banned do
JF-Expert Member
- Apr 27, 2017
- 574
- 506
Msanii akitoa wimbo mpya ukapata promo ya kutosha kila mtu anamdandia.Wimbo ukichuja wanatafuta mwingine mwenye kick.Pia wanamuziki wa Bongo hawana uhakika na maisha yao ya sanaa kwa sababu mashabiki wa bongo ni mutual fans au sigara kali.Shabiki wa Mr.Blue anaweza kuwa shabiki wa Darasa pia wa Diamond at the sametime ni shabiki wa Wema na Wolper wakati huohuo anashabikia taarabu na muziki wa Dance.Hii hali inafanya wanamuziki wa Bongo kukosa fanbase ya uhakika ma kufanya wasiwe na uhakika na kazi zao.Kama msanii anakuwa na mashabiki wa kudumu ni vigumu kubabaika na kuanza kubuni aina nyingine ya muziki tofauti na muziki alioanza nao.Mfano Brother Juma Mchopanga,Songa na wengineo wamesukumwa na upepo wa hali iliyopo na kuamua kuwatafuta mashabiki walio nje ya Muziki waliokuwa wakifanya hapo awali.Sidhani kama wangeweza kutoka pale walipokuwa kama wangekuwa na mashabiki wenye msimamo na itikadi kama wale mashabiki wa Tamaduni Muziki.Nadhani ndio maana Niki Mbishi na Nash wanalazimika kuwa pale walipo kwa sababu nyuma yao wana idadi ya watu inayowashinikiza kufanya Muziki ambao wamekuwa wakiufanya toka awali.Ushuri wangu kwa mashabiki wa Muziki Tanzania ninawaomba wawe na msimamo juu ya aina za Miziki ili kila muziki uweze kuwa na mashabiki wake.Hii itasaidia hata kuleta changamoto.Haya ni yangu binfsi mwenye maoni yoyote yale hata yaliyo kinyume anaruhusiwa kutoa.Mungu wabariki.