatizo la baba yako naona ni mkweli mno, hata msibani hasiti kusema marehem kafa kifo cha kizembe, hakuwa makini barabarani.

Ni hii tu kawaida yake.basi anaonekana kama ninja.
 
Back
Top Bottom