Shoctopus
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 3,434
- 1,985
Tangu Uhuru Tanzania haijahuisha ILO Conventions za kima cha chini cha mshahara! Matokeo yake ari na productivity ya mfanyakazi wa TZ inazidi kushuka hasa wa kima cha chini wakati huohuo wengi wao wanafanya lolote (kumwibia mwajiri) ili kuziba pengo ili waishi. Hii imeunda utamaduni wa kinafiki na ufisadi ngazi zote za ajira rasmi zenye nguvu kisiasa. Ndio hawa ambao wamejivika koti la ukada na/au uhafidhina ili mambo yabaki yalivyo (status quo).
Kundi kubwa la 'wahafidhina' hawa ndio waliteuliwa ujumbe wa BMK kuiponda rasimu ya Katiba mpya ya Warioba.
Nirudi kwenye mada. Umasikini ni umasikini, hauna itikadi, uwe CCM au UKAWA. Kwanini tusikubaliane kama Taifa kwamba mtu mwenye kipato chini ya T. Sh. x kwa mwezi au mwaka ni masikini. Hili liwe Lengo Kuu la Taifa na sera na mipango yote ya maendeleo ijikite hapa.
Tukikubaliana hivi tutaweza kumlenga MTU au FAMILIA badala ya miradi mikubwa ya magorofa na nyumba za mikopo isiyomnufaisha mlengwa.
Unapomkata kodi kubwa na michango ya akiba ya uzeeni, bima za afya kwa yeye mwenyewe na mkewe, mtoto/watoto; mtu ambaye ambaye mshahara wake haukidhi mahitaji take muhimu ya mwezi au mwaka (unamfukarisha) halafu umpe mafao/akiba yake baada ya kufikisha umri wa miaka 55/60 (kwenye nchi ambayo life expectancy ni 50 yrs) ni mauwaji tu!
Ndio mana hatuwaelewi mnaposema nchi hii ni tajiri wakati Sera zenu zinawafukarisha wananchi na kuwaneemesha wageni, kwa njia hii HATUFIKI!
Ukisha waneemesha wafanyakazi wa kima cha chini uaongeza soko la mazao ya mkulima na mfugaji unawawezesha watu hao kusomesha watoto wao na kupitia uwezo wao kimapato serikaIi itakusanya kodi zaidi na itaelekeza bajeti katika miundombinu, elimu, ulinzi nk.
Muwe na makubaliano kwenye mambo ya msingi ili muepuke kurudiarudia au kubadilisha sera kila mara kwasababu za eti itikadi za vyama tu! Huku mkulima na mfanyakazi wakigharamia malumbano yenu yasiyo na tija. Hebu fikirini mlivyotumia mwezi mzima kwenye BMK (watu 600+) kubishana juu ya kura ya siri au ya wazi! Mkilipwa malaki kila mmoja wenu kwa siku! Mwisho wa siku mkalamba mabilioni ya wanyonge mkakubaliana 'kunyonga' midomo yao kupitia Katiba ya Warioba! Ni unafiki wa kukufuru. HAMKO SERIOUS na dunia nzima inawashangaa.