Neno "siku hizi" ni kielezi na limewekwa kuonesha nyakati. Pengine mleta mada hakuwa akiyashuhudia hayo aliyoyaona nyakati za kale au hata hajawahi kusimuliwa hayo.
Pamoja na kwamba nafsi yoyote kati ya kike au kiume inaweza kuwa na hulka ya ukatili, lakini tabia hiyo haipendezi haswa ikifanywa na mwanamke tena kwa mtoto mdogo. Wahenga wanasema, "uchungu wa mwana aujuaye mama".