Msema yote
JF-Expert Member
- Mar 19, 2013
- 448
- 301
Wakuu tukiwa tunaendelea na wikiendi, mwenzenu usiku huu nimekumbuka mbali sana baada ya kusikia wimbo wa Chicco -Ineed some money,
Nimekumbuka miaka ya tisini na kitu huko Tarime - Mara, Tanzania Babu yangu (RIP) aliikuwa akiupenda sana wimbo huo, kwa hakika nyimbo zinakumbusha mbali, kuna wakati alikuwa akiimba.
Pia unanikumbusha hukohuko Tarime shule moja ilikuwa jirani na CMG karibu na mto wenye mti mkuubwa ukiwa unaenda hospitali ya bomani ilikuwa ni academy ya kizungu miaka hiyo ya tisini kulikuwa na mwalimu aliitwa LAWI (sielewi yuko wapi kwa sasa) alipenda kuwaimbia wanafunzi wimbo huu
kwa hakika sukrani za dhati zimwendee mgunduzi wa muziki kwani aligundua kitu kinachoweza fanya ukakumbuka vingi sana.
Vipi ninyi wakuu nyimbo zipi zinawakumbusha wapi na mnakumbuka nini?
NB. Yamkini wapo wataokumbuka majonzi, poleni sana kwa hilo lakini ni vizuri mkachangia ili tupate burudika sote kwa nyimbo za kila mmoja kwani wenda wimbo wako ambao ni huzuni ukawa kumbukumbu ya furaha kwa mwingine na kufanya siku hii ya leo kupitia uzi huu kuwa ya furaha kwako na kwetu sote kwani mwishao utaamini ya nyuma yalitokea ili leo itimie, yalitokea ili leo uwe ulipo, yalitokea ili upate faraja tumaini na nguvu ya kufika mbali zaidi. Lengo si kukumbushana machungu bali kuburudishana kwa kumbukumbu zilizosababisha tufike leo tulipo.
Tafadhali. Majungu, kejeli si mahala pake tuchangie kistaarabu, kwa maana ni kiendi hivo yatupasa kupumzika, kujiliwaza na kufurahi kwa maana hiyo haitakuwa ustaarabu ukikosa ustaarabu
Karibuni .

Last edited by a moderator: