Huu utaratibu wa Viongozi kuwaajiri watu wenye Ubunifu na Ujasiri unaua maono!

Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
11,634
26,373
Wakuu,

Miezi kadhaa iliyopita alijitokeza shujaa Majaliwa Mvuvi aliyethubutu kuwaokoa watu kutoka kwenye ajali ya Ndege iliyotumbukia baharini kwa kufanikiwa kufungua mlango wa ndege na kuanza kuokoa watu.

Mara baada ya taarifa zake kusambaa serikali ikatangaza kwamba aajiriwe jeshi la Zimamoto na uokoaji.

Jana iliripotiwa taarifa ya Mariamu Mwakabungu mwanamke aliyeamua kujitolea kuwaokoa watoto njiti na wale waliotelekezwa na mama zao kwa kuwapa huduma ya bure kuwakumbatia kwa ajili ya joto(Kangaroo mother care).

Mara baada ya taarifa zake kusambaa,ikatolewa taarifa kwamba rais amemzawadia Tshs Milioni mbili kama zawadi na tayari Waziri wa afya ameagiza mwanamke huyo kupewa ajira ya muda hapo na amemshauri asome ili apate Cheti cha form four ili akasomee Uuguzi(Nursing).

Kutambua mchango wao na kuwapa pesa za pongezi ni jambo jema lakini,Kitendo cha kuwaajiri au kuwaingiza kwenye mfumo wa ajira serikalini ni kuua maono na vipaji wa hawa watu.

Kwa upande wa huyu Mwanamke,serikali ilipaswa impe mafunzo zaidi tu ili abobee kwenye kitu alichopenda(Kangaroo care) na ikiwezekana awezeshwe kuanzisha kituo cha kutoa huduma hizo ambacho kingeweza kuwahudumia watoto wengi zaidi kupitia watu watakao kuwa wanajitolea,Faida yake ni kwamba kwanza itawasaidia watoto wengi,pili itahamasisha kujitolea kwa watu kikubwa zaidi huyu mwanzilishi atafanya kazi ya maono yake ambayo ndio anaipenda.

Sasa,hata baadae akiajiriwa kuwa Muuguzi(kama atapata cheti),kwanza atahudumia watu wachache sana kwa nafasi yake ya Muuguzi,pili sidhani kama atarudishwa tena kwenye kangaroo maana hakuna atakayekumbuka tena,kama mnavyojua teua tengua Viongozi wanaweza wasiwepo hawa waliopo sasa.

Kwa upande wa Majaliwa yule alikuwa mvuvi jasiri hivyo angewezeshwa kuvua kwa boti na vifaa vya kisasa vya uokozi au kufuga samaki kwa njia za kisasa ili aisende mbali na maono yake.

Kumpeleka Jeshi la zimamoto kwa vigezo(Qualifications)zake kweli atapata ajira ya kujihudumia yeye labda na familia yake lakini kama angebaki kwenye kazi ya maono yake na aliyozoea basi angejiajiri na kuajiri wengi pia.

Kwahio nashauri Viongozi mnapoona wabunifu wamejitokeza waulizeni kwanza wanataka wafanyiwe nini na serikali?kuwapa ajira hawawezi kukataa kwa sababu ya shida walizonazo na pia maagizo haya hutoka kwa Viongozi wakubwa wa kitaifa ila kama mkiwapa machaguzi pengine wasingetaka kuwa huko mnakowapeleka.

Ahsante.
 
Back
Top Bottom