Huwa wanajisiakiaje wakiona hivi ?

Huwa wanajisiakiaje wakiona hivi ?

joka57

Senior Member
Joined
Aug 29, 2014
Posts
138
Reaction score
49
halima6.jpg

MIEZI michache baada ya mbunge wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA), kumlipua bungeni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka, akidai anamiliki maelfu ya ekari za ardhi katika maeneo mbalimbali nchini, safari hii amemfuata jimboni kwake Muleba Kusini na kuahidi kula sahani moja ili kuhakikisha anarejesha ardhi ya wananchi anayodaiwa kupora. Mei mwaka huu, Mdee ambaye ni Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alirusha kombora hilo bungeni wakati akisoma maoni ya kambi hiyo kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka wa fedha 2014/2015.

Mdee, alisema Waziri Tibaijuka ana maslahi makubwa katika sekta ya ardhi ambapo anamiliki kiasi kikubwa cha ardhi maeneo ya Kigamboni na Kagera wilayani ya Muleba ambako katika eneo la Kyamnyorwa ana hekta 800.
Akihutubia mkutano wa hadhara huzi, katika Kata za Kasharunga, Bungangunzia na Muleba Mjini jimboni Muleba Kusini linaloongozwa na waziri huyo, Mdee ambaye
pia

ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA), aliahidi kula naye sahani moja mpaka arudishe ardhi anayodaiwa kuipora kwa wananchi wake hekta 2,000. Mdee aliwataka wananchi hao kuhakikisha wanachagua viongozi wa CHADEMA katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Desemba 14, mwaka huu, ili iwe rahisi kusimamia urejeshwaji wa ardhi yao kupitia vikao halali vya kijiji.

Alisema kuwa kwa mujibu wa sheria namba tano ya ardhi ya mwaka 1999, hairuhusu serikali za vijiji kutoa zaidi ya ekari 50, hivyo kwa jambo alilofanya Prof. Tibaijuka si tu kuwa amewadhulumu bali pia amevunja sheria za nchi.
"Jimbo hili lilitakiwa liwe mfano wa kuigwa nchini kutokuwa na migogoro ya ardhi, kwa kuwa mbunge wenu amepewa dhamana ya kusimamia ardhi, lakini jambo la kushangaza ndilo linaongoza kwa kuwa na kero kubwa za uporwaji wa ardhi.

"Hili la uporwaji wa ardhi ya wananchi wa Muleba hekta 2,000 nitaenda kumlipua bungeni kwenye Bunge la Novemba…kama Waziri Kivuli wa
Ardhi nitahakikisha nakula sahani moja na mbunge wenu mpaka awarudishieni ardhi yenu," alisema Mdee huku akishangiliwa.

Awali, wananchi hao walimweleza Mdee kuwa mbunge wao ameshindwa kusimamia ipasavyo mfuko wa jimbo hali inayofanya fedha kulundikana bila kufanyiwa kazi wakati zingeweza kutumika kumaliza changamoto lukuki iyowakabili ikiwemo ujenzi wa maabara wa shule za kata.

"Ameshindwa kutatua mgogoro wa kituo cha afya Nshamba, kuhusu ardhi na kusababisha kushindwa kujengwa kwa nyumba za madaktari na vyoo vyakutumia wagonjwa," walisema wananchi katika taarifa yao kwa Mdee.
Prof. Tibaijuka hakupatikana kujibu tuhuma hizo kutokana na simu zake za kiganjani kutopatikana kwa siku nzima ya jana.

Polisi wazui mikutano
Katika hatua ya kushangaza, Jeshi la Polisi wilayani Kyerwa, limewatawanya kwa mabomu ya machozi, wananchi waliojitokeza kumlaki Mdee wakati alipofika kusaini kitabu cha wageni kwenye ofisi za chama wilayani humo jana.

Jeshi hilo, lilitangaza kufuta kibali cha mikutano yote ya mwenyekiti wilayani humo kwa madai ya kupata taarifa za kiitelijensia kuwa hakutakuwa na usalama.
Katika hatua ya kushangaza, jeshi hilo lilitoa kibali cha kuruhusu mikutano hiyo lakini saa saba usiku wa kuamkia jana, lilipelekea taarifa ya kuisitisha nyumbani kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya.

Kama vile kulikuwa na shinikizo la kisiasa, polisi walifyatua mabomu ya amchozi hovyo kwa ajili ya kuwatimua wafuasi wa CHADEMA waliokusanyika kumlaki Mdee katika ofisi za chama zilizopo kijiji cha Kwarukwazi Kata ya Isingiro, saa 9:00 alasiri.
Kabla ya Polisi kuanza kurusha mabomu yao, Naibu Katibu Mkuu wa BAWACHA Taifa, Kunti Yusuph,aliwatangazia wananchi juu ya kusitishwa kwa mkutano huo, kwamba Mdee asingeweza kuzungumza nao na kuwataka wanawake waliojitokeza wakakutane katika kikao cha ndani kwenye shule ya Sekondari Ndagala.

Wakati viongozi hao wakijiandaa kushuka nyuma ya gari walilokuwa wamepanda kwa ajili ya kuondoka, polisi wakiongozwa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD), Pius Paul walianza kufyatua mabomu ya machozi.

Hatua hiyo iliibua taharuki kwa wananchi na kulazimika kukimbia hovyo kujificha kwenye nyumba zilizokuwa jirani na eneo hilo na hivyo kusababisha mkutano wa ndani uliokusudiwa kuwakutanisha wanawake kutofanyika.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya tukio hilo, Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Kyerwa, Deus Rutakyamilwa, alisema kuwa Oktoba 25 mwaka huu, waliwataarifu polisi kwa barua kuwa Mdee atafanya mikutano ya hadhara na wakaruhusiwa kuendelea na mikutano hiyo kwa siku walizoomba.


Chanzo: Tanzania daima

 
Udhalimu ni udhalimu tu wakati wote hata kama atakayekuwa anasababisha udhalimu huo ni mtu mwenye taswira nzuri kijamii, na ukweli ni ukweli daima hata kama utapingwa na wadhalimu wote...aluta continua!
 
Kila kiongozi ccm ni mwizi... mara 1b kapewa na iptl.... polisi wanashupaa kulinda ufisadi na mafisadi wakati wao wanaishi kwenye vibanda vya mabati, mshahara kiduchu....
 
Huyu teja wa kinondoni ndiyo mnalinganisha na prof. kweli nchi hii tu malimbukeni wa siasa
 
Udhalimu ni udhalimu tu wakati wote hata kama atakayekuwa anasababisha udhalimu huo ni mtu mwenye taswira nzuri kijamii, na ukweli ni ukweli daima hata kama utapingwa na wadhalimu wote...aluta continua!

Unalazimisha kumtafutia mtu udhalimu? Mungu hapendi hivyo
 
...ipo siku awe mama yangu,baba yangu ilimradi ni ccm nitamlenga
 
UTAFITI - TIBAIJUKA NDIYE waziri MBOVU KULIKO WOTE TANGU NCHI HII IPATE UHURU .
 
Back
Top Bottom