Huu usajili wa Catherine Ruge unaleta Utata kwa wengi

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
4,582
2,783
^911956F44D0DBBFC58B375AEA87F8AA98C9415D439E2065F86^pimgpsh_fullsize_distr.jpg
^327C8C8B8403756E5449E2E112F2FD0042C3E997C2C41B9D21^pimgpsh_fullsize_distr.jpg
^CC13FA46CC81F51219C397B575FA77EF994A984D6FCDA91A0E^pimgpsh_fullsize_distr.jpg
^8D18EFE4C3C9655D59FFFAA98867F888627425603A72DF84EA^pimgpsh_fullsize_distr.jpg
^B7DC282B8CDB021A5B54178D2C1E3AEEA82FF5D1700722F3DC^pimgpsh_fullsize_distr.jpg
^5984E88F79A478CA30874DC3B3314E4798315FB50C2FB1AE30^pimgpsh_fullsize_distr.jpg

Wakuu,

Kuna watu wanasema kuteuliwa wa Catherine Ruge kuingia katika Bunge la JMT, Dodoma, haujazingatia vigezo. Wengi wanasema yule si kilema, kwanini CHADEMA wasiweke kilema kuwakilisha vilema kuchukuwa nafasi ya marehemu aliyekuwa Mbunge mlemavu?

Wengi wanasema yawezekana ulemavu wa binti huyu unajulikana kwa wakubwa tu, ndo maana wamekuwa vipofu wa kufanya maamuzi yatakayokuwa na tija kwa taifa.

Sisi kama GT tunasemaje?

Hapa nimeona mambo yake. Ni kweli kilema chake wanajua wakubwa tu?
 
Uelewa elimu elimu elimu,ubunge wa viti maalum unachaguliwa na NEC kwa vigezo wanavyozingatia....na hakuna ubunge viti maalum ulemavu;hapana.viti maalum kikatiba ni viti ambavyo vipo kikatiba kuleta usawa wa kijinsia ubungeni.....mama elly macha akuchaguliwa kwa sababu ya ulemavu wa macho bali she was an educated woman,alikuwa daktari (PhD) hata Mh Ruge ameteuliwa kwa sabab ni msomi pia PhD candidate km mulikuwa hamujui.Kwa hyo chama cha siasa kipindi cha uchaguzi wanapeleka majina ya wawania viti maalum kwa ujumla wake kwa wale waliofanikiwa kuwa wawakilishi kugombania viti maalamu na hapo listi ya wawania inachukuliwa na NEC baada ya uchaguzi vyama vinagaiwa viti kulingana na uwiano wa wabunge wateule na vigezo ndio uchekecha na wa kumchagua na nani wa kumuacha na hii kazi ya ukechaji inafanywa na NEC wenyewe kwa wered na ufanisi.
 
Unapokuja na uzi andaa hoja sahihi za kuutetea. Usiongozwe na hisia hasi kila muda. Kwa namna hii ya uwasilishaji nyuzi kutakuwa hakuna tofauti ya mjuvi wa mambo na kuwadi wa habari. Vilevile hoja kama hii iliisha jadiliwa katika nyuzi zingine. Tuwe makini.
 
Nadhani mtoa mada ameangalia social life ya Mbunge mteule lakini huyu Dada ni mpiganaji kweli kweli ambaye anapigana sana na kuhakikisha wanawake wananyanyuka kiuchumi.

Na ni balozi Mzuri sana kupitia Umoja wa Mataifa ktk Woman empowerment.

Hizo post zake na picha zake ni social life tu wala si kigezo cha tabia mbaya wala kutokuwa makini na majukumu yake inategemea amekulia ktk familia za maisha yapi!!
 
Ufipa -kinondoni, hii mada ina ukakasi Sana.

Kwanza, NEC ndiyo inayochagua hao Wanawake wa viti maalum kama pana aliyefariki.

Pili, nafasi hiyo siyo kwa vigezo vya KE awe mlemavu

Tatu, watu wote hasa Wanawake kuwa katika siasa haina maana kuwa maisha yao ya mahusiano , mapenzi hadi ngono husimama la hasha. Bali hufanyika kwa heshima na nidhamu. Sababu, siasa haiwabadilishi kutokuwa na hisia za kiutu.

Tatizo lako, umejaa USHILAWADU!! , ndiyo maana ukaleta hizo SMS za Ms. Ruge na kuziwekea maneno yako machafu.

Nne, mbona huleti picha za wanaume wanasiasa wanaofanya ufukusa na ulevi. Au hujui kuwa nao ni wachafu zaidi,!?

Tano, hakika umewakosea sana Wanawake wote kwa uzi huu tena ni unyanyasaji wa kijinsia ulioufanya hapa wa kumdharau huyo Ms. Ruge.

Halafu, tambua hakuna msafi kwenye hii Dunia ya Mungu: Yenye vitu vya mzungu koko!!!
 
Back
Top Bottom